JWTZ - Tutambueni sisi ni Maaskari wenzenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ - Tutambueni sisi ni Maaskari wenzenu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Dec 8, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Habari wanajamvi,

  Nakuja na hoja mpya kidogo kwa jeshi letu la wananchi, mimi na wenzangu tuliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga taifa miaka ile ningeomba tutambuliwe na JWTZ kama maaskari kamili.

  Sisemi tuvae magwanda na tuhamie makambili laa hasha ila tutambulike kama ma askari wa Tanzania na kama kuna mahitaji yoyote ya wapiganaji basi tupewe fursa na sisi na kuwatumikia wananchi kwani tunajua mbinu zote na siri za kijeshi ingawa kwa sasa tupo uraiani tu kama wananchi wa kawada.

  Nimepata wazo hili baada ya Juzi nilivuka kigamboni kukutana na mama askari (Brigedia General) kwenye gari lake, nilishuka kwenye gari langu na kumpa heshima yake, tuliongea kidogo hadi tulipofika ngambo.

  Mazungumzo yetu

  Kijana unaonekana wewe kama askari?
  Ndiyo mama mimi ni askari na nina force number ambayo niipata baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi miaka ile inajulikana kama JKT kwa mujibu wa sheria
  safi sana kumbe jeshi letu lina askari wengi uraiani - smile na kicheko
  ndiyo mama tupo maakari wengi tu na usalama wetu ni mkubwa ila tunahitaji mazoezi kujiweka sawa kadri fursa zinapotokea
  yeah hilo ni wazo zuri kijana tutalifanyika kazi
  asante kwa kheri.  Mapendekezo yangu ni haya.
  1. Tuwe tunapelekwa refresher course na mazoezi ya kijeshi mara fursa zinapotokea
  2. Tupandishwe vyeo kutokana na elimu na utiii katika jeshi - kwa mafano mimi ningekuwa jeshini
  nafikiri ningekuwa cheo cha Meja kwa sasa
  3. Kwa baadhi yetu wanaopenda wanaweza kwenda makambini kufundisha au kufanya kazi za
  kitaalam kama engineering, udaktari, utafiti nk kwa muda maalum.

  Tuliopita Jeshini naomba mniunge mkono ili wazo hili tulipeleke kwa wanaohusika. nawakilisha.

  Wale wa Makutupora, Ruvu, Buhemba, Mlale, Oljoro, Msange, Mafinga, Bulombora n.k mpo? au bado mnaogopa zile trankadoso na kalinye kalinye?
   
Loading...