JWTZ kupiga doria barabarani: Mwamunyange ameenda mbali mno... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ kupiga doria barabarani: Mwamunyange ameenda mbali mno...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Richard, Oct 20, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Kwa wananchi wanaofahamu tofauti ya jeshi la polisi na jeshi la wananchi wa Tanzania, leo imeonekana kwamba kuna tatizo.

  Kwa wale wananchi wasiofahamu tofauti ya majeshi haya mawili wameona ni sawa na ni jambo la kushangaza kidogo la kuleta msisimko fulani.

  Polisi wakiwa na jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao, JWTZ wao ni kulinda nchi kwa ujumla na mipaka yake.

  Vurugu ambazo zimekuwa zikipikwa kidogokidogo zinaweza kukabiliwa na jeshi letu la polisi na sio JWTZ ambao wangeshughulikia matatizo na chokochoko kutoka nje ya Tanzania.

  Polisi ni chombo cha serikali chenye kutekeleza sheria "law enforcement" zinazotungwa na serikali ikiwemo sheria ya kutofanya fujo. JWTZ ni taasisi inayojitegemea ikiongozwa na mkuu wake wa majeshi likijumuisha vikosi vyote vya anga, ardhini, na majini.

  Jamani hapa pana kasoro tena ni kasoro kubwa kwa maana mkuu wa nchi hakuwepo vurugu zilipoanza na hata kukamatwa kwa Sheikh Ponda na polisi na kule Zanzibar kukamatwa kwa Sheikh Fareed. Pia waziri Mkuu wake bwana Pinda alitorokea London kufanya mkutano na watu 300 tu! Mkutano ambao lengo lake halijajulikana hadi sasa kwa wale wachambuzi.

  Sasa wale waliobakia kuongoza nchi wameshindwa kuona tofauti ya kuagiza nani atulize ghasia na ndio tunaona kosa la kiufundi la kutuma polisi na jeshi la ulinzi mitaani.

  Nina maswali yafuatayo:

  Je jeshi la polisi waliwaomba msaada JWTZ kusaidia kupambana na vikundi vya wahuni wachache wanaojiita waislam?

  Je nani ametoa maagizo ya JWTZ kujiingiza kwenye shughuli za kutuliza ghasia wakati kuna polisi wa kawaida na FFU ambao kutuliza ghasia ni kazi yao?

  Nani alikuwa akikaimu nafasi ya uraisi wakati akiwa ziarani Oman.

  Je ilikuwa ni fursa nzuri ya watu kuamua kutunishiana misuli kwamba nani mwamba kwa vifaa na vikosi- nikimaanisha mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange akaamua kumwambia kwa vitendo SAidi Mwema kwamba tulia dogo nikufundishe kazi?

  Kwa mawazo yangu kumetokea kosa kubwa la kiufundi kwenye kutoa maamuzi mazito yahusuyo usalama wa raia na mali zao na kwamba hakukuwa na vita bali vurugu ambazo zilihitaji polisi wadhibiti kwa uwezo wao bila JWTZ.

  Hivyo naweza kusema mkuu wa majeshi ameenda mbali mno kushauri au kuamua kuwaweka vijana wake barabarani kufanya doria.

  Nini mawazo yako?
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hawana kazi ya kufanya ndo maana..acha wazunguke majiani
   
 3. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Yaani tena wale waliomwagwa kitaa hawatoshi.

  Angewaongeza ili amalize upuuzi unaofanywa na wapumbavu wachache wanaodhani makanisani watu wanafundishwa kukojolea vitabu vyao. Makanisani watu wanafundishwa utakatifu, upendo na imani ya kweli ya kuwafikisha mbinguni. Wanaombewa magonjwa wanapona, wanafundishwa kuwapenda maadui zao na kujiepusha kulipiza kisasi kwani hiyo ni kazi ya MUNGU.

  Tofauti ni hii; Adui wa mkristo ni shetani wakati adui wa muislamu ni mkristo (inatokana na walichokifanya mbagala na zenji)
  Hivi mmeshajiukiza kwa nini waislamu wanaandama wakristo tu na wakati Tanzania na duniani kote kuna dini nyingi sana!? Sikupi jibu, tafakari, fanya utafiti then chukua hatua.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  waache vijana wapige jaramba la gwaride vs malawi..
   
 5. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wahenga wanasema BINADAMU NI HATARI kuliko mnyama yeyote hatari. Hatari hiyo hutokea baada ya binadamu kughadhibika na kuwa na uhuru wa kufanya chochote anachoweza kufanya. Ndiyo maana, katikati ya wanadamu zinaundwa sheria na kunakuwa na vyombo vinavyopewa dhamana ya kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na anayekiuka anachukuliwa hatua mwafaka. Mahali ambapo sheria hazifuatwi, inakuwa ni vurugu tupu na hali hiyo ni hatari kubwa tena sana kwa usalama wa raia wema.

  Mojawapo ya kazi kubwa ya serikali yoyote duniani ni kuongoza wananchi wake katika nyanja mbalimbali za kimaisha kwa kufuata sheria. Kazi nyingine ni kuhakikisha usalama wa wananchi na kuchukua hatua stahili kwa mtu, watu au kikundi chochote cha wananchi kinachotishia usalama wa wengine kwa kisingizio chochote kile. Serikali inayoshindwa kulinda usalama wa raia wake tena kushindwa kudhibiti uvunjifu wa sheria unaofanywa na mtu, watu au kikundi fulani cha watu, ni Serikali Dhaifu na hii ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa kwani kama nilivyosema mwanzo mwanadamu akiachwa aishi kwa uhuru unaovuka mipaka anaweza kusababisha hatari kubwa sana na ndicho kilichoanza kujitokeza hapa nchini.

  Hivi vikundi vinavyojiita vya wanaharakati wa kiislam vikiachwa viendelee kutamalaki, vitasababisha madhara makubwa kwa taifa hili la Tanzania ambalo kwa muda mrefu wananchi wake wameishi kwa amani na upendo. Natambua wapo waislam wengi tena wengi sana wanaowashangaa wenzao wanaofanya vurugu mitaani. Wapo wanaolaumu waziwazi kwamba watu hao wanaojiita wanaharakati wa kiislam wanautukana uislam na in fact wanauchafua uislam kwani uislam siyo dini ya vurugu. Ni dini ya amani.

  Ili kulinda usalama wa raia na mali zao, ningekuwa rais bila shaka ningetumia FULL FORCE siyo tu kuwadhibiti bali kutoa funzo kwao na kwa wale wanaofikiria kufanya fujo za aina hiyo kwamba linapokuja suala la usalama wa raia na mali zao, Serikali haina mchezo. Serikali lazima iwe tayari kulaumiwa na kikundi kidogo cha watu kwa faida ya wengi.

  Vurugu zinazoendelea Tanzania Bara na Zanzibar ni changamoto kubwa kwa marais wetu Kikwete na Shein. Wakiendelea kushughulikia masuala haya kimzahamzaha, amani ya nchi itatoweka na ikitoweka itachukua miaka mingi kuirejesha. Shime marais wetu washughulikieni ipasavyo hao wanaojiita wanaharakati wa uislam ili kurejesha utengamano wa watanzania uliokuwepo tangu enzi za marais wetu wa kwanza Mwl. Nyerere na Mzee Karume.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungi ibariki Afrika.
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona umetoa conclusion (maoni yako) kabla haujajibiwa maswali yako? Basi endelea kutumia hayo majibu yako, THREAD CLOSED
   
 7. KATUMBACHAKO

  KATUMBACHAKO JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  General Objective ya Jeshi lolote iwe polisi au JWTZ ni kulinda amani! Hata wewe ni jukumu lako kulinda amani! Hivyo hakuna kosa hapo
   
 8. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Udini umepandwa na 'rahisi' ambaye ni dhaifu na kutokana na udhaifu huo ameshindwa kudhibiti madhara yake. Hata mimi ningekuwa kiongozi wa nchi ningewashughulikia ipasavyo hao wanaojiita wanaharakati wa kiislam.
   
 9. P

  Paterne Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ultaka ww ndo ulinde aman ya nchi yetu nn wananch wana2lipa na ha2na kazi acha 2waonyeshe km kaz twaweza km mwataka rudien tena
   
 10. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete hawezi fanya hivo kwa sababu mtandao huo ndo ulimuingiza madarakani 2010.redio iman tusitarajiwe kufungwa, ataacha ichochee tu!
   
 11. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Angekuwa ni kikwete, kile kisanga cha Pemba 2001 kingeendelea muda mrefu sana na madhara yake bila shaka yangekubwa makubwa zaidi. Lakini Mzee Nkapa alikidhibiti kisawasawa kwa kufyeka waleta vurugu kiasi cha baadhi yao kukimbilia kwa ndugu zao Mombasa. Hiyo ndiyo FULL FORCE inayopaswa kuchukuliwa inapopambana na waleta fujo zisizo na mbele wala nyuma.
   
 12. u

  utantambua JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Humjui nani ni makamu wa rais?

  Mawazo yangu kama kweli JWTZ wamefanya patrol ni sawa na sahihi, na ni kwa manufaa yako, familia yako na nchi kwa ujumla.

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 13. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ulipouliza nani alikaimu uraisi wakati jk anashangaa kasri oman,? Jibu ni kwamba hakuwepo wa kukaimu kwa sababu hakukuwa na haja, nchi inajiendesha yenyewe AUTO-PILOT mode
   
 14. J

  John W. Mlacha Verified User

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wewe mwislam nini?
  thread akiifunga utachangia nini
   
 15. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Elewa kwamba amani hutafutwa kwa gharama yoyote ile kama kuna watu hawaelewi hilo waambie na swala amni siyo la kisiasa kama unavyofikiri wait and see kuendelea kucheka na nyani wakati una shamba la mahindi
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha combination ya BWM and Jemedari MAhita.
  Hata wakati wa Mrema walikuwa hawahemi!
  Sometimes I am wondering if we have a minister of Home Affairs!
   
 17. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  -Ni utaratibu wa kawaida tu ambao umetumika,lengo ikiwa ni kuwahakikishia raia wema amani na usalama.
  -Mji wa dar una raia wengi kuliko mji mwingine wowote nchini,hatuwezi kuzungumzia jeshi la wananchi kulinda mipaka wakati ndani si shwari.
  -Doria iliyokuwa inafanywa na JWTZ ni sehemu ya kuona kama kuna sehem vurugu zimekuwa kubwa kiasi polisi wanehitaji usaidizi nathalani kama kungekuwa na mapigano ya silaha.
  -Labda nikukumbushe kuwa wewe uliwaona Mgambo wa jiji,Polisi,FFU na JWTZ je unatambua kuwa kuna vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilikuwa vikifanya doria pasi ya wewe kujua?
  ;Basi hakuna matumizi mabaya ya vikosi hiki yaliyotumika sote tuna wajibu sawa kulinda amani ya nchi yetu hata kama mimi na wewe si maaskari.
   
 18. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mawazo yangu ni kwamba wewe mleta hoja pamoja na ukubwa wako hujui ni nani amiri jeshi mkuu!! pole sana! kama hao wanajeshi wako mitaani bila ridhaa yake basi huyo huyo amiri jeshi mkuu usiyemjua angekuwa ashatangaza uasi wa jeshi!

  Rais hata akiwa nje ya nchi bado anao uwezo wa kuwasliana na watendaji wake nchini na kuwapa maagizo licha ya kuwa yupo anaekuwepo kukaimu nafasi yake.

  Usiwe na dhana ya kuwa jeshi kazi yake ni kulinda mipaka tu! kama ingekuwa hivyo basi kambi zote za jeshi zingejengwa mipakani! adui wa taifa anaweza akawa ndani ya nchi vilevile, kikundi fulani kinaweza kuasi na kufanya mashambulizi ndani ya nchi kutokea msituni au popote pale ndani ya nchi halafu unataka jeshi lisubiri mipakani!

  Maandamano au ghasia vikizidi zinaweza sababisha rais kung'olewa madarakani kwa nguvu halafu unataka jeshi likae kimya!! TAFAKARI
   
 19. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waislamu watawapenda vipi wakristo(wasanii),wanawaombea walemavu hewa eti wapone. Nendeni mkawaponye walemavu wa Salender na ubungo. Wasanii tu kama ze Comedy.. Tokaga apa eti tunatafuta mbingu ipi upewe kwa usanii usanii tu.
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Watu hawakuelewa kwa nini wanajeshi walimwaga mitaani huu ni ujumbe kwa Chadema.
   
Loading...