Elections 2010 JWTZ waanza mazoezi ya kuzuia ghasia

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Katika hali ya kushangaza wanajeshi wa JWTZ wapo kwenye mazoezi makali, mithili ya yale ya FFU, bila shaka kujiandaa kwa kupambana na watakaopinga matokeo ya uchaguzi mkuu baada ya kuchakachuliwa kwa kura. Nimewashuhudia mimi mwenyewe pale Lugalo leo. Kwa kawaida mazoezi ya aina ile hufanywa na FFU. Kunani? Au ndio maelekezo ya Shimbo kutoka CCM?
 
mimi pia jana niliwashuhudia kwenye stesheni moja changa hapa nchini ilikuwa inaonyesha mazoezi wanayofanya sasa nikashindwa kuelewa wanatishia wananchi au wanamaanisha kitu gani?
 
Wanajeshi? Au mipaka yetu ipo hatarini? Hawa wanatisha toto nazo lol
 
Hehehe washapewa AMRI
hakuna wa kukataa wala kuhoji.
Naona mkulu anatumia kofia yake ambayo hawezi kujiuzulu nayo...
 
hii nchi ccm waliinunua lini na wapi? na shahidi yao nani? basi watupe risiti yetu tujue moja.
 
Nadhani Kikwete sasa amedhamiria kuendelea kuwa madarakani kwa nguvu baada ya kuona umma wa Watanzania hawamtaki yeye na mafisadi wake anaowalinda. Nguvu ya umma ndiyo itakayoamua. Let's wait and see.
 
Amiri Jeshi Mkuu kisha toa maagizo kuwa Polisi waibe kura na jeshi lisimamie wizi huo.
Unadhani nani wa kubisha?
Katika hali ya kushangaza wanajeshi wa JWTZ wapo kwenye mazoezi makali, mithili ya yale ya FFU, bila shaka kujiandaa kwa kupambana na watakaopinga matokeo ya uchaguzi mkuu baada ya kuchakachuliwa kwa kura. Nimewashuhudia mimi mwenyewe pale Lugalo leo. Kwa kawaida mazoezi ya aina ile hufanywa na FFU. Kunani? Au ndio maelekezo ya Shimbo kutoka CCM?
 
Mambo magumu, maji ya shingo. Wamejaribu kumharibia Slaa kuwa;
- ametuma na kanisa - watu hawaelewi Slaa anazidi kuchanja mbuga
-Amepora mke - ni kama mtu anazima moto kwa petrol
- ooh mabomu yake ni feki - Anatoa data za kiutafiti na kuwaambia wanaona ni za uongo wajitokeze hadharani kupinga na waende haraka mahakamani!
Sasa wameamua kutumia NEC na jeshi.

SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTEREZA - hata wanajeshi watasema enough is enough. yule raisi wa Burundi hata walinzi wake binafsi waligoma kumlinda.
 
Mlioko kyela vip Malawi wameanza fujo,na wa kule bukoba na kigoma twaomba upadates DRC kumechafuka.
Tunduma zambia tuko shwari?Najua namanga tutakuwa shwari.
Wale wa mipakani watujuze unaweza kuta nchi yataka vamiwa watu wameamua kula ligwalide.
Shimbo ana hofu ya kupokonywa tender yake ya power tiller na maduka ya jeshi waliojimiliksha?
 
Ooooh my Gooosh!
JKanataka kitu gani huyu?
Kwanini anataka kuipeleka nchi kwenye matatizo?
Tuliwaambia watu kuwa huyu mtu wa kuchekacheka si mzuri ati, tukaonekana tunamwonea wivu...Sasa hajui anawaweka roho juu hata wapenzi wake!.
Lakini nisemacho mimi ni kwamba ana'worsen hali, atapata strongly negative results!
 
Watatumia jeshi pamoja na NEC lakini wananchi bado wanahitaji mabadiliko. Wanajifanya kama hawajui yaliyotokea Kenya. Hiki kiburi ni cha nini? Wananchi wamechoka na wanataka kuongoza nchi yao wapendavyo na si kuamuliwa ni kikundi fulani.
 
Wakuu mpaka wetu na nchi ya Kenya mambo si shwari bwahahaha hahaha.
 
Mbona sioni mtu akisema tunaomba ushaidi wa picture!
Unaweza vunjwa wewe na kamela yako
 
Back
Top Bottom