JWTZ na siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ na siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Dec 16, 2008.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mod,unaweza kuiweka hii mahala inapofaa.

  Nimeshtushwa na taarifa katika habari ifuatayo kwamba Jenerali Robert Mbona alikuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1981.Labda sielewi vizuri kuhusu sheria inayowakataza watendaji wa vyombo vya dola kujihusisha na siasa (apart from kupiga kura) lakini nadhani hii haijakaa vizuri.Hebu soma extract hii hapa,then tujadili zaidi


  Sasa kama Mboma alikuwa mwanachama wa CCM wakati akiwa Mkuu wa Majeshi,hii haikuathiri utandaji wake wa kazi kwa namna moja au nyingine?Au ali-suspend uanachama wake katika kipindi cha utumishi wake then aka-renew baada ya kustaafu?Ikumbukwe hapa tunjamzungumzia kiongozi wa juu kabisa wa jeshi letu.

  Halafu vyama vya upinzani vinapolalamika kuhusu matumizi mabaya ya vyombo vya dola kwa manufaa ya CCM vinaambiwa havina hoja za msingi.Pengine hii ni wake up call kwa vile kuna uwezekano kwamba hata akina Mwema et al nao ni wana-CCM.

  As I mentioned earlier,sina ufafanuzi mzuri wa kisheria kuhusiana na ishu hii.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Dec 16, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280

  Nitachangia vizuri hapa nikitulia, una point nzito kabisa.
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Nadhani(kwa mtizamo wangu) alichukua uanachama kipindi kile ambapo siasa iliruhusiwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama(kipindi cha chama kimoja-CCM) na baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza akawa hajishughulishi na masuala ya kisiasa mpaka pale alipostaafu na kuamua kuendelea kuwa mwanachama wa CCM..Huo ni mtizamo wangu tu mkuu..btw kwani alipokuwa CDF amewahi kuonesha dalili zozote za kuipendelea CCM?????
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,554
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Nadhani chini ya ukiritimba wa chama kimoja...Mojawapo ya sifa za kupata nafasi yoyote a uongozi ni kuwa mwanchama mwaminifu na mtiifu wa TANU/CCM....Sasa kama tuko kwenye mfumo wa vyama vingi then ni lazima tufanye mabadiliko.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  kweli kaka inabidi kutulia maana taarifa hii kweli inashtusha!!!!!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nadhani alikuwa na maana alikuwa mwanachama kuanzia mwaka 1981 mpaka pale sheria ya vyama vingi ilipopitishwa na kuondoa mkoa wa majeshi automatically na uanachama wake ukakoma na somehow ukafufuka baada ya kustaafu U-CDF.

  Ni fikra zangu anyway....
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Wooooooooooote kabisa ni wana CCM kasoro OCD wa Tarime ambaye hata Makamba aliona kwamba jamaa ni mtumishi wa Umma na si mtumishi wa CCM.
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Labda swali hapa halijaeleweka, how would you determine this mkuu kwamba huenda alikua anapendelea CCM?

  - Kwa mfano aliajiri vijana wa CCM tu or what?
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMES,heshima mbele,kimsingi mtoa hoja(Mlalahoi) kauliza kama u CCM wa Mboma uliathiri utendaji wake wakati akiwa CDF...Ndo nikauliza je wakati akiwa CDF alionesha dalili zozote za kuipendelea CCM???,so nadhani jibu la swali hili(probably Yes/No) ndo litaweza kuonesha kama hali ya kuwa CDF while ni mwana CCM ilipelekea kuathiri utendaji kazi wa Mboma...Heshima mbele mkuu..Mzee wa sauti ya umeme..Be blessed
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Dec 17, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuanza kwa siasa za vyama vingi, shughuli za siasa zilipigwa marufuku kwenye majeshi yetu. Chini ya utaratibu huo, wanajeshi pamoja na polisi wote wanatakiwa wasiwe wanachama wa chama chochote hata kama walikuwa wanachama wa CCM zamani. Akina Marando walikuwa CCM damudamu wakati huo lakni baadaye wakaachana nayo, vivyo hivyo ndivyo ilivyotakiwa kwa wanajeshi wote.

  Hata kama Mboma hakuwa active kwenye siasa, lakini inaelekea kuwa alikuwa sympathizer mkubwa sana wa CCM. Jambo baya ni kuwa kwa vile alikuwa shabiki wa CCM, kwa vyovyote hakuwa impartial katika maaumzi yanayohusu CCM na vyama vingine vya upinzani. kama angetaikiwa kutuma batalion moja kwenda kuwafunza adabu mashabiki wa upinzai huenda asingesita. Kuna mifano ya kutosha kuonyesha kuwa vmakamanda wanaoishabikia CCM wamekuwa wanatumia madaraka yao vibaya dhidi ya upinzani: Mahita ni mfano mzuri sana aliyetamka hadharani kabisa kuwa anaivunjavunja CUF.

  Ningeshauri kuwa ili makamanda na majaji wasiwe na upendeleo kwa chama chochote cha siasa, kuwe na time interval ya wao kutoshiriki siasa za aina yoyote baada ya kustaafu; tena hapa kwetu iwe interval ndefu kidogo ili madaraka yao ya zamani yasahauliwe kwanza ndipo waanze sisas. Hii itasaidia kuwazuia kutumia madaraka yao kwa ajili kujijenga kisasa wakaribiapo kustaafu.
   
 13. RR

  RR JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Ingefaa kuwa na utaratibu wa kukoma kwa benefits wanazopata hawa wastaafu wa vyombo vya usalama iwapo watajihusisha na siasa, wanapokua wamestaafu.
  Achague kupoteza haki zake ama siasa.
   
 14. J

  Jitume Senior Member

  #14
  Dec 17, 2008
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Safi Mkuu Kichuguu,

  CDF ni mtu mwenye influence kubwa kwa wanajeshi kabla na baada ya kustaafu. Yafaa nafasi kama hizo, kama si kuwekewa interval ndefu,wasiruhusiwe kabisa kushiriki siasa hata baada ya kusataafu.

  Chukulia kama angepita kura za maoni na kushinda ubunge halafu anateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi (Mheshimiwa), Bila shaka jambo la kwanza litakuwa namna ya kwenda kuteketeza ushahidi kuhusiana na tuhuma dhidi yake -DEEP GREEN nk pia kushughurika na wachukia ufisadi badala ya huduma kwa umma!!

  Afadhari ameanguka kwiiikwiiiiiiiiiiiiiiiiiikwiiiiiiiiiiii
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wacha kamba zako za Tarime...
   
 16. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wooooooooote na wana CCM na ndiyo maana linapokuja suala la kuwashughulikia wapinzani huwa wanatekeleza kazi hiyo haswaaa. Mfano halisi ni Mahita alimpiga sana Mrema na zawadi yake ikawa ni kupewa nafasi ya u-IGP. Nishani iliyotukuka ya afande Tosi juzi juzi ni zawadi za namna hiyo. Tofauti na hayo angalia kule Mbeya Chadema walipotaka kuzindua Kampeni yao ya Operation Sangara polisi hao hao kama vile hawajui nini maana ya jina hilo wakadai waelezwe maana yake, hii yote ni kwa sababu ya kuwa na kadi za CCM mifukoni mwao.
   
  Last edited: Dec 17, 2008
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Well hakuna la kuficha kwamba CCM wamefanya kazi nzuri sana ya kuwapumbaza wanajeshi na kuwa incoperate ndani ya chama ili Chama na jeshi vitawale sambamba. Same story usalama wa taifa. Ndio maana mpaka sasa kwa watumisi wengi wa ngazi ya juu maslahi ya CCM ni maslahi yao binafsi, na kwao CCM inakuwa mbele kuliko Taifa. Lakini kushindwa kwa Mboma kwenye kinyang'anyiro ni baraka za mungu atleast watu wa Mbeya wameonesha kuwa wanaweza kusema NO kwa mafisadi. Na good news ni kuwa Makamba ameingia mkenge tena kwa kumuunga mkono mtu aliyeshindwa i do not know what will be next.
   
 18. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2008
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  La msingi nafikiri ni mfumo wetu wote wa uongozi ni mbovu.Nafikiri badala ya wakuu wa majeshi,au taasisi nyingine ya umma,kama mkuu wa chuo,au mkurugenzi wa taasisi ya umma,asiteuliwe na rais,bali ateuliwe na bunge chombo ambacho kipo huru ili mkuu wa majeshi awajibike kwa shughuli za kijeshi na kusiwepo any conflict of interest.Ilivyo sasa anawajibika zaidi kwa anayemteua,so hata kama chama kingine kitachukua madaraka na akawepo rais mpya itatokea the same.Lazima tushughulikie mfumo wetu wote wa uongozi.
   
 19. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2008
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu wa majeshi ni mtu mkubwa kweli kweli. na niwa muhimu sana pia. na anakuwa na influence kubwa kwa wanajeshi wenzie kama wachangiaji wengine walivyoelezea.
  hata hivyo yeye ni binadamu kama mimi na wewe na anaweza kupenda kujitumbukiza ktk siasa.
  sioni sababu ya kumnyima haki zake eti kwa vile anataka uongozi ktk siasa. ili iweje? kwanini iwe kwa wanajeshi tu au wakuu wa majeshi tu?
   
Loading...