Kabla hamjamshitaki Mbowe kwa tuhuma za ugaidi kamilisheni uchunguzi wa sumu aliyopewa Mangula

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,462
17,291
Naliomba jeshi la polisi likamilishe uchunguzi wa nani alimpa Mangula Sumu na ni nani aliemshambulia Lisu kwa risasi ili wote wajumuishe kwenye mashtaka ya kuua viongozi na ugaidi kama mnavotaka kufanya Kwa Mbowe!

Huku mtaani kuna tetesi zinazagaa kuwa Mama umesimamishwa Uongozi wako na Jeshi ndilo linaongoza nchi!Naanza kuamini kwasababu Tangu awamu ya tano mmewafundisha Watanzania kuvunja katiba nashukuru na jeshi limejifunza udhaifu huu ndio maana Upinzani unaminywa tena kwa kuvunjwa kwa sheria za nchi!

Mama hakufundishwa hiki tunacho kiona kuna watu wanafanya lao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
 
Ni wiki ya Mbowe na katiba mpya.

Asante Samia kwa kutuambia tunaleta chokochoko.

Tunasubiri mkwara wako mwingine.

Ukali hauigwi, be your normal motherly self.
 
Hivi yule mlinzi wa mh.Tundu Lissu amejisalimisha POLISI kwa mahojiano zaidi?!!!

Miaka inakatika SASA....
 
Hivi yule mlinzi wa mh.Tundu Lissu amejisalimisha POLISI kwa mahojiano zaidi?!!!

Miaka inakatika SASA....
Na zile CCTV camera alikuwa nazo mlinzi wa lissu?? Kipindi lissu anashambuliwa yule mlinzi au dereva wake alienda Kung'oa zile CCTV camera?? Halafu yule mlinzi ndiyo aliyoamuru wale walinzi wanaolinda yale nakazi ya viongozi kwa siku ile wasiwepo lindo?? Nafikiri tungeanza na haya kwanza
 
Waliotaka kumpa sumu Mangula kama unawafahamu nenda polisi katoe ushahidi wako ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Waliompiga Lisu risasi chadema na dereva wa Lisu wanaijua hiyo ishu ndio maana wamemficha dereva ili asije akakamatwa akahojiwa na baadae wahusika kujulikana, mpaka hapa hakuna ubishi kuwa ishu ya Lisu imekaa kichama zaidi ndio maana Mbowe na genge lake walikimbilia kumficha dereva.

Kuhusu raisi Samia ki ukweli alijitahidi kuonesha utu wa kutaka kushirikiana na wapinzani, lkn wapinzani wa Tanzania hawana utu. Wameitumia nia hiyo ya mama kujaribu kumkwamisha kwa kuanzisha mambo yasiokuwa na tija, mara operetion haki, mara tutamnyoa na wembe tulionyolea mtangulizi wake, mara wapange maandamano ambayo hata hivyo jeshi la polisi lilipiga marufuku, mara sijui walazimishe katiba nk.
 
Naliomba jeshi la polisi likamilishe uchunguzi wa nani alimpa Mangula Sumu na ni nani aliemshambulia Lisu kwa risasi ili wote wajumuishe kwenye mashtaka ya kuua viongozi na ugaidi kama mnavotaka kufanya Kwa Mbowe...
Sumu walipeanana wenyewe huko huko kwenye mAkorido yao, Samia karithi tabia zote mbovu mbovu za Magufuli
 
Back
Top Bottom