JWTZ mpaka leo imeshindwa kuajiri wasomi wenye vipaji halisi, sababu hizi hapa...

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,609
4,096
Ukiangalia mfumo mzima wa ajira utabaini yafuatayo
1. Waalimu waliopo vyuoni 90% ni kikwazo kwa wasomi wengi wanaojiunga na jeshi hilo, akitokea mwanafunzi mwenye elimu kubwa hata Phd watafanya kila mbinu wamfukuze kwa kisingizio cha utovu wa nidhamu au watacomment kuwa kafeli.

2. Trainning zao hazija base kutafuta vipaji vya kweli katika nyanja muhimu kitaifa, kama vile madaktari, Eng, nk. Mfano Nyumbu mpaka leo wameshindwa kuifanya iwe ya kizalishaji toka enzi za mwalimu. Lugalo mpaka leo hawana hata blood bank sababu wanasayansi tiba hawapo ndio maana wanashindwa kukabiliana na migomo ya MH, sababu huko wengi 80% ni AMO na CO.

3. TMA ni kikwazo kikubwa sana katika kuwapata wasomi wazuri ndani ya jeshi hilo, elimu ya rasilimali watu kwa waalimu inawezekana ikawa ni issue. So they are trying to reduce the number of students kwa visingizio vya nidhamu ambayo ukifuatilia kiundani sio nidhamu as such but ni kutojua ubaya wakumfundisha mtu at certain level na kumwachisha mafunzo. HILO N BOMU BAADAYE.

4. Mazingira dhaifu kuwawezesha wenye vipaji kubuni kwa uhuru na kutumia taaluma zao, kufanya tafiti chanya maeneo yao ya kazi, mpaka leo hatujaziona.

5. Officer aliyetokea uraiani moja kwa moja I mean those who have got a little knowledge kuwa mkufunzi, atafundisha nini kama sio kupika majungu na kukosa comfidence?

Hayo machache yaliyobainishwa hapo juu ni chanzo kikubwa cha jeshi letu kuwa kama lilivyo hivi leo.
 
Nina masters ya Law ( LLB) na natarajia kujiunga na JWTZ mwakani.
Hiyo master of law ambayo umeiita LLB labda itakuwa imetoka chuo cha kata,bora usingeweka hata hicho kifupisho maana umeonekana ulivyo mtupu na haiyo llb yako ndio maana unataka kujificha huko jwtz kwa kuwa huwezi kufanya chochote kwenye uwanja wa sheria.
Tukiacha hayo sijui kuna ukweli/uongo gani katika hoja ya mleta mada.
 
Unaonekana unalazimisha kuajiliwa ....Jeshi si kampuni kama ya mkonge!
 
inaonekana kama ulifukuzwa monduli...,

kwa kifupi, pamoja na kipaji ulichonacho nidhamu ndiyo pillar ya mafunzo yako,, jeshi ni nidhamu, period! Na nidhamu ndio inaleta ufanisi kwenye uwanja wa vita, unapotoa amri mfuasi akatumbukize hand grenade kwny kifaru cha adui, hatakiwi kujiuliza hata kwa sekunde moja.., na hii nidhamu inajengwa kwenye mafunzo, ndio maana jeshini kuna adhabu za kipuuzi kabisa,, mfano unaambiwa umwagilie maua wakati mvua inanyesha,,, ukileta mambo ya logic utaona kua mkufunzi wako ni mpuuzi hana akili,,,, lakn thts part of disciplining you,, ufanye ulichoamrishwa hata kama hupendi,, na hii sio kwa jwtz tu, proffesional armies zote wana namna mbalimbali ya kufundisha nidhamu..,

Kuhusu kuajiri vipaji,,, kwa hili nakubaliana na ww kabisa kwamba japo jeshi linaajiri wasomi na siku za karibuni wanaajiri kwa wingi zaidi, ila bado kuna upungufu mkubwa sana wa wasomi wa fani mbalimbali,, lakini pia tutambue jwtz ipo kwenye transition period,,, kuna individuals ambao hawapendi kabisa hawa watoto wasomi wanaingia na kutoka na manyota fasta,, resistance kwenye change lazima iwepo, ila in general jeshi limeamua liwe dogo na la kisomi na ndio maana kwa sasa hakuna std 7 anaajiriwa wote ni form four and above unless ni mwanamichezo au ana kipaji flani cha sanaa...,

Ukiondoa isolated incidents za wakufunzi wachache kuwachukia wasomi,,, wakuu ngazi za juu wanataka jeshi dogo la kisasa na la wasomi..., na pale monduli bana ukichukiwa na wakufunzi,,, chances za kumaliza ni ndogo sana,,,

Nawaasa watakaopita interview inayokuja hivi karibuni,, pale monduli jishushe,, ni yes sir, yes staff, hata kama task ulopewa logically doesnt make sense
 
Moshe Dayan najua when it comes to mambo ya JWTZ uko very deep.
Swali langu kwako ni hili, kama kweli jeshi linafanya reform na kuanza kuajiri wasomi wengi lakini kwa utaratibu wa jeshi hao wasomi lazima wafaulu shughuli ya monduli, na huko monduli ndiko kunatuhumiwa kuwa na matrainer wanoko hasa wale wa vteo vya chini.
JWTZ inafanya juhudi gani kuondoa huo unoko/uonevu ili wataalamu/waomi hao watumie taaluma zao kwa manufaa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Na kwa nchi zilizoendelea wasomi wanaojiunga na majeshi wanakuwa treated ''kinyaninyani'' kama mnavyowafanyia monduli?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umenena ukweli mtupu tatizo wakubwa wengi Jeshini elimu zao za kimagumashi.

Si kweli..., kama utaweza kupata ushahidi kwamba kuna senior officer kuanzia brig.gen kwenda juu mwenye elimu ya kimagumashi,,, naomba mods wanipe ban ya maisha,, maana hizo ndizo ngazi za maamuzi kijeshi.., ukipata hata mmoja tu kwa jeshi la sasa mm naomba ban ya maisha
 
inaonekana kama ulifukuzwa monduli...,

kwa kifupi, pamoja na kipaji ulichonacho nidhamu ndiyo pillar ya mafunzo yako,, jeshi ni nidhamu, period! Na nidhamu ndio inaleta ufanisi kwenye uwanja wa vita, unapotoa amri mfuasi akatumbukize hand grenade kwny kifaru cha adui, hatakiwi kujiuliza hata kwa sekunde moja.., na hii nidhamu inajengwa kwenye mafunzo, ndio maana jeshini kuna adhabu za kipuuzi kabisa,, mfano unaambiwa umwagilie maua wakati mvua inanyesha,,, ukileta mambo ya logic utaona kua mkufunzi wako ni mpuuzi hana akili,,,, lakn thts part of disciplining you,, ufanye ulichoamrishwa hata kama hupendi,, na hii sio kwa jwtz tu, proffesional armies zote wana namna mbalimbali ya kufundisha nidhamu..,

Kuhusu kuajiri vipaji,,, kwa hili nakubaliana na ww kabisa kwamba japo jeshi linaajiri wasomi na siku za karibuni wanaajiri kwa wingi zaidi, ila bado kuna upungufu mkubwa sana wa wasomi wa fani mbalimbali,, lakini pia tutambue jwtz ipo kwenye transition period,,, kuna individuals ambao hawapendi kabisa hawa watoto wasomi wanaingia na kutoka na manyota fasta,, resistance kwenye change lazima iwepo, ila in general jeshi limeamua liwe dogo na la kisomi na ndio maana kwa sasa hakuna std 7 anaajiriwa wote ni form four and above unless ni mwanamichezo au ana kipaji flani cha sanaa...,

Ukiondoa isolated incidents za wakufunzi wachache kuwachukia wasomi,,, wakuu ngazi za juu wanataka jeshi dogo la kisasa na la wasomi..., na pale monduli bana ukichukiwa na wakufunzi,,, chances za kumaliza ni ndogo sana,,,

Nawaasa watakaopita interview inayokuja hivi karibuni,, pale monduli jishushe,, ni yes sir, yes staff, hata kama task ulopewa logically doesnt make sense
Mkuu hilo ndilo jeshi, usiende pale Monduli kutafuta nyota ukatanguliza shahada zako, hizo zitakuja fanya kazi baadae!! Kwanza uwe discipline upate harassment ili uwe askari mzuri, mambo ya jeshi yanahitaji utii, fikiria bomu limetupwa hapo chini unaambiwa down, wewe unajishauri kwa nini si tutakuokota vipande vya nyama???? Kamanda mzuri lazima awe na discipline, hapo tutapata best soldier !!!! Pole kama ulikwenda ukashindwa kupaform, tekeleza amri maswali baadae!!!

Moshe Dayan najua when it comes to mambo ya JWTZ uko very deep.
Swali langu kwako ni hili, kama kweli jeshi linafanya reform na kuanza kuajiri wasomi wengi lakini kwa utaratibu wa jeshi hao wasomi lazima wafaulu shughuli ya monduli, na huko monduli ndiko kunatuhumiwa kuwa na matrainer wanoko hasa wale wa vteo vya chini.
JWTZ inafanya juhudi gani kuondoa huo unoko/uonevu ili wataalamu/waomi hao watumie taaluma zao kwa manufaa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Na kwa nchi zilizoendelea wasomi wanaojiunga na majeshi wanakuwa treated ''kinyaninyani'' kama mnavyowafanyia monduli?
Mkuu mambo ya jeshi yako hivyo hivyo matrainer wengi elimu zao ni za chini, tafuta hata record za WESTPOINT kwa jeshi la AMERICA au Loyal College UK kupitia cadet school lazima uwe harassed ili apatikane soldier mzuri especially officer ambaye ni commander wa unity!!! Mkuu tafuta training program ya majeshi mbali mbali hasa western armies!! Huwezi kupata best officers kama hujawatoa uraia ingawa mara nyingi wanapewa short courses badala ya long program!! Wataalamu wanapewa special treatment wanapomaliza course, hivyo vijana wavumilie tuu undava ili baadae wafaidi!!

Back
Top Bottom