Hizo Enda..... mbona nyingi zina maana gani?
Wairaqw ni wengi mno. Idadi yao inakadiriwa kuwa zidi ya millioni mmoja.Wengi sasa wamehamia Loliondo, Iramba, Kondoa, Dodoma, Kiteto, Kilindi n.k., huko hakuna DAA"WI[/QUOTE
Kupotea kwa kabila kunaweza kukatokea but baada ya kipindi kirefu sana. Pamoja na mambo mengi swala la watu kuoa au kuolewa nje ya makabila yao na si tu Wairaqw inachangia. Pia tusisahau kuwa watu huhama na kuhamia. Maeneo ambayo zamani yalikaliwa na kabila moja tu leo yanakaliwa na makabila mengine-mfano mzuri ni wasukuma na wadatooga waliohamia kwenye bonde la mto rufiji na kuanza kufuga ingawa haikuwa jadi ya watu wa pwani kufuga. Leo hii hawa nao wanajulikana na wanajiita kama warufiji.
Kuhusu daawi-haiwezi changia kabila kuondoka hata cheme actually inaweza saidia kabila kukua kwamfano-swala la ndugu wa damu kutooana, ukiangalia kwa upana wake pia kama kuna tatizo la katika ukoo fulani kwenye maswala ya uzazi basi kwa kuoa nje ya ukoo hili tatizo linakuwa limekwepeka kwa kiasi fulani.
Kwa ufupi tu Wairaqw wako zaidi ya 500,000 na ukijumlisha waliochanganyikana na wabondei wa Tanga, na waliohamiakwingineko wanaweza fikia kwenye 700,000 lakini millioni ni idadi kubwa mno.
Ila wadada zao wazuri kama wale wa Singida ila sasa kwa Mgao duu kama Dawasco!
bora wapotee tu kwanza hawana asili ya tz wana asili ya huko huko iraq
Pamoja na sababu hiyo, kabila la ki-Iraqw ni wengi sidhani kama litapotea. Ukianzia Karatu, Daudi, Masieda, Bargish antsi, Arri, Mbulu mjini, Anslay, Gehandu, Gedamar, Titiwi, Kwermusl, Khaday, Kainamu, Nahasey, Tsaayo-raat, Hayloto, Murray, Qwam, Kuta, Siday, Tlawi, Masqaroda, Diyomati, Bashay, Dongobesh, Tumati, Mongahay, Endoji, Bashnet, Gidhim, Maretadu, Gibdiyo, Gidmadoy, Gidarudadaw, Simhha, Haydrer, Semonyandi, Mewadani, Musru, Endagikot, Endaharghadakt, Endamasaki, Endamilay, Endanachan, Endanyawish, Erboshan, Ngw'andakw, Yarotamburda, Qatabella, Qamatananat, Qambush, Datlaa, Dumanangw, Endagew, Muguruchan, Maghang, Haydom mpaka kule Murkuchida ni wao tu. Pia kule Yaeda chini na Mungowamono kwa Wahadzabe wapo wachache.
Ni kweli kabisa Mkuu DA'AWI inatutafuna vibaya, Ukiacha kabila kupotea, Ukweli ni kwamba Asili au tamaduni zimeshapotea, Maeneo mengi vijana wamechanganyika sana, ni sehemu chache sana ambazo bado wanaheshimu mila na tamaduni. Sehemu kama Iriqwada'au kule milimani maeneo ya Mbulu ni kati ya sehemu chache ambazo bado hazijaharibika. Kuhusu DA'AWI ngoja tuwasubiri akina Afrodenzi, dena Amsi na wengine watueleze vizuri.
Hivi jamani Wairaq si ndio hao hao Wambulu? Yaani akina Slaa. Nadhani kuna mambo wanayotofautiana kutokana na upande wanaotoka au imani kalina lugha yao ni moja, hebu nielewesheni!
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni. na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe. Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine. Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako. Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.
hivi slaa kumbe ni mwalabu wa Iraq???? CHADEMA KUMBE NDIYO INAYOTAKA KUWARUDISHA WAALABU , HII HATARI
Naas loale!!..karibu Batosu ziwani!!
Uendelee hadi Endalaqanet,Dareda, Maganjwa, Masqaroda, Gudedesh, Endasak, Nangwa, Giting, Sabilo, Basoduqwang, Endagaw,Sigino..............