Ka edit picha yake, matokeo yake kapewa talaka

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,971
35,113
Dada yule alikuwa ame mu add mumewe FB wakawa ni marafiki.
Dada pamoja na mumewe niwatumishi wa umma idara ya afya.
Mumewe akawa amepata safari ya zaidi ya mwezi mmoja humu humu ndani ya nchi.
Yule dada akawa amepost picha kwenye ukurasa wake wa FB, picha ambayo ame ifanyia editing halafu akaandika yuko Mombasa Kenya.
Mumewe kaona ile picha, kumbuka yuko safarini hayuko nyumbani.
Bwana yule baada ya kurudi safari, alimuuliza mkewe Mombasa alienda kufanya nini? Dada kajitahidi kumuelewesha kwamba ni picha tu ame edit, lakini mwanamme anasisitiza kuwa wataalamu wa IT wamemwambia kuwa, itakuwa ni kweli alikuwa Mombasa Kenya.
Dada amefika mbali hadi kumwambia mumewe kuwa akaangalie kwenye daftari la mahudhurio kazini siku hiyo ataona kwamba alikuwa kazini, lakini mzee hataki kuamini kuwa mkewe hakuwa Mombasa Kenya.
Hadi ninatuma huu uzi bidada anatafuta chumba cha kupanga.
:mad::mad::mad:
 
Wanaume limewachoma eeee. Muwe mnatafakari msichukue maamuzi ya haraka haraka. Nimefurahi hii thread nimepata kujua akili zenu mlio wengi, mnakurupuka kama huyo kaka Santana Big Dy
 
Yawezekana jamaa anaamini kuwa alipoenda mombasa watu wameutumia mtandao pendwa wa ti.go na ndio hicho kinachomuuma zaidi pengine.
 
Naona wengi mnamlaumu huyo mume aliyetoa talaka,na nyie wadada muache maisha ya maigizo,una edit uonekane ulikua Mombasa ili iweje? kwanini usiishi maisha unayoishi? huko FB ndio maana sitaki hata kupajua,upuuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom