JWTZ kupiga doria barabarani: Mwamunyange ameenda mbali mno...

HAKUNA tatizo kwa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (TPDF) kuingia mitaani na kusaidia kusimamia sheria na kulinda amani.

Tatizo lililopo ni kuwa
hawajatuambia kama Jeshi
letu la Polisi ambalo ndilo
lenye wajibu wa kulinda
amani na utulivu na
kuhakikisha usalama wa raia limeshindwa kazi yake. Kuna sababu moja tu ya Jeshi (army) kuruhusiwa kuingia mitaani kushughulikia matatizo ya kiraia;
wakati Jeshi la Polisi limezidiwa au limeshindwa.

Hili ni muhimu kulielewa. Jeshi la Polisi ndicho chombo ambacho kimeundwa kisheria kushughulikia usalama wa raia na utulivu nchini.

Ndicho chombo chenye jukumu la kuzuia uhalifu, kusaka wahalifu na kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali. Ndicho chombo basi ambacho wananchi wanatakiwa kukizoea katika maisha yao linapokuja suala la usalama wa maisha, mahali, na mali
zao.

Upande mwingine Jeshi lina jukumu la tofauti sana na Polisi. Kwa vile wote wanavaa sare na wanapigiana saluti
kuna watu wanaweza
kufikiria majeshi haya mawili yanaweza kubadilishana;
Polisi wakawa Wanajeshi na Wanajeshi wakawa Polisi.

Jeshi wana jukumu kubwa la kwanza kabisa ambalo ni kulinda “mipaka yetu”. Mara nyingi watu wanaposikia “kulinda mipaka” wanachukulia kuwa ni kulinda tu mipaka pembezoni mwa nchi.

Kimsingi “kulinda mipaka”
maana yake ni kuhakikisha
kuwa nchi yetu inakuwapo na eneo lake linaheshimika
(territorial integrity). Katika hili ni jukumu la Jeshi kuhakikisha kuwa nchi jirani hazitishii eneo letu na hivyo
haziwezi kuchukua hata nchi moja ya eneo leo. Ndiyo maana wakati wote Idi Amin analeta chokochoko tulijaribu kwa njia nyingi za
kidiplomasia kushughulika
naye lakini alipovuka mstari kwa kuingia katika ardhi yetu ana kuidai ni yake hatukuwa na
uchaguzi mwingine zaidi ya kuhamasisha Jeshi kuingia vitani. Hii ni ile sehemu inasema kulinda nchi kutoka kwa maadui wa “nje”.

Lakini kuna kazi nyingine ya tofauti ya Jeshi ambayo
inahusiana na hiyo ya kwanza; kulinda nchi kutoka kwa
maadui wa ndani. Kiapo hiki cha kulinda nchi kutoka kwa maadui wa ndani hakina
maana wahalifu, vibaka au
wezi. Hii ni kazi ya Polisi.
Tunapozungumzia maadui wa “ndani” tuna maana wale watu ambao nao kama maadui wa nje wanatishia uhai wa Taifa letu.

Maadui wa ndani wenye
kutishia Taifa wanaweza
kuwa ni wanasiasa au
viongozi walioko madarakani.
Hii ndiyo sababu kwenye
baadhi ya nchi ambapo taasisi za kisiasa zinapokuwa zimeshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi Jeshi
linashika madaraka (kwa
mapinduzi).

Hili lilitokea Misri baada ya
kuanguka kwa serikali ya
Hosni Mubarak. Hata hivyo,
pamoja na vurugu zote
zilizokuwa zinatokea, Jeshi la Misri halikuingia mitaani kuanza kusimamia kazi za Polisi mpaka pale mchakato wa kisiasa na kimapinduzi ulipokamilika.

Jeshi la Polisi limeshindwa?

Ili tuweze kuhalalisha au labda niseme “waweze kuhalalisha” JWTZ kuingia mitaani na kuzunguka katika makarandinga yao ni lazima kwanza wakubali kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa.

Ikumbukwe tayari wengine
tulishajenga hoja kuwa Jeshi la Polisi ni bovu, viongozi wake wazembe, na maono yake ni ya ki CCM.
Limeshindwa kujipanga na kuwa la kisasa na limeendelea
kuwa lenye mtazamo wa
kisiasa.

Tumeshuhudia jeshi hili
lilivyogeuka kuwa adui wa
demokrasia na kuwa
kandamizi dhidi ya upinzani wa kisiasa. Matokeo yake
limekuwa na haraka kukandamiza upinzani wa
kisiasa na kuminya haki za
raia kusimama dhidi ya
serikali yao. Matokeo yake
limejiaminisha kuwa
linajukumu la kulinda watawala na si kulinda
wananchi wakitumia haki zao za kisiasa.

Hoja ya Lula wa Ndali Mwananzela,Raia mwema 24 oct 2012
 
kama umegundua kukitokea fujo wanaoletwa ni FFU na sio polisi wa kawaida...ni kwamba polisi wa kawaida kazi yao ni kufanya paper work vituoni? kusimamisha magari na kuangalia kama yana insurance na wenye magari wana leseni? maana inaonekana inapokuja vurugu ffu ndio pekee wanaoweza kuzuia fujo na sio polisi sasa sijui polisi wao kazi zao ni nini, sasa hivi hata ukiingiliwa unaona ni bora kuita security company kama KK security watafika mapema nyumbani kwako kuliko ukiita polisi kama mtoa mada alivosema hapo juu ni bora jeshi la polisi livunjwe sioni really wanachofanya zaidi ya kutubambikia kesi, kutaka rushwa na kuonea jamii hasa wasiokua nacho
 
jerry mulo anawajua! ila aliwaaibisha.

Aliwaaibisha kivipi mkuu wakati alisema ukweli kwa kuwatoa kwenye luninga. Asilimia nyingi ya watanzania wanajua fika kwamba kazi za jeshi la polisi ni kama zifuatazo:

1. kuwabambikizia kesi watu wasio na hatia.. hata mkuu wa nchi analifahamu hili...

2. Kuomba rushwa ya kila namna ili mradi kitu kiende mfukoni au kinywaii mwao (sababu ya maisha duni na kazi zao ... wanaishi full suit na kutegemea kujikomboa toka kwenye magodown ya nyumba za bati)

3. kuwapa wahalifu taarifa za watu waliowashtaki wahalifu hao

4. Kutofika katika maeneo ya uhalifu au tukio kwa wakati wa haraka sema kama dakika tano tangu tuko litokee

5. kufanya kazi kwa kuwapendelea ccm na wafanyabiashara

6. kuwa makalani wa kuandika RB ambazo hazifuatiliwi kwenye vijikarasi visivyo na nembo ya polisi, muhuli wa polisi au tarehe na mwandishi wa RB hiyo.

7. Mwisho ni kutokuwa impartial, independent na confidence na kazi zao kwa ujumla... wanafanya kazi kwa remote control labda kwa sababu asilimia kubwa ni polisi wa voda fasta su shule za kata ...

8. Wavivu wa kutojiendeleza kishule, kitechnologia na kuendana na dunia ya internet na uharifu kwa wakati huu wa kisasa

kufutwa kwa polisi hakutasaidia kitu kama mfumo mzima wa kuboresha productivity yao kuanzia recruitment ya wanaostahili, kuongeza masurufu ya kazi zao ili waondokane na vishawishi vya rushwa kama TRA na kuwezeshwa kwa kutumia technology ni mambo ya haraka yanayotakiwa kufanywa kabbla ya kufutwa kwa polisi
 
Back
Top Bottom