JWTZ, wafanikiwa kutegua bomu lililokuwa limetegwa visiwani Zanzibar

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,161
1,535
Wakuu saa moja ilopitA kulikua na taharuki kubwa Darajani watu walikua wanakimbia ovyo. Tetesi ni kuwa kuna bomu la kutegwa.

Sasa hivi kuna mshindo mkubwa umesikika sasa cjui kama ndio hilo bomu . Mwenye taarifa atujuze.

UPDATES:
Ni bomu kweli lilitegwa karibu na kituo cha polisi Mkunazini . Kuna clip iko facebook inaonyesha wakati wa kuteguliwa.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar, amesema jana Jeshi la Wananchi kwa kushirikiana na polisi wametegua bomu lililotegwa pale Mkunazini
attachment.php

attachment.php



Wanabodi,

Zanzibar hali tete!. Kuna bomber mmoja, katega bomu eneo la Darajani Zanzibar, kisha huruma kuhusu vifo ikamuingia, akaogopa na kuamua karipoti polisi, polisi nao wakaogopa bomu, wakaripoti JWTZ, JWTZ wakaingilia kati, wakalitegua bomu hilo kwa kulilipua bila kuleta madhara.

Kwa mujibu wa Radio One, Wataalamu hao, wamefanikiwa kulilipua bomu hilo lililokuwa limetengwa eneo la Darajani Zanzibar!.

Kama mambo yenyewe ndio haya, kuna uwezekano wa uwepo wa suicidal bombers!.

Haya yamechangiwa na huruma na udhaifu wa dhaifu!, ingekuwa ni enzi za Nyerere, hakuna mtu yoyote Zanzibarr ambaye angethubutu hata kukohoa!. Leo mtu anajitangazia ushindi halafu bado yupo, anaachwa tuu hivi hivi tukiendelea kumchekea!. Si mnakumbuka ya Jumbe?!.

Suluhisho la Zanzibar ni ama CCM wakubali matokeo, mshindi halali atangazwe, akabidhiwe madaraka, au SMZ ifunge tuu macho ichukue maamuzi magumu, vinginvyo Zanzibar ita suffer the consequences!.

Tanzania bara hatuwezi kuiacha Zanzibar situation ikiwa volatile hivi ilivyo, ama Rais Kikwete afanye kitu, au Magufuli aapishwe kesho Jumapili, ili tangu Jumatatu, "hapa kazi tuu" ianze rasmi Jumatatu, na kazi number 1 ni Zanzibar Heshima!, Adabu!.

Mkumbuke Zanzibar haiwezi kuachwa hivi hivi kwa kisingizio, uchaguzi ni mambo ya ndani ya Zanzibar, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT!, Tanzania ni nchi moja, yenye upande mmoja wenye amani tele, na upande mwingine wenye hali tete!.

Huyo kijana aliyekiri kutega bomu Darajani, akimtaja aliyemtuma, asikamatwe, wala asifunguliwe mashitaka yoyote!, inatakiwa akimtaja tuu aliyemtuma, ni kimya kimya!.

Pasco

 

Attachments

  • bomu.jpg
    bomu.jpg
    37.6 KB · Views: 3,659
  • bomu1.jpg
    bomu1.jpg
    17 KB · Views: 3,525
Last edited by a moderator:
Zanzibar umeanguka hautakuja kusimama tena!
Pole sana Zanzibar!
Wajinga wachache ndiyo waliopenda kukuangusha!
Hatima yako ipo mikononi mwa Mungu!
 
Wale waliosema bao la mkono lina faida kwao walikosea. Ladba halitakuwa na faida kivile. Tuombe Mungu atunusuru maana huwezi nyanyasa raia wakoo kiasi kikubwa namna hii.
 
Wakuu saa moja ilopitA kulikua na taharuki kubwa Darajani watu walikua wanakimbia ovyo. Tetesi ni kuwa kuna bomu la kutegwa.

Sasa hivi kuna mshindo mkubwa umesikika sasa cjui kama ndio hilo bomu . Mwenye taarifa atujuze.

Wapi huko?Arusha,Mtwara su Katavi?
 
Hivi huyu Jecha Salum Jecha anajua mshindi halali wa uchaguzi wa Zanzibar?
Hasituletee stori za Kivuito wa Kenya!

Ni kweli hiyo habari.na tayari hilo bomu limeshalipuliwa na askari na hakuna madhara yeyote.ila taharuki kubwa ipo watu wana hofu na nj8a zimefungwa kuanzia makao makuu ya ccm.mpaka haile sellasie school
 
njia pekee ya kuzuia machafulo zanzibar either ya mda mfupi au mrefu ni kumpa maalim self ushindi wake na si vinginevyo maana hata uchaguzi ukiridiwa na akashinda wa CCM ,cuf hawata kubali na machafuko yataendelea milele.

na hata kabla ya hvyo pia watu wanaweza kuacha kupiga kura yakapiga majimbo yale ya unguja tu yenye wanachama wa CCM.
CCM kweli hawana akili,maalimu ameshinda majimbo yote pemba na baadhi ya majimbo unguja mwenzio Dr.shain hajashinda jimbo hata moja pemba huoni umisha shindwa?
 
Kama hio habari ni ya kweli basi nina hakika kwa 100% kuwa ni Usalama wa Taifa ili wawshingizie Viongozi CUF wawatie ndina na Wapate Huruma kutoka Mataifa ya Nje waweze kubakia Madarakani Zanzibar
 
yaani ngajim mmoja tu aliyepewa heshima kubwa ya kuwa mwenyekiti wa ZEC anaweza kusabisha umwagaji wa damu mkubwa na yeye kukosa heshima kbsaa ktk maisha yake yote
 
Back
Top Bottom