JWTZ kuvunjwa -- kuanzishwa kwa Jeshi la Shirikisho la Afrika Mashariki (JSAM)

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
JWTZ inasubiri adui aje na mizinga na makombora akitaka kuteka nchi ndio wapambane naye. Lakini adui akija na makaratasi (yaliyoambatana na posho?) kama vile EAC, hawana habari naye, hata kama anatimiza malengo yaleyale, na kuzidi, kama angejaribu kuja kwa makombora.

Kwa kuwa JWTZ ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ambayo jamhuri na mipaka yake inafutwa na EAC, Uhamiaji nao unakuwa wa EAC (a.k.a viza moja), hakuna sababu tena ya kuwa na JWTZ, ambayo kazi yake tunaimbiwa kuwa ni kulinda mipaka ya Tanzania, bali tuwe na Jeshi la Shirikisho la Afrika Mashariki (JSAM),kama ambavyo jitihada zinavyokamilishwa.

Tayari mipango iko pia mbioni
kufuta Jeshi la Polisi la Tanzania na kuanzisha la Afrika Mashariki.

Kadhalika, Usalama wa Taifa Tanzania utafutwa na kuanzishwa ule wa EAC
ili kupunguza gharama.

Sources:
- Skyscrapercity Website
- Jaluo blog
- All africa website
- Newvision website
- Business daily Africa website

Asante Mkuu kwa kuweka makala na linki kibao. Jamani, hayo maneno yenye rangi ni linki.
 
Haitawezekana kuvunja Jeshi la polisi au JWTZ na kuanzisha la EA.Nimesoma hizo links,inavyoonesha ni kuongeza ushirikiano katika mambo ya kiusalama.Kwanza ni kitu kisichowezekana kwa sababu hatujaungana kuwa nchi moja,ni ushirikiano wa kiuchumi tu.Labda baadae mambo yakienda vizuri tunaweza kuanzisha ushirikiano wa kiulinzi kama ilivyo NATO.
 
Kwanza shukran kwa joellincoln na Sikonge.

Haitawezekana kuvunja Jeshi la polisi au JWTZ na kuanzisha la EA.

Joss, unanikumbusha kila Mdanganyika anapobainishiwa maana ya EAC reaction huwa ni hiyohiyo: "Haiwezekani!", "Hatutakubali", "We ni zee jongo!", "Unatunga tu", "maneno unayosema ni makali!", "tunashirikiana kiuchumi tu" n.k., hata kama maandishi yapo wazi.

Natamani ningekuwa kama ninyi wenzangu ambao hamuoni maafa ya EAC yanayokaribia kulikumba taifa letu.

Mlenge
 
"The process is geared towards the creation of a regional Police force as the partner states approach political federation, expected to be concluded by 2013.

The chairperson of the sectoral council on inter-state security, Sophia Simba, said the security sector was instrumental in identifying threats that may delay the integration." -- New Vision

Hiyo 'regional' hapo maana yake siyo 'mkoa'!
 
East Africa: Region Moves Closer to Having Regional Army
In New Vision
 
JWTZ inasubiri adui aje na mizinga na makombora akitaka kuteka nchi ndio wapambane naye. Lakini adui akija na makaratasi (yaliyoambatana na posho?) kama vile EAC, hawana habari naye, hata kama anatimiza malengo yaleyale, na kuzidi, kama angejaribu kuja kwa makombora.

Kwa kuwa JWTZ ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo jamhuri na mipaka yake inafutwa na EAC, Uhamiaji nao unakuwa wa EAC (a.k.a viza moja), hakuna sababu tena ya kuwa na JWTZ, ambayo kazi yake tunaimbiwa kuwa ni kulinda mipaka ya Tanzania, bali tuwe na Jeshi la Shirikisho la Afrika Mashariki (JSAM), kama ambavyo jitihada zinavyokamilishwa.

Tayari mipango iko pia mbioni kufuta Jeshi la Polisi la Tanzania na kuanzisha la Afrika Mashariki.

Kadhalika, Usalama wa Taifa Tanzania utafutwa na kuanzishwa ule wa EAC ili kupunguza gharama.

I suppose this is day dreaming at its worst!!
Hivi mkuu, na Amri Jeshi mkuu anahamia wapi Nairobi,Kampala Kigali au Bujumbura?
Kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu, maswala nyeti haya!!
 
EAC inaundwa kwa kufuata katiba za nchi husika. Vyombo vya Serikali ambavyo vipo kikatiba haviwezi kuvunjwa ama kupokonya mamlaka yake, vinginevyo katiba za nchi husika zimefanyiwa marekebisho.
 
I suppose this is day dreaming at its worst!!
Hivi mkuu, na Amri Jeshi mkuu anahamia wapi Nairobi,Kampala Kigali au Bujumbura?
Kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu, maswala nyeti haya!!
Amirijeshi mkuu anakuwa Jenerali Museveni (Mungu ampe nini?), halafu anamkabidhi Jenerali Kagame, halafu kabla ya zamu ya Kikwete kufika, uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais wa Afrika Mashariki unafanyika.
 
EAC inaundwa kwa kufuata katiba za nchi husika. Vyombo vya Serikali ambavyo vipo kikatiba haviwezi kuvunjwa ama kupokonya mamlaka yake, vinginevyo katiba za nchi husika zimefanyiwa marekebisho.
Si kweli. EAC inaundwa na mikataba na itifaki ya EAC, ambayo iko above sheria na katiba za nchi husika.
 
Si kweli. EAC inaundwa na mikataba na itifaki ya EAC, ambayo iko above sheria na katiba za nchi husika.

Hakuna kitu kama hicho, EAC haipo juu ya katiba za nchi husika, ingekuwa hivyo Kikwete, Kibaki na wenzao wangekuwa wameshajiuzuru kwa kukiuka katiba.

Suala la katiba ni kubwa ndugu yangu, EAC haiwezi kuvunja jeshi wala chombo chochote kilichowekwa kikatiba katika nchi wanachama. Ndo maana makubaliano yao kule ni mpaka yapitishwe na mabunge husika hata kama Marais wanakuwa wameshasaini. Suala la kubadili katiba linafuata azimio la Butiama tehe tehe tehe (i mean kura ya maoni ya wananchi wote).
 
Mosby's Medical Dictionary, 8th edition. © 2009, Elsevier. Defines Denial as "an unconscious defense mechanism in which emotional conflict and anxiety are avoided by refusal to acknowledge those thoughts, feelings, desires, impulses, or facts that are consciously intolerable. " (Denial (psychology) - definition of Denial (psychology) in the Medical dictionary - by the Free Online Medical Dictionary, Thesaurus and Encyclopedia.)

It is all part of subconscious defence mechanism. (Teaching Clinical Psychology - Defense Mechanisms)

Denial is a psychological reaction that is found even at national level (Denial - children, therapy, adults, examples, person, people, used, personality, theory, Definition, Theory of denial, Examples of denial, Treatment of denial).

So I can understand your denials, though you see with your own very eyes information to the contrary of what you deny.

Once you overcome this denial, we can devise strategies to save our dear country, before it is too little, too late.
 
Wanaposema sasa kuna amani,
ndipo uharibifu huja ghafla,
wanapokutana kupanga mipango,
mataifa kuwa kitu kimoja,
hawataungana bali watazidi tengana mbali.
Wangelisoma neno la Mungu,
watafakari unabii,
wasingesumbuka wangeenda kwa Yesu
wapate amani ya kweli...........
(Huu ni wimbo niliousikia hivi karibuni redioni)

Someni maandiko na muyaelewe.
 
"The process is geared towards the creation of a regional Police force as the partner states approach political federation, expected to be concluded by 2013.

Mkuu Mlenge sijui ni kwa makusudi au kwa bahati mbaya mbona hukuweka maneno haya, ambayo kimsingi yanaondoa hofu ya kufutwa kwa jeshi la polisi "....Security and internal affairs ministers, together with the regional Police chiefs, on Friday signed recommendations that would ensure a co-ordinated workforce....."
 
Back
Top Bottom