JWTZ kuanzisha Benki:- Je ni benki ya JWTZ au Vingunge wa JWTZ?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,827
JESHI la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuanzisha benki yake itakayowasaidia wanajeshi kupata mikopo ya riba nafuu, kwa ajili ya kuendeleza kipato na mitaji ya biashara zao.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhamasisha shughuli za ujasiriamali ndani ya jeshi hilo Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Meja Jenerali Sylvester Rioba, alisema hivi sasa wana mtaji wa Sh1.7 bilioni na kwamba, wanahitaji Sh15 bilioni ili kutekeleza azma hiyo.

Jenerali Rioba alisema kutokana na hali hiyo, fedha hizo zitapatikana kwenye michango ya wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ngome (Ngome Saccos), kila mwanachama anatakiwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kufanikisha mpango
huo.

"Kuanzishwa kwa benki ya jeshi kutaweza kusaidia kuwapatia mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ujasiriamali, kutokana na hali hiyo tumepanga kupitisha michango ya wanachama," alisema. Aliendelea kuwa kutokana na hali hiyo, mkutano huo utawasaidia kuelimisha wanajeshi na watumishi wa umma, ili kujiunga kwenye Saccos hiyo ambayo itawakomboa.

Alitoa mfano wa nchi ya Rwanda ambayo wanajeshi wake wamepiga hatua ya maendeleo kutokana na kuanzishwa kwa benki hiyo na kwamba, imetoa mikopo kwa wanajeshi na watumishi wa umma, suala ambalo kwa Tanzania inawezekana.

Alisema mara nyingi wamekuwa wakipata mikopo kutoka Benki ya CRDB ili kukuza mitaji ya biashara, jambo ambalo mpaka sasa limewasaidia kupiga hatua. Hata hivyo, Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB, Sebastian Masaki, alisema wamekuwa wakifanya kazi na Ngome Saccos kwa miaka mingi, jambo ambalo limesaidia kuwaongeza idadi ya wanachama na mitaji yao.

Ngome Saccos ni miongoni mwa taasisi 500 ambazo tunafanya nazo kazi na kwamba, wamekuwa wakilipa mikopo yao kwa wakati, jambo ambalo linatufanya tuweze kushirikiana nao kwa ukaribu," alisema Masaki.
 
hawa wanafikiri sisi hatuna akili...... tunajua mnatafuta namna ya kuhalalisha hizo trilioni tatu.....lakini angalieni....dunia inaanguka taratibu.....marekani .....uingereza......hakuna kitakachosimama
 
Hivi kwa bibi Jeshi linataka kuingia kwenye biashara wakati wameshaproove failure kwenye MEremeta?
 
...............................Aliendelea kuwa kutokana na hali hiyo,mkutano huo utawasaidia kuelimisha
wanajeshi na watumishi wa umma, ili kujiunga kwenye Saccos hiyo ambayo itawakomboa...........

[SUP]Kichwa cha habari kilitakiwa kuwa ni Saccos na sio benki amabvyo ni vitu viwili tofauti. Jeshii au taasisi yeyote kuwa na SACCOS ni sawa. na sidhani kuwa ndio itaaanza Zipo. mammbo ya management hilo ni suala lingine.

Sasa sijui mleta mada kakosea kwa bahati mbaya au.....
[/SUP]
 
Mleta mada hajakosea walisema wana mpango wa kuanziaha benki ambayo itawapa wanajeshi mikopo yente riba nafuu ili waweze kuwa na maendeleo.
 
Wafute kauli yao mara moja. Hicho ni kiini macho wanafikiri nani yuko usingizini. Kwanza katika hii sayari tunayoishi mbali na Habitable zone.
Ukweli ni kwamba hakuna jeshi la nchi lililokuwa na benki yake, Si kwa mataifa tajiri na yenye uwezo na hata mataifa maskini yasiyo na uwezo.
Yapo mabenki zaidi ya ishirini nchini Tanzania na yanatoa mikopo kwa mtu wa aina yeyote ili mradi ufuate kanuni zao. Na kama wanajeshi
tayari wameshajidhamini kwa kuwa ni wafayakazi tena wa seikalini na kipato chao tosha kwa dhamana ya kulipa mkopo.
Wajitambue kama wanajeshi kazi yao ni ulinzi ususani wa mipaka yetu, na wasijihusishe na maswala ya kibiashara.
Huyo Shimbo wala asipate tabu yeye azisalimishe tu hizo pesa serikalini bila kufanya ujanja ujanja. Pesa zikirudi na kuwasaidia maskini
ambao hata mlo wa siku moja ni mashaka kwao na kuweza kupata matibabu kwa familia zao nafikiri watakusamehe kwa hilo. jaribu kufikiri
tena na usiangamize Taifa.
 
wazo zuri kila la heri
JESHI la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuanzisha benki yake itakayowasaidia wanajeshi kupata mikopo ya riba nafuu, kwa ajili ya kuendeleza kipato na mitaji ya biashara zao.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhamasisha shughuli za ujasiriamali ndani ya jeshi hilo Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Meja Jenerali Sylvester Rioba, alisema hivi sasa wana mtaji wa Sh1.7 bilioni na kwamba, wanahitaji Sh15 bilioni ili kutekeleza azma hiyo.

