JWTZ na Polisi nao hupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu kwa Tanzania Bara?

The king mswati

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
787
820
Wakuu Habarini za Asubuhi.

Nilikuwa naomba mwenye ufahamu kuhusu hiyo title hapo anijuze.

Je, Jeshi la wananchi wa Tanzania pamoja na Askari polisi nao huwa wana haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wa nchi?

Maana kuna kazi zingine najua huwa zina miiko yake na katika hili mimi nilikuwa nadhani hawapigagi kura kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa, lakini nilichokiona jana huku Zanzibar kimenifanya niulize swali hapa leo.
 
Kila raia ana haki ya kupiga kura akikidhi vigezo...
Duuh..kama hawa wajomba wanapiga kura kumchagua rais, majeshi yetu si yangekuwa yana asi kila kukicha aisee...

maana hata wapinzani jeshini wangekuwepo na pia na wao wangekuwa wanaandamana kudai haki na sijui hapo ingekuwaje 🤔🤔🤔.

Na pia pale mgombea flani anaposhinda alafu watu wengine wasimkubali waanze kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi, then askari watumwe wakazime maandamano, vipi hapo huoni kuwa kuna askari wanaweza kujiunga na kuwa sehemu ya maandamano hayo?

Nahitaji ufafanuzi kidogo hapa kuhusu hii maada mkuu.
 
Hawa ruhusiwi. Ni mwiko. Vikosi vyote vya ulinzi na usalama. Yaani traffic officers, mgambo, wajeda, askari wa raia, Vikosi vya zima moto na kadhalika,hadi TISS, hawa wote hawa ruhusiwi kupiga kura.

Ila awamu hii mambo mengi yanafanywa kinyume na utaratibu so usishangae.

Kura wameanza kupiga Tanzania visiwani then ndio tuje sisi Tanzania Bara

Kiongozi aliyemaliza muda wake kuitwa Raisi na kuendelea na majukumu kama vile bado yupo katika ofisi na mawaziri wake.

Mambo ni mengi sana yanafanywa kinyume na utaratibu, miiko yetu, na utaratibu wa kikatiba.
 
Ila awamu hii mambo mengi yanafanywa kinyume na utaratibu so usishangae.....

Kura wameanza kupiga Tanzania visiwani then ndio tuje sisi Tanzania Bara

Kiongozi aliyemaliza muda wake kuitwa Raisi na kuendelea na majukumu kama vile bado yupo katika ofisi na mawaziri wake.

Mambo ni mengi sana yanafanywa kinyume na utaratibu, miiko yetu, na utaratibu wa kikatiba.
Asante mkuu kwa ufafanuzi wako maana hata mimi ndicho nilichokuwa nakifikiria kichwani sema sikuwa na uthibitisho huo.
Ila kilichonishangaza ni kwamba Tume ya uchaguzi huku visiwani (ZEC) ilikuwa imetangaza kuwa watu watakaopiga kura tarehe 27 (jana) ni maafisa watakaoenda kusimamia uchaguzi tarehe 28 (leo) na miongoni mwa maafisa waliotajwa na ZEC kwenye uhusika wa upigaji kura tar 27 walikuwa ni Askari polisi + wasimamizi wengine wa uchaguzi.
Sasa nikawa najiuliza tangu lini askari wakapiga kura kumchagua Rais ? Nikawa nadhani labda huku Zanzibar askari huwa wanapiga kura ila Bara sijawahi kuona wala kusikia vitu hivyo.
 
Kila Raia Ana haki ya kupiga kura ,,ilimradi awe ametimiza vigezo,,,husikA,,,wanajeshi,,polisi ,,,Tiss,,,na vyombo vyote vya usalama ,,,,wanahaki ya kuhudhuria ,,,mikutano ya wanasiasa,,,na kusikiliza Sera zao,,na mwishowe,,,Wana haki ya kikatiba ya kumpigia mtu wamtakae baada ya kuelewa Sera zake,,,,... Kisichoruhusiwa Ni kijiunga na vyama vya kisiasa /kushabikia siasa,,,
Asante mkuu kwa ufafanuzi wako maana hata mimi ndicho nilichokuwa nakifikiria kichwani sema sikuwa na uthibitisho huo.
Ila kilichonishangaza ni kwamba Tume ya uchaguzi huku visiwani (ZEC) ilikuwa imetangaza kuwa watu watakaopiga kura tarehe 27 (jana) ni maafisa watakaoenda kusimamia uchaguzi tarehe 28 (leo) na miongoni mwa maafisa waliotajwa na ZEC kwenye uhusika wa upigaji kura tar 27 walikuwa ni Askari polisi + wasimamizi wengine wa uchaguzi.
Sasa nikawa najiuliza tangu lini askari wakapiga kura kumchagua Rais ? Nikawa nadhani labda huku Zanzibar askari huwa wanapiga kura ila Bara sijawahi kuona wala kusikia vitu hivyo.
 
Hawa ruhusiwi. Ni mwiko. Vikosi vyote vya ulinzi na usalama. Yaani traffic officers, mgambo, wajeda, askari wa raia, Vikosi vya zima moto na kadhalika,hadi TISS, hawa wote hawa ruhusiwi kupiga kura.

Ila awamu hii mambo mengi yanafanywa kinyume na utaratibu so usishangae.

Kura wameanza kupiga Tanzania visiwani then ndio tuje sisi Tanzania Bara

Kiongozi aliyemaliza muda wake kuitwa Raisi na kuendelea na majukumu kama vile bado yupo katika ofisi na mawaziri wake.

Mambo ni mengi sana yanafanywa kinyume na utaratibu, miiko yetu, na utaratibu wa kikatiba.
sio kweliii, watu wote wanaruhusiwa kupiga kura hao unaowasema miaka nenda rudi tupo nao mtaani tunapanga nao mistari kwenda kupiga kura, tatizo ni moja tuu asiwe amevalia mavazi ya kazi, nje ya hapo wanapiga kura vizuri tuu na ukiwakagua wengi wana vitambulisho vya kupigia kura.
 
Huwa wanaletwa Zanzibar kuja kujazi kura.....Maana Zanzibar ni Military BASE ya Bara.
Ninachojua ni kweli kwamba suala la ulinzi na usalama wa nchi (Jeshi +polisi) ni Suala la Muungano kwa hiyo najua Polisi + Jeshi halina utanganyika wala uzanzibar bali ni la Utanzania.
Lakini mimi swali langu kuu ilikuwa ni Je kwa mujibu wa miiko ya kazi yao (Polisi + Jeshi) wanaruhusiwa na katiba ya nchi kupiga kura ? Ama kwa lugha raisi kujihusisha na siasa.
 
sio kweliii, watu wote wanaruhusiwa kupiga kura hao unaowasema miaka nenda rudi tupo nao mtaani tunapanga nao mistari kwenda kupiga kura, tatizo ni moja tuu asiwe amevalia mavazi ya kazi, nje ya hapo wanapiga kura vizuri tuu na ukiwakagua wengi wana vitambulisho vya kupigia kura.
Duuh...hapa changamoto sasa,nimwamini yupi sasa ambae ana reference ya uhakika ya kikatiba maana naona wengi tuna majibu ya stori za vijiweni.
 
Ninachojua ni kweli kwamba suala la ulinzi na usalama wa nchi (Jeshi +polisi) ni Suala la Muungano kwa hiyo najua Polisi + Jeshi halina utanganyika wala uzanzibar bali ni la Utanzania.
Lakini mimi swali langu kuu ilikuwa ni Je kwa mujibu wa miiko ya kazi yao (Polisi + Jeshi) wanaruhusiwa na katiba ya nchi kupiga kura ? Ama kwa lugha raisi kujihusisha na siasa.
Kupiga kura sio kujihusisha na siasa.Kupiga ni kushiriki katika maamuzi.So sio wapiga kura wote wananshiriki katika SIASA.So haki yao ya kupiga kura ni haki ya KIRAIA kwa sababu wao ni RAIA ila hawaruhusiwi kuwa makada wa chama chochote cha SIASA
 
😁😁😁 umefafanua lakini bado kuna utata...bado tu najiuliza Askari au mwanajeshi akapiga kura alafu akatangazwa magufuli mshindi wakati yeye (polisi au mwanajeshi) alimpigia Lissu, then kukatokea vurugu wao wakatumwa wakazime zile vurugu huoni kuwa kunaweza kuwa na uasi hapo hata na wao wakaungana na waandamanaji ?
 
Back
Top Bottom