JWTZ na W/wa ULINZI Tunahita Maelezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ na W/wa ULINZI Tunahita Maelezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jul 4, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mimi kama mwananchi ambae kwa sasa ni wakawaida ni mstaafu wa JWTZ niliyeshiriki kikamilifu kumtimua Nduli,.Wananchi huwa wanaambiwa kazi moja ya jeshi ni kulinda mipaka yetu na wengine wanaitikadi ya ule mwenge kumulika kwenye mipaka ,je baada ya kufariki kwa Mwalimu Julius ,jeshi na mwenge vimekufa ?

  Sasa hivi nchi yetu imekuwa ni njia ya kufikia Ulaya,na wapita njia wanaotumia njia hii huwa hawana hata pasi au karatasi za kuingia nchini mwetu ,la ajabu zaidi watu hawa huingia na kupitishwa katikati ya Tanzania wakitumia njia kuu
  Waethiopia wasomali na wengine hupita wakiwa wamejazwa kwenye malori kama mbuzi au makontena yaliyofungwa kutokea mpaka wa kaskazini wakielekea mpaka wa kusini magharibi na wanaokufa hutupwa njiani kama kuku ,na dereva akiona wateja wake wamechoka ya kuelekea kifu huwamwaga na kuwaacha popote pale.

  Nielewavyo njia kuu nyingi zina mageti mengi tu mbali ya entry za mipakani ,inakuwaje malori haya hupita humu bila ya kukamatwa ila ukipita na gunia la mkaa utakiona cha mtema kuni kuchomwa na miba.Huu ni udhaifu wa vyombo vya ulinzi.Na tunadanganywa kuwa hawa hutumia njia za panya kwa maana hiyo tunaweza kuvamiwa hadi ikulu kwa kutumia njia za panya.

  Hivi Waziri na wakuu wa Jeshi hawaoni kama kuna kasoro ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ,hawawezi kutumia majasusi wa jeshi letu kubaini njia hizi na kuwabaini wahusika ,kati ya wanaotupwa wengine huwa bado wapo hai hivi hawawezi kuwafanyia au kuwachunguza na kupata data kamili za tokea mwanzo wa safari yao na njia walizozipita ?

  Na kama njia walizopita zikigundulika kuwa sio hizo za mapanya kwa maana wamepita katika njia za mipakani kwa nini hawawahoji hao wanaohusika na hayo mageti na mipaka ? Ikibidi kuwawajibisha !
   
Loading...