Kabisa naibiwa hivi hivi na Airtel, Nimeona niseme tu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,742
Nimekuwa nikitumia mtandao wa Airtel kwa muda mrefu sasa. Lakini siku za hivi karibuni nimegundua kama Airtel wamekuwa si waaminifu katika uhusiano wetu.

Airtel they are cheating. kuna kifurushi huwa najiunga cha GB1 uishaji wake umekuwa wa kushangaza sana. Kiasi najiuliza why airtel wanifanyie hivi hata mimi ambaye nimekuwa mteja wao wa muda mrefu?

Inawezekana kabisa nikawa sijaangalia videos au kutumia sana internet but soon inakuja meseji yao kuwa nmetumia asilimia 90 za bundle.

Najiuliza nimetumia wapi hizo data? Hakuna kitu ambacho ngesema maybe nime download pasipo mimi kujua au nme update. No, i know how to manage my phone.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana kwa hii mitandao ya simu kwa wizi wanaotufanyia sisi wateja Mpaka natamani ngeeenda kuishi tena USA au Canada kule hawana wizi wa namna hii.

Nchi za kiafrika ni shida sana.nmepita pita nchi za wenzetu internet si gharama kama huku.hili jambo serikali ya kikwete ilisema kwa kuleta mkongo wa taifa tungekuwa na ahueni.

But kama kawaida Wanasiasa na ahadi ni ndugu ila utekelezaji na Wanasiasa ni mbingu na ardhi.
 
Hamia halotel kitu mwaaa unateleza Kama upo kuzimu mpaka raha..
Nawapigia cha puo kwa maana siendi mbio,situmii bando za chuo kwa maana sina kituo..
Halotel baba lao hivyo vishekeli vikalale kwao😅

NB:silipii tangazo atakae mind ajue ye ni ka kenge😜
 
  • Thanks
Reactions: amu
Nkajua umeibiwa TV na kibaka Kumbe bando?😂 dawa yao hamia mtandao mwingine kwan sh ngap? si buku tu?
 
Walio wekeza huku africa si hao hao wa usa na canada nk ,

kIongOzI Wa BaaDae
 
Hata voda nao wanafanya huu ujambazi, unakuta 1gb inaisha kwa kuperuzi twitter ndani ya nusu SAA tu wakati hapo kabla nilikuwa nakaa nayo wiki nzima
 
Ingia kwenye data usage uone app inayotumia zaidi mb
Screenshot_20200517-094001_Settings.jpg
 
Mkuu kuea kama mimi tu nimeshakubali kuibiwa na siku wasiponiibia nitawakumbusha tu.
 
Airtel wamekuwa wahuni sana, wanafanya wizi wa vifurushi vya internet bila hata kujali. Kuna mtu kaweka kifurushi cha internate 8GB trh 2/6/2020, leo trh 4/6/2020 kifurushi kimeisha, matumizi yake ni ya kawaida. Miezi kama miwili hivi iliyopita alikuwa anaweka kifurushi cha 5GB na matumizi yake yalikuwa ni makubwa kulinganisha na sasa, alikuwa anaweza kukaa na kifurushi hicho wiki 3, lakini hiki cha 8G kimeisha ndani ya siku 3, imenishangaza sana, au ndo ile tunasema " It is impossible to make some one better off without making some one else worse off"
 
Hawa jamaa ni wezi wa kupindukia. Week imepita nimenunua GB 12 saa 2 Usiku kufika saa 5 hakuna bundle. Nikaenda airtel blanch wakaangalia kwenye madude yao wakasema tunalifanyia kazi tumetuma e-mail sijui wapi. Nenda tutakupigia simu. Nikaondoka lakin sikuwa na bundle jingine wala hela ya bundle. Ilikuwa alihamis nikakaa mpaka jumamosi Kimya. Nikaamua nipige customcares, Ndio ngud tumeona ulinunua bundle na halipo kwenye matumizi. Leo hatufanyi kazi mpaka siku za kazi. Jumatatu nikapiga tena. Wakanipa number za mtu gani sijui. Nikamchek, jamaa kasema tunaangia kesho Piga simu mida ya mchana. Leo nikapiga tena wameniambia kesho nipige tena. Hii na mara ya pili kuibiwa na mpka nilisajili line mpya. Mwanzo ikawa Powa lakin siku zinavyozidi na mateso mno.
 
Back
Top Bottom