Jenerali Rioba alisema kutokana na hali hiyo, fedha hizo zitapatikana kwenye michango ya wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ngome (Ngome Saccos), kila mwanachama anatakiwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kufanikisha mpango
huo.

"Kuanzishwa kwa benki ya jeshi kutaweza kusaidia kuwapatia mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ujasiriamali, kutokana na hali hiyo tumepanga kupitisha michango ya wanachama," alisema. Aliendelea kuwa kutokana na hali hiyo, mkutano huo utawasaidia kuelimisha wanajeshi na watumishi wa umma, ili kujiunga kwenye Saccos hiyo ambayo itawakomboa.

Alitoa mfano wa nchi ya Rwanda ambayo wanajeshi wake wamepiga hatua ya maendeleo kutokana na kuanzishwa kwa benki hiyo na kwamba, imetoa mikopo kwa wanajeshi na watumishi wa umma, suala ambalo kwa Tanzania inawezekana.

Alisema mara nyingi wamekuwa wakipata mikopo kutoka Benki ya CRDB ili kukuza mitaji ya biashara, jambo ambalo mpaka sasa limewasaidia kupiga hatua. Hata hivyo, Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB, Sebastian Masaki, alisema wamekuwa wakifanya kazi na Ngome Saccos kwa miaka mingi, jambo ambalo limesaidia kuwaongeza idadi ya wanachama na mitaji yao.

Ngome Saccos ni miongoni mwa taasisi 500 ambazo tunafanya nazo kazi na kwamba, wamekuwa wakilipa mikopo yao kwa wakati, jambo ambalo linatufanya tuweze kushirikiana nao kwa ukaribu," alisema Masaki.
 
mmmmmhhhhhhh aisee ukikopa benki hiyo ikibidi ulipe kabla ya wakati mana hao watuuuuuuu baaalaaaaaaaaaaaaaa. wanaweza kukufata hata muda bado na utalipa. teh teh
 
pesa za gen shimbo na Rais wenu zinaanza kuzaa matuta like trilly!!
 
hivi ni jeshi la nchi gani duniani lenye kumiliki mabenki ya kibiashara?

Mkuu, mimi nilifikiri JWTZ kazi yao ni ya kijeshi na si biashara, lakini inaonekana hapo TZ JWTZ wanaweza hata kuwa na chama cha siasa. Sasa wana BENKI, khaaa.
 
natoa pongezi kwani ili ni agizo toka kwa wakuu ni namna gani fedha za ufisadi zirudi jeshini na wapewe wanajeshi kupitia benki hii

Attachments

  • PICT0022.JPG
    PICT0022.JPG
    318.3 KB · Views: 56
Mna jidangaya JWTZ haijawai kuwa na nidhamu ya fedha hata siku moja. Ulizeni serikali inalipa riba ya shilingi ngapi ile mikopo ya Tunakopesha na Mikopo wanayoingia wanajeshi.

Wanshidnwa kumanage vitu tehcnical kama magari ndio wataweza kumage fedha . kama ni kweli ni Maumivu kwa walipa kodi.

Wafanye Saccos inawatosha mambo ya benki ni kuingiza mkenge serikali kama dili za meremeta
 
Mkuu nakubaliana nawe sana.Binafsi nimeona hiyo NGOME BANK pale makongo na kujiuliza sana je huu utitiri wa miradi ndani ya JWTZ inafuata misingi ya jeshi hilo kweli ama ni namna ya kuhalallisha uchochoro wa matumizi mabovu ya raslimali za taifa na baadae wananchi wakihoji waambiwe ni mambo ya USALAMA WA TAIFA
Jeshini ndio taasisi inayoongoza kwa zabuni hewa na zenye bei maradufu ya soko na pia ndio taasisi inayoongoza kwa DEZO kuanzia Maji,umeme,nyumba mpaka mabuti ya deso.ukiachilia mbali manunuzi ya duty free na priviledge nyingine as if kama bila wao nchi haiendi au wao ndo most important cadre than others
Turudi nyuma pia taasisi za kukuza mitaji na BoT walitolee ufafanuzi hilo na ikiwezekana lipigwe zuio ili kuepuka migongano pindi matokeo mabaya yatakapotokea kwenye hiyo benki
 
Back
Top Bottom