JWTZ waanza mazoezi ya machafuko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ waanza mazoezi ya machafuko

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by We know next, Oct 25, 2010.

 1. W

  We know next JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanzegu wa JF na watanzania wote kwa ujumla wenu, yale yaliyosemwa sana kwamba JWTZ wanawekwa chonjo ktk uchaguzi huu, ni ya kweli tu. Nimeshuhudia kwa macho yangu pale Lugalo jeshini mida hii ya saa saba na nusu mchana, wanajeshi wa JWTZ walikuwa wanajifua pale ktk viwanja vyao. Nimesema hivyo kwasababu zana walizokuwa nazo ni zile zana ambazo hutumika kutuliza ghasia, kama vile virungu, ngao, machela na mabomu ya machozi. Nimewaona wakiwa na zana mpya kabisa, ukiziona zile ngao zao ni rangi ya silver, zinawaka kwelikweli. Nadhani yaliyosemwa si bure. Bila shaka vikosi vyote vitakuwa na zoezi kama hilo hapa nchini.
   
 2. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dr. slaa kashasema vurugu zitaanzishwa na CCm na vikundi vyake. Kwa hiyo si ajabu,
  Lakini lazima waumbuke mwaka huu
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo kazi yao. Wanao wajibu wa kusaidia polisi pale ambapo watazidiwa. Iwapo watahitjika kufanya hivyo halafu ikatokea hawapo tayari tutawashangaa!! Katiba ya nchi na sheria ya usalama wa nchi zinawataka wawe tayari kwa hilo. Hivyo inatakiwa wana JF na wananchi kwa ujumla tuwasifu kuwa wako makini na wanajua wajibu wao. Au unataka walale tu halafu baadaye uwalaumu? Tusichangaye suala la ulinzi wa nchi na siasa !!!!. Kila mtu atimize wajibu wake, wewe kapige kura 31/10, ndio wajibu wako.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haya ni mazoezi ya kawaida tu wanajiandaa kusimamia usalama wa raia wakati wakupiga kura. Nenda kapige kura yako uko salama kabisaaaa cku hiyo!
   
 5. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Hii thread haina maana sana wakati huu. Hawa wanajeshi wetu wako kwenye mazoezi ya kawaida kabisa na wala hayana uhusiano sana na uchaguzi. Hawa muda wote wanatakiwa wawe wenye utayari, sasa hapo ni kujaribu kuwakumbusha baadhi ya techniques za kupambana na ghasia. Hii haina maana kuwa uchaguzi utakuwa na ghasia. Habari kama hii kwa sasa ni kutaka kutisha watu, hivyo ninafikiri si busara sana kuindeleza hapa. Cha msingi ni kuwaacha watu wakachague viongozi wao kwa uhuru na haki bila kuwaandikia habari za vitisho. Hizi ni habari za magazeti kama mtanzania, Uhuru na Jamboleo. Kwa ushauri tu ni bora kuwapuuza watu hawa kuliko kuwapaisha. Asanteni sana
   
 6. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama ni wajibu wao kusaidia polisi pale polisi wanapozidiwa kwa nini iwe mwaka huu, miaka ya nyuma aghaaaa.Sisi tunasema hatuogopi kwani uoga wetu ndio umasikini wetu.
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Kwa tetesi zizizopo ni kuwa siku ya uchaguzi hawa wanjeshi wanavaa Gwanda za FFU kwa hiyo ni vigumu kuwagundua.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  HII KALI!
  Watadhalilika, maana hakuna atakaeleta fujo, kazi ni moja kuimwaga ccm!
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Yeah, your right, Jimmy.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  wameshiba uji wa bure hao..mazoezi wamfanyie nani..Si waende Afganistan kama wao vidume....
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  nimeambia jina langu lipo kwenye list so kesho naelekea MWanza kwa ajili ya kupiga kura kwa dk wa ukweli hon. W.P.S

  mwaka huu sitanii na wala siangalii kundule
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama haya mazoezi ni ya kawaida. Tuache kuuhadaa umma. Ukweli ni kwamba JK anajua ni nini atakachokifanya mwaka huu na anajua kwamba watanzania hawatakubali. Iweje mazoezi ya kawaida yashirikishe hadi kujaribisha king'ora cha kutangazia hali ya hatari? Kama tangu wakati wa Nyerere hadi leo hawakuwa kukijariibisha hicho king'ora iweje wafanye hivyo leo? Na swali lingine, ni je huu ndo uchaguzi wa kwanza kufanyika Tanzania? Mbona hizo chaguzi nyingine zote hatukusikia kwamba wanajeshi wanajiandaa kusaidia polisi? Naona CCM mwaka huu mmeamua kwa dhati kabisa kumwaga damu zetu.
   
 13. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  wananchi wakiamua... wameamua... !! CCM wakishindwa watafanya TZ isiwe kisiwa cha mani tena!!
   
 14. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mambo kama haya siyo ya kupuuzia. We fikiri wana rungu, mabomu ya machozi na ngao, nijuavyo hivi vifaa hutumiwa na polisi na kama kazi inahitaji jeshi huwa lazima wachukue silaha nzito zaidi. Ieleweke kwamba Polisi wakishindwa na kama adui ana silaha za Moto ndipo jeshi linapotumika. sasa inakuwaje wanafanya mazoezi yanayofanana na yale ya jeshi la polisi. katika hali kama hii lazima tushtuke na si jambo la kusema kirahisi tu kwamba tunawatisha watu
   
 15. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo mwaka huu?
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Haya sasa utawala wa kijeshi is around the corner!!!
   
 17. d

  dotto JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi nafarijika maana hawatapigia CCM kura maana watakuwa kazini.


  MIMI DR.WILBROAD SLAA NAAPA KUILINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA. NITAANZA KWA VITENDO NA MAFISI WOTE!!!! EE MUNGU NISAIDIE!:doh:
   
 18. October

  October JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Most wananchi have made up their Minds, They are going to Vote CCM Out. It does not matter whether TPDF are exercising or Not.

  Nadhani wanajiandaa kukabiliana na vurugu zinazoweza kutokea wakati wa kuapishwa zitakazowezafanywa na wanachama wa chama kikuu cha Upinzani CCM

  Mwaka Huu Mchele na Chuya vitajitenga.!!!
   
 19. M

  Matarese JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo neno, halafu JWTZ karne hii wanafanya mazoezi na virungu,vya kazi gani wakati wao sio polisi?
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Jeshi ni nini? Jeshi hilo lipo kwa ajiri ya nani? mbona mnaogopa ogopa? we amka asubuhi piga kura yako then tusibiri matokeo. Hayo majeshi yatariport kwa yeyete atakayeshinda.
   
Loading...