JWTZ na helikopta za Mtumba

Hii iliyopata ajali ni matokeo ya huo ununuzi batili?

Absolutely! Alinunua huyohuyo Vithilan na jeshini pia, Nakumbuka za jeshi mbili zilianguka kipindi kilekile, Moja iliangukia serengeti jamaa wakipiga picha za Kitallii. Ndio maana Jana mimi nilisema Wafe tu hao wakina Kova maana hayo ni matokeo ya Ufisadi wao.
 
Absolutely! Alinunua huyohuyo Vithilan na jeshini pia, Nakumbuka za jeshi mbili zilianguka kipindi kilekile, Moja iliangukia serengeti jamaa wakipiga picha za Kitallii. Ndio maana Jana mimi nilisema Wafe tu hao wakina Kova maana hayo ni matokeo ya Ufisadi wao.

Nakubaliana na wewe bora wangekufa tu labda ndo wangepata fundisho
 
Naelewa kuwa hili la helikopta za mitumba liliwahi kuzungumzwa hapa JF na michango kadhaa imetolewa. Hata hivyo kuna kitu kimenisukuma kutaka mada hii wana-JF tuliangalie kwa mapana zaidi. Kinachonijia akili kwa mtazamo wangu huenda ni kutojali au ujeuri wa wahusika katika kulifatilia kwa umakini jambo hili na angalau kuchukua hatua.

Nijuavyo baada ya helikopta hizo aina ya Agusta Bell model 412 EP kununuliwa kwa utaratibu batili watu walinyooshea kidole JWTZ na Usalama wa taifa. Sina kumbukumbu ya kilichofata zaidi ya kusoma kwenye magazeti juu ya kesi ya kudai fidia ilifonguliwa na kampuni ya Khasia Enterprise LTd kudai fidia kutoka JWTZ kwa kuvunja mkataba wa ununuzi wa helikopta hizo.

Kilichonisukuma zaidi kuweka hii topic hapa kwa mara nyingine ni jinsi gani uzembe na urafi wa watu wachache unavyosababisha maisha ya watu wengine kupotea...Kati ya helikopta 4 zilizonunuliwa, 2 zimeshaanguka na watu wamepoteza maisha. Kwa maoni yangu kama waliohusika na uchafu huu hawatachukuliwa hatua kuna uwezekano mkubwa hili likajirudia tena. Kwani kuna tabia ya binadamu kuangalia matokeo ya tatizo la kwanza alillosababisha.

Pia napata ugumu na mtiririko mzima wa ununuzi wa helikopta hizi na kuhusika tena kwa Shailesh Vithlani ambaye inasemekana alihusika pia katika ununuzi batili wa rada. Huyu muhindi ana mazingaombwe gani ya kutufunika watanzania hadi kutuibia kiasi hiki?? Kwani huyu muhindi aliwatia mchanga wa macho maafisa kadhaa wa JWTZ kukubali awatafutie hizo helikopta kwa bei ya dola za kimarekani milioni 9.2 badala ya bei ya awali iliyotolewa na Khasi Enterprises Ltd ya dola za kimarekani milioni 4.7 kwa kila helikopta.

Napata uchungu jinsi tunavyogeuzwa wajinga kwa kuibiwa mchana kweupe wakati huo huo maisha ya watu yakipotea. Nina imani hata famili za marehemu waliokufa katika ajali ya moja ya hizo helikopta huko Arusha wakilijua ( huenda wanalijua kupitia vyombo vya habari)hili itawauma sana ingawa wote tunaamini kuwa kifo kimepangwa lakini kuna uzembe mahali fulani.

Nashauri hata hizo helikopta 2 zilizobaki zisitumike tena kuepusha madhara mengine zaidi. Na hao maafisa wa JWTZ waliohusika na ununuzi wenye milungula hebu wafikishwe kwenye vyombo vya sheria jamani.

Samahani kama kuirudisha mada hii tena kutawakwaza wana-JF lakini lengo langu ni kutaka tuliangalie hili jambo kwa mapana zaidi.

Naomba kuwasilisha.
Hv bongo hakuna private investigator company zaidi ya hawa waandishi wa habari,kama zipo waibue mambo ya kufanya watambulike.
Kama cruel zipo za kutosha kwanini uchunguzi usifanyike maana huku serikalini utanyamazishwa mdomo kisa ni SIRI YA USALAMA WA TAIFA NA HABARI HUISHIA HAPO.
 
Wahindi ndio wezi wakubwa ila wanajia jinsi ya kutoa rushwa pia. Bora mchina kuliko Mhindi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom