JWTZ na Mahusiano ya Kujenga Uchumi wa Kisasa: Maswali yasiyojibiwa

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,020
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,020 280
  • Tanzania Mpya Bila Ulinzi Mpya - Inawezekana?

Tanzania inahitaji kujionesha ni taifa linalojiamini na ambalo linajua uwepo wake una maana gani. Ili kuweza kufikia hapo ni lazima kwanza kama taifa tutambue na kuwa tayari kulinda na kutetea uwepo wetu kama taifa kutoka tishio lolote la uwepo huo (existential threat). Karibu mataifa yote ambayo yameweza au yanajenga nchi za kisasa yamejikuta yakiangalia pia dhana hii ya sababu yao kuwepo na hivyo kujenga uchumi na miundombinu ambayo itahakikisha kuwa taifa hilo linakuwepo. Katika nchi kama ya kwetu ambayo inataka kuwa ya kisasa hatuwezi kabisa kutenganisha uchumi kutoka kasika jeshi au nafasi ya jeshi katika kuulinda uchumi huo na hata kuuchochea.

Maswali yanahitaji kujibiwa

a. jeshi letu ni la nini hasa? swali jepesi lakini lina uzito wake. Zamani tulikuwa ni jeshi ambalo lilikuwa zaidi kwa ajili ya ulinzi katika mazingira ya vita baridi na tishio la uvamizi wa Afrika ya Kusini, Wareno n.k Hivyo lilikuwa ni jeshi la kiukombozi zaidi (liberating force) na hivyo tulifanya vizuri sehemu mbalimbali. Lakini leo hii jeshi hili ni la nini? Hatuna tishio la kuvamiwa na Afrika ya Kusini, hatuna tishio la kuvamiwa na Wareno na wala hatuna tishio hasa la kuvamiwa na nchi yeyote jirani so jeshi letu linatulinda kuhusu nini au nani hasa?

Jibu la swali hilo ni msingo wa nadharia ya kijeshi (foundation for the military doctrine). Naomba kupendekeza kwamba lazima jibu lihusiane na uchumi.

b. Jeshi letu linasimamiwaje na siasa zetu liko vipi? Mojawapo ya mambo ambayo binafsi yananitaza ni kuwa jeshi letu liko kama jeshi la CCM hivi ambapo viongozi na muundo wake unafikiria zaidi uwepo wa CCM kuliko kitu kingine chochote. Sasa hili lina sababu za kihistoria bila ya shaka kwani baada ya mgomo wa jeshi wa 1964 jeshi liliundwa likiwa limefungamana na TANU na kwa karibu miaka thelathini uongozi wa jeshi ulikuwa vile vile unahusiana na uongozi wa kisiasa wa chama tawala. Sasa katika mazingira ya vyama vingi jeshi letu linakuwa vipi? Leo hii Dr. Slaa anaweza kwenda na kuzungumza na viongozi wa jeshi kuelezea sera za CDM, je kiongozi wa jeshi anaweza kwenda kutembelea ofisi za CUF kujifunza mambo ya CUF bila kuoneakana anapendelea kitu fulani? Je kiongozi wa CCM anaweza kuwepo kwenye kundi la maafisa wa JWTZ bila kuonekana anapendelewa na jeshi?

Je katika mfumo wa vyama vingi ni taratibu gani zinazoongoza mahusiano ya jeshi na vyama vya siasa? Je jeshi laweza kukaa pembeni na kuacha siasa ziendeshwe huku lenyewe likita tayari kumpigia saluti yeyote anayechaguliwa na wananchi? au linaweza kuapa kama ilivyokuwa kwa jeshi la Zimbabwe kuwa halitompigia saluti kiongozi wa upinzani?

Nadhani kuna mambo ambayo ni muhimu kuyafikiria kidogo - nimewahi kuyaandika huko nyuma kidogo na inshallah, nitaliendeleza kwa kina hili wazo siku moja.

a. Uchumi wa Kisasa unataka Ulinzi wa Kisasa (Moden Economy demands modern defenses)

Mojawapo ya vitu ambavyo unaweza kuviona kirahisi nchini sasa hivi ni msisitizo mkubwa uliopo katika kuufanya uchumi wetu kuwa wa kisasa zaidi na wenye kuendeshwa na sekta mbalimbali. Kutoka kwenye uchumi wa kilimo hasa na kuwa uchumi wa uzalishaji wa viwandani na hata wa sekta nyingine. Kutokana na msisitizo huo uchumi wa Tanzania unazidi kutoa nafasi zaidi kwa wananchi japo naweza kujenga hoja kuwa sidhani kama tumefikia hata 5% ya uwezo wetu kiuchumi. Sasa uchumi wa namna hiyo unavutia watu wengi na mojawapo ya hatari zake ni kuvutia watu wahalifu na watu wenye nia mbaya.

Mwaka huu peke yake tumesikia jinsi madawa ya kulevya kwa mashehena yakikamatwa katika ardhi yetu, ukijumlisha hilo na tuhuma za ufisadi unaweza kuona toka mbali tu kuwa uchumi wetu unavutia zaidi ya watu wema au taasisi njema. Kutoka mbali unaweza kuona kwa urahisi kabisa kuwa bila kuulinda uchumi huu utaenda ile njia ya Nigeria. Binafsi hiyo ndio hofu yangu kubwa sana kwamba Tanzania itaenda njia ya Nigeria kwa sababu tumeshindwa kujipanga na kukabiliana vilivyo na changamoto za uchumi wa kisasa.

Ukiangalia China kwa mfano, tangu walipoanza mabadiliko makubwa ya kiuchumi mwishoni mwa 1970s walienda sambamba na mabadiliko yao mtazamo wao wa kijeshi. Walienda pamoja na kujenga uchumi wa kisasa kujenga jeshi la kisasa. Leo hii japo jeshi la China halijafikia uwezo wa majeshi kama ya Marekani na hata Ufaransa kwa kiwango kikubwa sana limekuwa jeshi la kisasa na linaanza kujitambulisha zaidi. Wiki chache tu zilizopita Jeshi hilo limetoa whitepaper ambayo inaelezea kile kinachoitwa "Peaceful Rise" kwamba China inataka kuinuka kama taifa lenye nguvu bila kulazimisha kukandamiza au kuonesha nguvu hizo kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine. Ni wazo zuri lakini ninaamini siku moja china itahitaji kujitutumua kijeshi kutuma ujumbe kuwa "imefika". Na utakuwa mwanzo wa aina nyingine ya Vita baridi.

Kwa tanzania Jeshi na vyombo vyetu vya usalama bado ni vya kizamani sana. TISS, Polisi na TPDF yenyewe bado havijawa katika level ya kuweza kuwa walinzi wa uchumi wa kisasa. Na ninaamini tutapata shida sana siku yakigundulika mafuta na hivyo kufanya "wakubwa" kujichekelesha zaidi na kwa mtu yeyote anayeona yanayoendelea ataelewa wazi kabisa courtship inayofanywa na Marekani haina malengo ya leo bali zaidi ya kesho. Je ni kwa kiasi gani tutangeneza vyombov ya kisasa?

Kati ya vyama vyote vya kisiasa kwenye uchaguzi mkuu uliopita ni CHADEMA ndicho kilichokuwa na maono ya kubadilisha na kuleta mfumo wetu wa vyombo vya usalama kuleta ulinzi wa kisasa wa uchumi wetu. Bila kuongozwa na mtazamo wa kuboresha uchumi na usalama kwa wakati mmoja matokeo yake ni kuwa tutakuwa na uchumi mkubwa ambao utakuwa prone to manipulation n.k the so called the Nigerian Way. Tutapigana, tutachinjana na kufisadiana huku tunachelekea "uchumi wetu unapaa!".

b. Jeshi la WTZ halijaweza kuwa jeshi ambalo linawajibika kwa wananchi sawasawa. Kuna hali ya impunity of sort kiasi kwamba hizi cable zinatuonesha hofu ya viongozi wa kiraia kulisimamia jeshi na hivyo jeshi linaanza kuwa an institution with its own gear. Hii ni hatari sana. Ninaamini mojawapo ya mabadiliko tutakayoyahitaji ni kuhakikisha kuwa jeshi kweli linarudishwa mikononi mwa wananchi. Dhana ya Jeshi katika nchi ya kidemokrasia bado haijazama na angalizo la kina Retzer kuwa jeshi letu bado lina socialist tendencies ni kweli kwani tuliona wenyewe wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana.

Tayari tumeshaona mgongano kati ya Bunge na Urais, tumeona kidogo tu mgongano wa Bunge na Mahakama; bado hatujaona mgongano kati ya Mahakama na Urais na vile vile mgongano wa Serikali (Bunge, Urais Mahakama) na Jeshi. Mgongano huu ni wa lazima ili kuweza kuchora mistari sahihi. Mgongano kama huu umetokea Uturuki ambapo viongozi kadhaa wa jeshi walikamatwa na kufikishwa mahakama na kusababisha wakuu wengine wa jeshi kujiuzulu. je itakuwaje siku current military leaders wa Tanzania wanakamatwa na kufikishwa mahakama kutokana na ufisadi? Je, hofu kuwa ufisadi jeshini ukiumbuliwa jeshi linaweza kuasi ni ya msingi?

Katika kujibu maswali hayo tunakabiliwa na changamoto ya kujiuliza juu ya mahusiano ya jeshi na vyama vya siasa n.k Lakini vile vile inahoji hasa nadharia za kijeshi za nchi je zinatokana na siasa za vyama au zinatoka kwenye jeshi tu? Je ipo haja ya kukaa kama taifa kwanza tunapozungumzia Katiba Mpya kufikiria vile vile juu ya Nadharia ya kijeshi ya nchi yetu? Je katika kujenga uchumi wa kisasa na taifa la kisasa jeshi letu litakuwa na nafasi gani? Tukiangalia kutoka mbali tunaweza kuona kuwa ripoti za Wikileaks hasa kuhusiana na mahusiano ya utawala wa kijeshi na ule wa kiraia tunabakia kujiuliza maswali ambayo labda hatutaweza kuyajibu mara moja.

Lakini ni maswali ambayo yanahitaji na kustahili kujibiwa, kama siyo leo basi siku moja.

MMM
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
13,778
Likes
8,512
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
13,778 8,512 280
Mzee Mwanakijiji heshima mbele,Mwl Nyerere aliwahi kutaka tuwe na jeshi dogo na la kisasa tena baada tu ya vita vya kagera,je kulikuwa na mpango maalum kutekeleza hilo? Kama upo huo mpango kuna utekelezaji wowote unaoufahamu binafsi?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,020
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,020 280
Mzee Mwanakijiji heshima mbele,Mwl Nyerere aliwahi kutaka tuwe na jeshi dogo na la kisasa tena baada tu ya vita vya kagera,je kulikuwa na mpango maalum kutekeleza hilo? Kama upo huo mpango kuna utekelezaji wowote unaoufahamu binafsi?
Kwa kweli sifahamu juu ya mpango huo. Nimesoma kwenye mojawapo ya hizi diplomatic cables kuwa kuna kamati imeundwa kuangalia modernization ya jeshi letu sijui imeteuliwa lini, wajumbe wake ni nini na ina TOR gani.
 
F

FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
8,088
Likes
93
Points
145
F

FJM

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
8,088 93 145
Kwa kweli sifahamu juu ya mpango huo. Nimesoma kwenye mojawapo ya hizi diplomatic cables kuwa kuna kamati imeundwa kuangalia modernization ya jeshi letu sijui imeteuliwa lini, wajumbe wake ni nini na ina TOR gani.
Ukisoma hizi cable ni dhahiri kuwa jeshi letu kwa sasa linapata strategies toka Washington. Sisemi hili kishabiki, la hasha! Everything walichopendekeza Washington including Tanzania kuweka afisa jeshi mwambata kwenye ubalozi wa Washington ilikubalika. Na cable hizi ni za miaka kadhaa hivyo mipango mingi imeshatekelezwa. Kama nchi kuna ulazima (haraka) kuangalia tena upya mipango ya maendeleo ili kujua nafasi ya jeshi/ushiriki wa jeshi katika mipango hiyo. Na katika kupitia mipango hiyo swali la msingi ambalo wanatakiwa watumie (kama guidance) ni hili: ni Tanzania ya aina gani tunataka kujenga? Hiki ndicho kinatakiwa kuwa kiini cha thinking kwa politca elite wetu.

Sasa hivi tuna vision 2025, na huu mpango wa maendeleo uliozinduliwa na rais hivi karibu. Je kwenye hivi vitu viwili Jeshi lina nafasi gani? Au nini defination ya Jeshi katika development strategies za Tanzania? Whether wanataka kushirikiana na Marekani, au China au nchi nyingine yoyote ni lazima wajiulize 'ushirika wetu na huyu au yule unaendana vipi na national development strategies? Lakini kama tutaendelea kufanya kazi kupitia huu mfumo wa 'ad-hoc tutakuwa tunajiandalia laana toka kwa wajukuu zetu. Thinking inatakiwa ibadilike kabisa na haiwezekani rais aendelee kutegemea ushauri toka kwa watu wale wale walimsindikiza kwenye hizi kashfa za cables. He needs to bold and get a new crew otherwise the ship is sinking fast.
 
emmathy

emmathy

Senior Member
Joined
Sep 22, 2010
Messages
147
Likes
11
Points
35
emmathy

emmathy

Senior Member
Joined Sep 22, 2010
147 11 35
Mwanakijiji nikupongeze kuliona hili la wanasiasa kuendesha jeshi na si wananchi kuendesha jeshi, wasiwas wangu yakitokea kama ya syria wanasiasa watalitumia jeshi kuwakandamiza wenye jeshi lao(wananchi), ikiwa ni miaka hamsini ya uhuru nadhani inabidi tutafakari nakutenda kama watu wenye maono si kama watu wakucopy nakupest-kuendelea na jeshi la ulinzi-bali kuwa na jeshi lakuwasaidia wananchi kukua kiuchumi
 
G

gogomoka

Senior Member
Joined
Jun 13, 2008
Messages
124
Likes
2
Points
35
G

gogomoka

Senior Member
Joined Jun 13, 2008
124 2 35
Mwanakijiji,

Hayo maswali yote uliyouliza ni ya msingi na yanahitaji majibu sahihi na ndipo hapo tutakapoweza kwenda mbele. Tunahitaji Major Reform and Re-training kwenye sector ya ulinzi na usalama na ndipo hapo tutaweza kuendelea mbele inavyotakiwa. Leo hii hata kama Chadema watashinda uchaguzi...hiyo existing entranched ideology/propaganda ya kuamini kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho pekee chenye mamlaka ya kuongoza nchi itasababisha constant destablisation ya nchi. Mfano mzuri ni Pakistan Military(using ISI) na PPP (Chama cha Bhutto).
Majibu ya maswali yako ndio yanatakiwa yawe msingi wa Mafunzo kwa Maofisa vijana wanaokuja pale Monduli. Hawa senior officers waliopo wachache ni old timers i.e Waitara ambao hawakubali kuendeshwa na waliiva kwa siasa za chama kimoja. Seniors wengineo wanaangalia kujiweka sawa kama wanasiasa walivyobusy kuiba. Kwa hiyo hakuna wakumtoa mwenzie ila ni ushkaji. Tunaweza kuwaondoa CCM madarakani kama Egypt, lakini nchi ikashindwa kutawalika kutokana na jeshi kuwa na hofu. Inatubidi tujiandae ipasavyo kabla ya kuaffect change. Kwa kuanzia inatubidi tutumie strategy kama ya US wanavyojaribu kwa nguvu sana kupenetrate jeshi letu by "recruiting" our young special forces soldiers kwa kutumia mwanya wa kutoa scholarship za training kwenye military training facilities zao. Nafahamu hiyo ni tradition la kila jeshi kupeleka vijana kusoma lakini Wamarekani wamekuwa aggresive mno na Waitara akawastukia na kugoma(kwa mujibu wa leaked Cables). Vyama vya upinzani (CDM, CUF etc) na wao inabidi watumie tactic hiyo: focus kucultivate relationship na upcoming senior officers ili kujenga confidence na kuaminiana. Itasaidia jeshi kujua opposition partiy sio kibaraka wa UK au US bali ni wish ya Watanzania waliochoka na CCM. Hilo likiwezekana hata CCM wakijaribu kuiba...jeshi litawatimua kwa kuwa linaona upuuzi wote unaoendelea.
MDC/Tschangirai kule Zimbabwe walishindwa kwa kuwa hawana mahusiano yeyote na military ya Zimbabwe. Jeshi haliwaamini kwa hiyo wanaona bora tuendelee na shetani waliyemzoea ZANU-PF.

CDM ijifunze toka kwa Jeshi la Israel, wanahakikisha wanawapa scholarship all young upcoming potential junior officers waliopo WestPoint na Kule Virginia kupata nafasi ya kuona jeshi la Waisrael linafanyaje kazi. Hiyo inawapa nafasi ya kuanza kuform both professional and personal relationships na future Gen.Patreus's etc Hivyo basi hata kuwe na political leadership mbovu vipi jeshi la US linabaki kuwa nguzo ya Waisrael

Nawasiliasha.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,020
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,020 280
Inatubidi tujiandae ipasavyo kabla ya kuaffect change. Kwa kuanzia inatubidi tutumie strategy kama ya US wanavyojaribu kwa nguvu sana kupenetrate jeshi letu by "recruiting" our young special forces soldiers kwa kutumia mwanya wa kutoa scholarship za training kwenye military training facilities zao. Nafahamu hiyo ni tradition la kila jeshi kupeleka vijana kusoma lakini Wamarekani wamekuwa aggresive mno na Waitara akawastukia na kugoma(kwa mujibu wa leaked Cables). Vyama vya upinzani (CDM, CUF etc) na wao inabidi watumie tactic hiyo: focus kucultivate relationship na upcoming senior officers ili kujenga confidence na kuaminiana.
Umesema mambo mazuri kweli kwa mfano naweza kujiuliza itakuwaje kama kiongozi wa upinzani say Dr. Slaa, Zitto au yeyote akaamua kutembelea makao makuu ya jeshi katika ziara rasmi ya jeshi? Je kuna watu wakuwa nervous?

Je itakuwaje kama itagundulika baadhi ya majunior officers wa jeshi wanauhusiano wa karibu na upinzani?

Upande mwingine naamini uhusiano wa Jeshi la Misri na Marekani ulisaidia sana kuzuia jeshi kuingilia kati kumuokoa Mubarak kwa kutumia nguvu. Je hili litakuwa jambo zuri kuwa na jeshi ambalo liko so penetrated na wakubwa hawa kiasi kwamba it become impotent kuweza kuinuka dhidi ya raia wake? Maana utaona jeshi la Yemen na la Misri yote yana mahusiano ya karibu sana na US na yote yamekuwa very muted kwenye kushughulikia upinzani ukilinganisha na jeshi la Libya au Syria.
 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Likes
101
Points
145
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 101 145
Mwanakijiji,

Hayo maswali yote uliyouliza ni ya msingi na yanahitaji majibu sahihi na ndipo hapo tutakapoweza kwenda mbele. Tunahitaji Major Reform and Re-training kwenye sector ya ulinzi na usalama na ndipo hapo tutaweza kuendelea mbele inavyotakiwa. Leo hii hata kama Chadema watashinda uchaguzi...hiyo existing entranched ideology/propaganda ya kuamini kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho pekee chenye mamlaka ya kuongoza nchi itasababisha constant destablisation ya nchi. Mfano mzuri ni Pakistan Military(using ISI) na PPP (Chama cha Bhutto).
Majibu ya maswali yako ndio yanatakiwa yawe msingi wa Mafunzo kwa Maofisa vijana wanaokuja pale Monduli. Hawa senior officers waliopo wachache ni old timers i.e Waitara ambao hawakubali kuendeshwa na waliiva kwa siasa za chama kimoja. Seniors wengineo wanaangalia kujiweka sawa kama wanasiasa walivyobusy kuiba. Kwa hiyo hakuna wakumtoa mwenzie ila ni ushkaji. Tunaweza kuwaondoa CCM madarakani kama Egypt, lakini nchi ikashindwa kutawalika kutokana na jeshi kuwa na hofu. Inatubidi tujiandae ipasavyo kabla ya kuaffect change. Kwa kuanzia inatubidi tutumie strategy kama ya US wanavyojaribu kwa nguvu sana kupenetrate jeshi letu by "recruiting" our young special forces soldiers kwa kutumia mwanya wa kutoa scholarship za training kwenye military training facilities zao. Nafahamu hiyo ni tradition la kila jeshi kupeleka vijana kusoma lakini Wamarekani wamekuwa aggresive mno na Waitara akawastukia na kugoma(kwa mujibu wa leaked Cables). Vyama vya upinzani (CDM, CUF etc) na wao inabidi watumie tactic hiyo: focus kucultivate relationship na upcoming senior officers ili kujenga confidence na kuaminiana. Itasaidia jeshi kujua opposition partiy sio kibaraka wa UK au US bali ni wish ya Watanzania waliochoka na CCM. Hilo likiwezekana hata CCM wakijaribu kuiba...jeshi litawatimua kwa kuwa linaona upuuzi wote unaoendelea.
MDC/Tschangirai kule Zimbabwe walishindwa kwa kuwa hawana mahusiano yeyote na military ya Zimbabwe. Jeshi haliwaamini kwa hiyo wanaona bora tuendelee na shetani waliyemzoea ZANU-PF.

CDM ijifunze toka kwa Jeshi la Israel, wanahakikisha wanawapa scholarship all young upcoming potential junior officers waliopo WestPoint na Kule Virginia kupata nafasi ya kuona jeshi la Waisrael linafanyaje kazi. Hiyo inawapa nafasi ya kuanza kuform both professional and personal relationships na future Gen.Patreus's etc Hivyo basi hata kuwe na political leadership mbovu vipi jeshi la US linabaki kuwa nguzo ya Waisrael

Nawasiliasha.

Mkuu Gogomoka,

Hoja yako ni nzuri sana nakuunga mkono ila kuna sehemu umependekeza vyama vyetu vya upinzani esp CUF&CDM kujaribu kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa Jeshi letu hili, ndio ni vizuri ila tatizo lililopo ni kuwa wana jeshi walio wa chini kabisa ndio wana uhusiano na vyama vya upinzani ila wakubwa zao wamemezwa na ufisadi wa CCM kwa kuleweshwa na pesa za umma hapo kuna tatizo ni kubwa inatubidi kufanya nguvu ya ziada kwa hilo na kupata utaalamu wa kupenetrate
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
13,778
Likes
8,512
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
13,778 8,512 280
Majadiliano haya yananifanya nianze kuelewa kwanini viongozi wa cdm wako makini ku comment au kukosoa sera za USA kwa uwazi!
 
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2008
Messages
812
Likes
91
Points
45
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2008
812 91 45
trust me.., kuna officers na askari wengi sana ambao wanakerwa sana na maamuzi ya wanasiasa..., na ukitaka kuamn hlo angalia uchaguzi uliopita kwenye vituo vilivyo makambini hasa kwny majiji na pia kuna usemi maarufu jeshini..., pale ambapo m2 anakua hawezi kufanya maamuzi magumu anapewa jina la mwanasiasa...,<br />
<br />
Kuhusu kulifanya jeshi kuwa la kisasa.., juhudi zinaonekana japo kwa kasi ndogo.., wasomi wengi wanajiunga na jeshi kwa sasa.., maslahi yameboreshwa sana na kwa sasa nchi ina command 3.., land, navy na adc...,<br />
<br />
Ukisema jeshi linamlinda nani unakosea..., mwananchi lazma ajiskie yuko salama ili kuweza kufanya shughuli za kiuchumi..., na ki-stratejia za kijeshi majirani wote ni probable enemies na ndio maana radar stations na border sentries zinawekwa kistratejia kumuangalia huyo unayemuita jirani.....<br />
<br />
Mengi yanafanywa kuboresha ujuzi na ubora wa jeshi..., mfano, kwa sasa nchi ina marine commandos achilia mbali wale airborne <br />
<br />
La msingi hapa kujua jeshi kama jumuia ina wa2 wana mawazo tofauti..., ila wafanya maamuzi kwa sasa ni ile cream ya zamani waliopitia hata kwny uongozi wa chama.., nadhani si busara kusema jeshi ni hv jeshi ni vile.., na amini nikikwambia kama maslahi yangeendelea kuwa mabaya na hali ya siasa inavyoendelea kwa sasa..., matukio kama ya ubungo yangekua yanatokea kiila siku<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
<br />
wa nchi la nchi imeaminiwa sana hadi kupewa peace-keeping missions darfur na lebanon
 
A

Ame

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
3,357
Likes
668
Points
280
A

Ame

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
3,357 668 280

Pamoja na kuwa wanausalama wengi kama jeshi and the like at individual level wameanza kuenda nje ya dominant culture na syatem ya chama kushika hatamu bado CCM ndiyo dominant system katika kila area ya nchi hii iwe elimu; uchumi; ulinzi; siasa etc kwahili baba wa Taifa alifanikiwa sana. Na kwamba ile adherance and coherence to the system inapungua as days go na watu wanaanza kuona at individual level kwamba its possible to survive without being associated to the dominant system; CCM. Tatizo naloliona ni kuwa wakati Techno instituional complex structure ya CCM iki disintegrate hakuna dalili ya imaging dominant system nyingine na hapa mimi naona kuna hatari kubwa. Kusipokuwa na dominant systems zenye kueleweka kuna tokea kuwa na viji weak systems nyingi nyingi jinsi tunavyoona mfano kwenye vyama vya siasa ukiacha CCM na chadema ambayo inaanza kujijenga na bado hakijiwa na strong greep to the communites kiasi cha kujenga techno institutional complex. Sasa athari ya hili ni kuwa ukiwa na hizo weak kind of institutions ambao individuals wanaweza ku move from one to another bila kuwa costed/risk kunahatari ya ku create chaos na asiwepo hata mmoja wakuweza kui contain. Tunaona baba wa Taifa alikuwa centre of comand katika mambo mengi na alipoondoka ikaonekana wazi kuna kitu kimetoka effect ya kuondoka kwake kila mtu ni shahidi kuanzia kwenye chama chake mwenyewe; governance ya nchi kama maadali ya viongozi etc na pengine hata usalama wa raia na nchi?!(Inahitaji angalizo).

Kwahivyo wakati dominat system ikiji decompose whether strategically ama naturally hakuna nyingine zinazo imerge ku take position ili kuweza ku coordinate issues whether Socio-politically; economically or otherwise. Kwa ku note tu CCM was everything na hivyo it was more than a mere political party sasa ni jukumu letu kuliona hili nakuamua kuanza kujenga mifumo inayoeleweka ambayo hai mimic characters za baba wa taifa (Mtu) ama u-CCM (political party). Tumeona mifano ya nchi ambazo zimeweza ku survive bila kuwa na political leaders lakini maisha yakaendelea kama kawaida na athari ake zikawa siyo significant to the commoners kwasababu kuna mifumo iliyo imara ku contain hizo shocks.

It was a necessity during Nyerere's era kuwa na such kind of a dominat system kama (party-personal based) kwani raia wengi walikuwa bado kuelimika na pia environment ya wakati huo ililazimu iwe hivyo. Bahati mbaya sana wako watu hawataki to let it go kwa sababu za kimaslahi ya kibinafsi zaidi kuliko ki utaifa. Nivizuri sasa kila raia mwenye mapenzi mema na nchi hii kuchukua hatua stahiki kujenga mifumo ambayo inakuwa checked na wengi na usalama wa kila mmoja ukazingatiwa kuliko ilivyo sasa ambapo ni kundi fulani liko more engaged katika mambo ya kitaifa huku majority wakiachwa nje na bdo hao wachache wakiwa na uhakika wakulindwa kwa garama yoyote kufanya wapendavyo.
 
Keynes

Keynes

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
501
Likes
24
Points
35
Keynes

Keynes

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
501 24 35
Mzee mwanakijiji.
Mi watanisamehe kwa kusema kwamba kwa kipindi kirefu nimekua nikijiuliza umuhimu wa jeshi letu kama yalivyo majeshi ya nchi nyingine duniani bila kukosa majibu.

1. kuna sababu gani ya tenda ndogo ndogo za ujenzi wa nchi kama vile feeder road za miji na madaraja kuchukuliwa na makampuni ya nje wakati jeshi lipo?
2. Kuna sababu gani ya kulalamika shule za kata hazina waalimu wa kutosha wakati JKT ipo inaweza ikawa inafanya kazi ya crushing programme kwa wanafunzi wanaomaliza form six?
3. Kuna sababu gani kilimo kuduwaa nchini bila miundombinu ya umwagiliaji wakati jeshi lipo? Ina maana hata ufundi wa ujenzi wa mitaro ya umwagiliaji hawana?

Kwa kua duniani kwa sasa hakuna uvamizi kwa kiasi kikubwa na nchi yetu hatuna makundi mengi jeshi lingetakiwa liwe linatengeneza income kubwa sana na ikiwezekana liwe linajitegemea lenyewe kimiradi na kila kitu.

Mimi hua najiuliza na hua napata majibu kwamba kuitoa ccm madarakani ni ngumu sana maana bado jeshi halina elimu ya kujitofautisha kati yake na serikali....wala halijui kama Raisi ni cheo au taasisi inayotokana na yaliyotamkwa kwenye katiba na wala siyo chama wala mtu binafsi.

CCM wangetakiwa wawe na moyo wa kukubali kwamba siku ikitokea chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza nchi wakiache kwa moyo mmoja ili kuona kama kutakua na mabadiliko...pia itawasaidia wao ku relax na kujifunza mambo mapya kwa wenzao badala ya kuwa chama cha kulaumiwa na wananchi kila siku....Mi naamini kila raia atakubali kuongozwa na rais kutoka pande yoyote kama tu kutakua na utatuzi wa matatizo ya kiuchumi tuliyo nayo.
 
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
44
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 44 0
.................
Sasa hivi tuna vision 2025, na huu mpango wa maendeleo uliozinduliwa na rais hivi karibu. Je kwenye hivi vitu viwili Jeshi lina nafasi gani? Au nini defination ya Jeshi katika development strategies za Tanzania?
Kweye kilimo kwanza nafasi yao ni kusambaza matrekta . Ila ingepedeza zaidi kukawa na strategy kuwa JKT kila mkoa na hata Jeshi la Magerea yakawa na mashamba ya mfano. ili Majeshi yetu yawe mfano wa kilimo kwanza .

Napingana na hoja ya ziito alisposea JKT irudi na wabunge wote ambao hawakwenda waende. Hil sio sahihii ni kupoteza pesa kwa watu wasio sahihi.Wabuunge na watu wengine tayari wana career na taaluma.
  • JKT inatakiwa inagallie namna ya kuboresha skills na kuyamudu mazingira kwa vijana walioshindwa kuendelea na elimu vijijini na sehemu mbalili. Sasa tukianza tena kuwapeleka wabunge na watu wenye kazi zao tayari ndio tunarudi kule kule jeshi la ukombozi wa kisiasa.
  • JKT intakiwa ianglie namana ya kutoa elimu ya uvuvi wa kisasa kwa vijana wa mwanza musoma na agera
  • JTK inatkiwa n namna y utoa elimu ya ufugaji bora kwa vijana kimasai ambao bado wanarithishana mbinu za ufugaji wa kizamani
  • Hakuna seheumu amabapo vijana wanweza kujfunza ufugaji nyuki. So mbinu zinaotumika ni za kiasili.
  • JKT inatakiwa iwe na chuo na mfunzo ya riadha au vituo vya kuibua vipaji vya michezo tupate wanaridha kama kenya.
tulitakiwa tuone Jeshi linashirikiana na VETA mbali mbali ktka program maalum . wanafuni wakimaliza theory za VETA, JTK inachukua kwenda kumalizia ngwe ya mazoezi kwa vitendo kwa miezi kadhaa.
 
A

Ame

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
3,357
Likes
668
Points
280
A

Ame

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
3,357 668 280
Mzee mwanakijiji.
Mi watanisamehe kwa kusema kwamba kwa kipindi kirefu nimekua nikijiuliza umuhimu wa jeshi letu kama yalivyo majeshi ya nchi nyingine duniani bila kukosa majibu.

1. kuna sababu gani ya tenda ndogo ndogo za ujenzi wa nchi kama vile feeder road za miji na madaraja kuchukuliwa na makampuni ya nje wakati jeshi lipo?
2. Kuna sababu gani ya kulalamika shule za kata hazina waalimu wa kutosha wakati JKT ipo inaweza ikawa inafanya kazi ya crushing programme kwa wanafunzi wanaomaliza form six?
3. Kuna sababu gani kilimo kuduwaa nchini bila miundombinu ya umwagiliaji wakati jeshi lipo? Ina maana hata ufundi wa ujenzi wa mitaro ya umwagiliaji hawana?

Kwa kua duniani kwa sasa hakuna uvamizi kwa kiasi kikubwa na nchi yetu hatuna makundi mengi jeshi lingetakiwa liwe linatengeneza income kubwa sana na ikiwezekana liwe linajitegemea lenyewe kimiradi na kila kitu.

Mimi hua najiuliza na hua napata majibu kwamba kuitoa ccm madarakani ni ngumu sana maana bado jeshi halina elimu ya kujitofautisha kati yake na serikali....wala halijui kama Raisi ni cheo au taasisi inayotokana na yaliyotamkwa kwenye katiba na wala siyo chama wala mtu binafsi.

CCM wangetakiwa wawe na moyo wa kukubali kwamba siku ikitokea chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza nchi wakiache kwa moyo mmoja ili kuona kama kutakua na mabadiliko...pia itawasaidia wao ku relax na kujifunza mambo mapya kwa wenzao badala ya kuwa chama cha kulaumiwa na wananchi kila siku....Mi naamini kila raia atakubali kuongozwa na rais kutoka pande yoyote kama tu kutakua na utatuzi wa matatizo ya kiuchumi tuliyo nayo.
Umesema vyema kabisa. Mfano ni jinsi uchumi wa America ulivyo wezeshwa na sera sahihi ambapo technology kwasehemu kubwa iko centered kwenye Jeshi la USA. Ukiangalia innovation and invention za technology pamoja na public procurement zake kabla hazijafikia market level ambapo consumers na suppliers wanaongozwa na market frame work; zinafanikiwa kwasababu ya jeshi lao ambalo ndiyo dominant system yao katika kuwezesha individuals na taasisi zinazoelekea kuwa potentials katika ku-invet ama innovate technologies. Mfano mzuri ni hii revolution kwenye ICT kama vile mitandao ambayo sasa dunia nzima tumeweza kuwa networked ni udhihirisho wa kazi nzuri ya vyombo vya usalama vya USA na hasa jeshi. So si lazima tufanye copy-paste lakini tunaweza nasi tuka build in what is existing kuja na invention zetu za kitaasisi kuleta maendeleo na hapo hapo tukijenga uzalendo na capacity ya kujilinda wakati huo huo.
 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Likes
101
Points
145
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 101 145
Mzee mwanakijiji.
Mi watanisamehe kwa kusema kwamba kwa kipindi kirefu nimekua nikijiuliza umuhimu wa jeshi letu kama yalivyo majeshi ya nchi nyingine duniani bila kukosa majibu.

1. kuna sababu gani ya tenda ndogo ndogo za ujenzi wa nchi kama vile feeder road za miji na madaraja kuchukuliwa na makampuni ya nje wakati jeshi lipo?
2. Kuna sababu gani ya kulalamika shule za kata hazina waalimu wa kutosha wakati JKT ipo inaweza ikawa inafanya kazi ya crushing programme kwa wanafunzi wanaomaliza form six?
3. Kuna sababu gani kilimo kuduwaa nchini bila miundombinu ya umwagiliaji wakati jeshi lipo? Ina maana hata ufundi wa ujenzi wa mitaro ya umwagiliaji hawana?

Kwa kua duniani kwa sasa hakuna uvamizi kwa kiasi kikubwa na nchi yetu hatuna makundi mengi jeshi lingetakiwa liwe linatengeneza income kubwa sana na ikiwezekana liwe linajitegemea lenyewe kimiradi na kila kitu.

Mimi hua najiuliza na hua napata majibu kwamba kuitoa ccm madarakani ni ngumu sana maana bado jeshi halina elimu ya kujitofautisha kati yake na serikali....wala halijui kama Raisi ni cheo au taasisi inayotokana na yaliyotamkwa kwenye katiba na wala siyo chama wala mtu binafsi.

CCM wangetakiwa wawe na moyo wa kukubali kwamba siku ikitokea chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza nchi wakiache kwa moyo mmoja ili kuona kama kutakua na mabadiliko...pia itawasaidia wao ku relax na kujifunza mambo mapya kwa wenzao badala ya kuwa chama cha kulaumiwa na wananchi kila siku....Mi naamini kila raia atakubali kuongozwa na rais kutoka pande yoyote kama tu kutakua na utatuzi wa matatizo ya kiuchumi tuliyo nayo.

Mkuuuuu hapo umelonga si utani
swali la kwanza na la pili yange chukuliwa umuhimu kwanza kama taifa siju kama tunge kuwa hapa wakuu,

My Take:

Swali la kwanza wizara ya ujennzi ituambie pia je huwa wanashirikiana na wajeda katika hilo na kama ndio basi kasi yake ni ndogo na kama bado basi ni wajibu wao wizara kama wizara kushilikiana na wajeda kwa maeneo mugumu especially katika ujenzi wa miundombinu
 
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
5,106
Likes
49
Points
145
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
5,106 49 145
Mzee mwenzangu,

Natumai mzima wa afya na unaendelea na shughuli zako. Siku za nyuma kidogo niliandika swali kwa wabunge linalosema je Tanzania imejiandaa vp na cyber security. Siku nyengine niliandika swali kuuliza kama nchi yetu ina policy yeyote kuzuia ukopaji wa ovyo ovyo usio na kikomo. Kwa kweli yalikuwa ni maswali ambayo mwisho wa siku nilitaka kuuliza swali moja nalo ni JE VYOMBO VYETU VYA USALAMA VIMEJIANDAAJE NA USALAMA WA WATANZANIA?

Kama maswali yangu mawili yaliyotangulia niliuliza kila mmoja angelikuwa na ufahamu anaoujua mwenyewe. Ila binafsi ufahamu na malengo yangu yalilenga kuwazindua wanausalama wetu yaani TISS, Army na Police. Hilo ni kwasababu wakati tunayakumbatia mabadiliko ya uchumi vile vile tuwe tumejiandaa kubadilika na jinsi definition ya usalama au kwa jina maarufu national security. Miaka ya 1970s, 1960s tulikuwa na zama zinaitwa zama za vita baridi na our country ilikuwa ni miongoni mwa nchi zisizofungamana na upande wowote (non-aligned movement). Ilipoanguka soviet union ni marekani sasa hivi ndie anayetawala dunia akishikiriana na washkaji zake France, Uingereza na wengineo. Hilo limepelekea marekani kutanua nguvu zake hadi kwenye rasilimali za nchi nyengine kulinda interest za nchi za magharibi.

Kutokana na hilo ulimwenguni sasa ni kama vile ukitaka kuwa na sisi au face the consequences. Marekani na wenzie wanatumia njia mbali kuzitibua nchi nyenginezo kama kuzitengenezea mazingira ya kuzishambulia (tumeona Libya, Iraq, Afghanistan). Pia hutumia njia za kijasusi kuweza kuwatibua nchi walengwa kwani ya kuwaparaganya na wao kupata kile wanachokitaka (mifano hai ipo kama Angola, Liberia, Egypt). Hilo haimaanishi kwamba tusiwe na ushirikiano na nchi za magharibi bali ni vema vyombo vyetu vya usalama vikajiandaa na ushirikiano na nchi hizo na pia kuwa tayari kukabiliana na changamoto zozote zinaweza kujitokeza.

Dunia ya leo ni mchanganyiko na mabadiliko na hivyo basi Jeshi lijiandae na changamoto hizi ili kuweza kuhakikisha linalinda usalama wa raia wake.

Pia kuna changamoto zinatokea ndani ya nchi mfano cyber crime, espionage nk. Changamoto hizi husababisha na kundi la watu wenye niambaya na nchi yetu. Pentagon ya marekani (wizara ya ulinzi marekani or sometimes inajulikana kama Department of Defence) according CNBC huwa inashambuliwa na majasusi wa kimtandao karibia mara 100 kila siku. Siamini kama mtandao wa jeshi haushambuliwi na majasusi wa mtandao na hivyo basi ni bora kuwepo na uboreshaji wa jeshi la nchi yetu ili liendane na sayansi na technology. Jeshi wanatakiwa na technology ambayo uraiani itachukua miaka pengine kufika na sivyo vyenginevyo.

Pia vyombo vya usalama kama TISS na Police vinatakiwa kubadilika na kulinda raia badala ya watawala. TISS inatakiwa iende na technology na sayansi na pia ibadilike kuendana mazingira ya mabadiliko ya kiuchumi. Mfano kitengo cha Economic Intelligence Unit kinatakiwa kiwe makini kupambana na mafisadi kwani ufisadi ukizidi it becomes a national security matter. Vile vile wanatakiwa kuwa kitengo cha Cyber crime kitakachoshikirikiana na Economic Intelligence Unit kudhibiti external threats, ugaidi na mambo mbali mbali.

Pia ukopaji wa ovyo wa serikali na ufisadi unaweza kuhatarisha usalama wa nchi kutokana na kwamba nchi inakuwa imefilisika. Kufilisika kwa nchi kunapelekea serikali kushindwa kutimiza wajibu wake na kuchochea uvunjaji wa sheria. Mifano hai ipo mfano Greece, Sierra Leone tumeona fujo zilizotoka na ufisadi kuvuka kikomo na serikali kufilisika kumepelekea watu kutoheshimu sheria za nchi na kujiamulia watakalo. Hilo limepelekea mfano Sierra Leone kutokea mauaji ya kutisha na Greece kutokea fujo zisizokwisha kwa sababu ya watu wachache wasioona athari zinazosababishwa na ufisadi na ukosekanaji wa uwajibikaji serikalini.

Dunia ya leo inabadilika na vyombo vyetu vya usalama vinatakiwa kubadilika ili kwenda na wakati. Kuna external and internal threats ambazo hutokea kwa mfano majasusi wanaweza kutumika kuwafitinisha ili mpigane na mwishoe mkaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe (mfano Angola). Vyombo vya usalama vinatakiwa viweze kutambua threats za duniani sasa zinabadilika. Kama ulivyosema mwanzo China wameendelea kiuchumi wa kunyanyua uchumi wao na vyombo vyao vya usalama. Lakini mie pia nakupa mifano mengine ambayo labda hujaiona. Nchi kama Taiwan, South Korea, Singapore, Malaysia, Indonesia nazo pia zimekuwa kiuchumi kwa kuboresha vyombo vyao vya usalama. Kuna walioamua kuwa na ukaribu na nchi za magharibi kama Taiwan, Singapore, Malaysia, South Korea. Kuna wengine waliamua kuwa na ushirikiano wa kijasusi kama Indonesia kwasababu ya ugaidi.

Binafsi sioni tatizo kwa Marekani kushirikiana na kijeshi na kiusalama ila mashirikiano hayo yawe kama Taiwan, Singapore, South Korea na Malaysia kuwa yamelenga katika kuinua uchumi wetu na sio vyenginevyo. Nawashauri wakuu kwa ufahamu zaidi ninachokimaanisha mtafute movie moja inaitwa SYRIANA mtaelewa kitu gani ninachokilenga.
 
Rugambwa31

Rugambwa31

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2009
Messages
227
Likes
4
Points
35
Rugambwa31

Rugambwa31

JF-Expert Member
Joined May 13, 2009
227 4 35
Nakubaliana na maeleo yenu hapo juu. Mm pia nilikuwa najiuliza sana bila majibu, kwann jeshi letu lisiwe lakujenga nchi hasa kipindi hiki.

Tatizo ni jeshi letu kuegemea upande mmoja yani serikali hasa ccm. Maendeleo yote nchi za ulaya yametokana na majeshi yao kufanya kazi usiku na mchana hasa kwenye swala la ICT kama mdau hapo juu halivyo helezea. Leo hii hapa kuingia jesho nimbine tena wanatudanganya wanaitaji wasomi lkn nenda huone wanavyoleta noma kwenye kuchukua hao ni balaa sana.

Mm natamani sana JESHI LA TZ lishikwe na wasomi kwanza na libadilike hili kuleta tija.
1. kuna ma inginia huko, watujengee barabara, mashule, makazi bora kwa raia
2. kuna madaktari huko, wafanye tafiti nyingi pia, wajitolee kutoa huduma hasa vijijini ambako ni tabu sana
3. kuna walimu, tuna shule kibao hazina walimu hasa kata skuls, wakapige kazi huko

Jamani mm naimani kama jeshi likijipanga nakuacha mambo yao kama ya ubinafsi waviongozi baadhi, nasema TZ itakuwa moja ya nchi bora afrika na duniani kote.

Tatizo tz yetu ni ubinafsi tu ndounatumaliza. Kama tukijua kwamba tupo duniani kuakikisha kila mtu anaishi kwa amani na kupata maitaji yake bila kikwazo nakuapia mbona tz itakuwa kama pepo vile.

tupo pamoja, naiona tz yenye neema inakuja mbeleni.
 
Arafat

Arafat

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2009
Messages
2,582
Likes
48
Points
0
Arafat

Arafat

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2009
2,582 48 0
Heshima yako Mkuu, Mwana wa Kijiji!

Ki nadharia na ki vitendo huwezi kujenga uchumi katika dunia hii bila kuwa na Jeshi Imara lililojikita katika Intelijensia na Ulinzi Imara, wataalam wanasema " A country's military capability is derived from its economic capacity and a both country's economic capacity and military powers are what determines its capability to exert and maintain its political, social and economic independence in the world, hence economic power depends on strong Military power" [Tutakuja baadae kuona kuwa kumbe Qadhaffi hakuwa na Uchumi imara ulijengwa juu ya nguvu za Jeshi imara la Umma, ndio Maana kuondoka kwake ili kuwa kama kumsukuma mlevi wa gongo; kumbuka neno Jeshi Imara la Umma], hii Mkuu si kwa Uchumi wa kisasa tu, hapana ni kwa chumi zote hata katika kipindi cha vita baridi lengo kuu na nadhana kuu ili kuwa ni kulinda aina ya siasa tunayoifuata ambayo kwa kifupi ili kuwa ni kulinda uchumi wa kijamaa, kwa sasa majibu, mbinu na uweledi unapaswa kupanuka haraka na kuweka wigo imara zaidi kwa kutumia mbinu za kisasa na kujenga jeshi la Umma, Kama mwalimu alivyopenda liitwe Jeshi la Wanachni wa Tanzania, jina zuri sana. Hivyo kimsingi nakubaliana nawe moja kwa moja.

Kabla sijachangia hoja mama, naomba nikukumbushe kuwa katika hili eneo ndipo Nyerere alicheza na ndipo kuna msingi Mkubwa wa chumi za nchni za Magharibi na kama ulivyosema mwenyewe hata China walipofumbuka macho waliwai kupaweka sawa haraka, na pia hapa ndipo viongozi wengi wa Kiafrica wanapo pakosea na kimsingi ndio chanzo cha vurugu nyingi za Africa na hata kuanguka kwa mataifa yote ya Africa ambapo vita vimewai kutokea. Pia nitoe angalizo kuwa hii hoja yako ni muhimu na imekuja wakati muhafaka maana hata sisi kama Taifa tayari tumesha tetereka na tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Jeshi lenye muono wa kujenga uchumi wa kisasa kwanza lazima liwe Jeshi lilijengwa katika Misingi ya Utaifa na Umma wa nchni husika, na si Misingi ya Mtu na familia yake wala si Misingi ya Chama chochote cha siasa! Msingi wa kujenga Jeshi la kujenga Uchumi tayari Mwal Nyerere alikwisha kuuweka hivyo kama baada ya Nyerere tunge pata waungwana wenyewe uchungu na nchni hii ilikuwa ni kuunganisha nadhalia za kiuchumi na kusonga mbele ila bahati mbaya sana tumerudi nyuma hata kufikia aina ya majeshi kama yale ya Qadhaffi, Nigeria, Liberia, Kongo, nk. Viongozi wengi wa Kiafrika si viongozi wasafi na hawana muono katika kujenga chumi za nchni zao badala ya kujijenga wao kama watu binafsi, ndio maana rushwa na kashfa kama hizo zimejaa africa na kila kona hata hapa kwetu, hivyo viongozi wa namna hiyo hawawezi kuona haya unayoyasema wawo wana waza Kujenga Majeshi imara na tiifu ambayo yata walinda dhidi ya mapinduzi yoyote ya Kisiasa na hivyo wanajenga majeshi kwa ajili yao binafsi na familia zao, ndio maana utaona Jeshi la Libya lilikuwa hadi na Briged inatwa Hamisi ikiwa chini ya Mtoto wa Qadhaffi aitwaiye Hamisi so simple so easy! Huwezi kushangaa katika nchni yoyote ya kiafrika malengo yao sasa ni kujenga jeshi ambalo lipo kwa ajili ya kulinda iwapo kuna mtu atajitokeza kuhoji uhalali wa yanayofanyika katika ardhi ya nchni yake na watawala waliopo, nasikitika kutoa mfano wa Mnadhimu wetu Bwan Shimbo alipojitokeza wakati wa uchaguzi uliopita kama mfano mwingine wa ndani.

Nikirudi katika hoja mama, mchango wangu ni kuwa ili tuweze kujenga Jeshi kama unalolisema tuanzie pale Mwalimu alipotuachia, tuongeze wasomi waliobobea katika Jeshi letu, nadhani unafahamu nchni za Magharibi Jeshi ndio centre za research zote nyeti na muhimu na ndiko kuna bongo zote zilizo tulia, ninaposema wasomi naomba nisieleweke vibaya kuwa ni hawa watu wetu walijaa serikali wenyewe vyeti wakati vichwani hamna kitu! hao siwapendi na siwataki kabisa wabakie tu kumsukuma Jairo na gari lake. Hivyo basi utaona hata mabalozi wetu sasa walipaswa kuwa wana usalama na wanajeshi, tuangalie uwezekano wa military sells kuanzia na uzalishaji wa JKT kuwa bidhaa za kuuzwa nje katika soko la kimataifa, training kwa nchni changa kama southern sudan katika vyuo vyeti vya kijeshi na hata katika vyuo vyao ndani ya nchni yao kwa mikataba minono ya kliuchumi, logistic support za kijeshi na kupanua wigo hata kusipoendeka kama somalia kwa bidhaa zetu maana tuna jeshi imara sasa wakati huo, kujijenga katika mbinu za kisasa za kivita zaidi, nk yapo mengi sana nitarudi baadae kidogo.

Utaona nchni kama USA wapo bisy na cable information za kila aina hizi zote zinakwenda kufanyiwa thathimini za kiuchumi na kiulinzi na hao mabalozi wao wote ni maintelijensia, siyo nyie mnachagua madem wenu na ndugu zenu ndio ilimradi ajira bila kujuwa hata wanafanya nini..
 
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
1,566
Likes
9
Points
135
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
1,566 9 135
Kweli mkuu MMM umesema , Jeshi letu bado liko kwenye zama za Chama kushika hatamu ndiyo maana mwaka jana walipoona hali ni tete wakajitokeza na kupigia debe chama chao. Lakini katika hali hii leo vyama vingine vya siasa vinaweza kupokelewa na kukubaliwa na jeshi? Hali ilivo sasa tuhuma nyingi za ubadhirifu zinzhusisha chama tawala (Msekwa anapinga jina hili) na serikali na Jeshi kwa upande mwingine maana yake viongozi wa majeshi yetu wamegeuka na kushirikiana wanasiasa (walioko madarakani) kuhujumu mali na uchumi wa nchi, ndoa yao hii ni hatari sana kwa demokrasia yetu.
Katika hali hii ya amani (hakuna vita) jeshi linapaswa kujiunga na kutoa huduma mbali mbali kama kutoa elimu (kuna waalimu wengi jeshini), huduma za afya, ujenzi wa shule, zahanati za kata, barabara, madaraja na siyo kukaa tu makambini bila kazi, hata hiyo KILIMO KWANZA imegubikwa na tuhuma kibao jeshini kuwa ni miradi ya viongozi wa jeshi. Hakuna impact yoyote kwenye kilimo kwanza kutoka jeshini. Safari bado ni ndefu.
 
BinMgen

BinMgen

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
1,828
Likes
35
Points
145
BinMgen

BinMgen

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
1,828 35 145
Nakubaliana nawewe ila kipengele kimoja tu, kwamba kwavile huoni kitisho chakuvamiwa na Wareno na SA unahisi jeshi halinakazi tena ya ulinzi na badala yake unataka jeshi lifanye shughuli nyengine, hapa kwa mtazamo wangu hauko sawa, jeshi linakiwa kuwa active muda wote kwani adui hakuletei barua.
 
Forum statistics

Threads 1,235,090
Members 474,351
Posts 29,211,811