Ka Mtindo huu Nchi hii kuendelea ni vigumu

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,043
Sijui kwanini kila kitu Tanzania uwa kinafanyika kwa mihemko au nguvu za soda?

Nakumbuka lilikuja suala la usafi ambapo kila Jumamosi watu tulitakiwa fanya usafi na takataka kuwekwa barabarani kisha gari za taka ziwe zinapita na kuuondoa.

Wazo lilikuwa zuri ila tatizo likaja kwamba gari hazipiti uchafu unatapakaa na mwingine kuingia kwenye njia za maji za barabara.

Basi ikabadirishwa ikawa kwamba kila kaya itakusanya uchafu na gari likipita ndipo upelekwe barabarani.
Lakini huku kwetu Tegeta imepita zaidi ya mieizi mitatu hakuna hata gari linalopita.

Nahisi hilii suala lilikuwa kick tu kwisha habari yake.

Tanzania hakuna jambo linaloweza kuwa endelevu uwa mambo mengi nguvu ya soda tu halafu muda ukipita ni business as usual.

Hatuwezi kuendelea katu kwa style hii.
 
Elimu tu ndio shida. Badala ya kutumia mabavu na vitisho ilitakuwa watu waelimishwe ili suala la usafi wa mazingira iwe sehemu ya maisha yao
 
Mkuu hamia kijijin tu unachimba shimo la taka hutokuja tena kulalamikia hilo suala.

pole sana kwa adha hiyo
 
tungepata viongozi wakakamavu huu upuuzi usingekuwepo, viongozi wetu wengi hawakuzaliwa na vipaji vya kuongoza bali upigaji na ubinafsi, unakuta kiongozi kalegeea yaani anatetema kabisa
 
tungepata viongozi wakakamavu huu upuuzi usingekuwepo, viongozi wetu wengi hawakuzaliwa na vipaji vya kuongoza bali upigaji na ubinafsi, unakuta kiongozi kalegeea yaani anatetema kabisa
Tatizo kubwa ni mfumo mpya wa ulipaji wa kandarasi, ulioanzishwa!! Umekuwa na usumbufu, pesa ya eneo husika ikishalipwa iende manispaa, ndio waigawe tena kwa wakandarasi wote, bila kuangalia kuwa imetoka eneo gani?!! Una kuta yule ambaye amekusanya sana kwenye eneo lake, anagawana na wale waliokusanya kidogo/ambao hawajakusanya!! Ndio maana wengi wanashindwa kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom