JWTZ inalijua hili?

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,835
630
Wadau naomba kufaamishwa kisheria hii imekaaje,mara nyingi sana hapa lugalo ukipita asubuhi una kuta wanajeshi wakiwakamata waendesha pikipiki na bajaj kwa makosa aitha kwa kutokuvaa helmet au kupita kushoto aka kutanua.
Mara nyingi huwapa adhabu ya kufyeka nyasi kwenye campus yao.
Swali wajame kisheria inaruhusiwa?
Sio unyanyasaji kweli huu?

Nawakilisha!!!!
 
wamepungukiwa manpower
 
Kuna mamo mengine yanasikitisha mno.
Yote hii inatokana na raia kutojua haki zake za msingi. Basi!!
 
Kuna mamo mengine yanasikitisha mno.
Yote hii inatokana na raia kutojua haki zake za msingi. Basi!!

Wanajeshi wanatumia hujuma kwa mgongo wa ujinga wa Watanzania na uwajibikaji mbovu wa Serikali.
 
Ni ujinga wa "pedestrians": Madereva wengi (hata wa magari) hawafahamu "Sheria za Barabarani" - Leseni waliletewa! Na matokeo yake ndiyo hayo - Wale vijana huwa nawaona wakifanya zoezi la kufyeka kila nikibatika kupita njia hiyo! It is SAD lakini kila mara huwa najiuliza "Hii nchi inatawaliwa na NANI hasa?" Kwa maana kila mtu ni Polisi, Mahakama, na Magereza - It simply a BANANA Republic!
 
Wewe hujajua tu kuwa nchi hii inaongozwa kijeshi

1. Rais JK - Luteni Kanali
2. Katibu Mkuu CCM - Luteni Yusuf Makamba
3. Naibu Katibu Mkuu - Captain G. Mkuchika
4. Katibu Uenezi - Captain J. Chiligati
5. Meneja wa Kampeni - Kanali A. Kinana
6. Msemaji wa Usalama CCM - Luteni Generali A. Shimbo
 
Ni ujinga wa "pedestrians": Madereva wengi (hata wa magari) hawafahamu "Sheria za Barabarani" - Leseni waliletewa! Na matokeo yake ndiyo hayo - Wale vijana huwa nawaona wakifanya zoezi la kufyeka kila nikibatika kupita njia hiyo! It is SAD lakini kila mara huwa najiuliza "Hii nchi inatawaliwa na NANI hasa?" Kwa maana kila mtu ni Polisi, Mahakama, na Magereza - It simply a BANANA Republic!

Hopefully ni uozo wa system nzima kwani wangekuwa strict kusingekuwepo haya mfano kuletewa lesini,rushwa nk
 
Jeshi likishakosa kazi ya kufanya ndio linajiingiza kwenye mambo ya kipuuzi kama hayo. Tatizo hili jeshi letu linaajiri watu wasio na elimu na wasio wabunifu. Wangekuwa na watu competent wangekuwa innovative na kuunda hata silaha na ndege zao wenyewe. Nchi nyingi duniani ugunduzi wa maana huanzia Jeshini. Hawa wa kwetu wanasubiri kupewa tender za ku-supply uniform na maharagwe jeshini matokeo yake ndio hayo.
 
Enoe la jeshi ni eneo la ukakamavu, raia wote mnapopita lazima muonyeshe kwa mfano utii wa sheria na kanuni za nchi hii hata kama kwa kuigiza. Sasa ukitanua Lugalo na wajeda wapo ulitaka wakuchekee wakati watu wamekula viapo vya utii?

Tii sheria na usipende kulalamika kijinga. Enzi zetu hata kuangalia mpira Air wing ukonga hakuna kuporomosha matusi, walevi wote walikuwa wanatuliza mpira ikiwa mpira unapigwa Airwing, hata Boom na Ashanti ilikuwa inapelekwa huko kudhibiti fujo. Hakuna adhabu za kupelekwa rumande, adhabu ndogo na kuchekesha za kijeshi.

Sio kila kitu cha kulamu vingine mjilaumu wenyewe kwanza kabla ya kulaumu serikali, kwanza hiyo rugalo enzi za mwalimu raia alikuwa anakatiza? barabara ya bagamoyo ilikuwepo. ugeni wenu mjini ndio umekuwa kero zaidi manake mnakuja na sheria zenu na kutaka kuonewa huruma bila sababu za msingi.
 
Wakuu wakati mwingine mnakosea sana, unajua hii nchi ina sheria nyingi tu zingine ziko sawa na za maana zingine hovyo na zimepitwa na wakati. lakini kwa mfano kutanua barabarani ni kosa na watu wanajua na police wanaona wanakaa kimya sasa pale jeshini ukidakwa unafanya kazi kama zile ni sawa ambazo hata kisheria zinaitwa ( community services) ile adhabu ni nzuri kuliko kupeleka mtu mahakamani akamalize mda na karatasi.
 
hivi Mwamnyange analijua hili mbona ni aibu tupu jeshi la wananchi kufanya kazi za polisi ? huu ni ukiukaji wa utawala bora na kama wamewakamata wapelekwe kwenye sheria na siyo kuwapa kufyeka naona kweli wamepungukiwa manpower.
 
Wakuu wakati mwingine mnakosea sana, unajua hii nchi ina sheria nyingi tu zingine ziko sawa na za maana zingine hovyo na zimepitwa na wakati. lakini kwa mfano kutanua barabarani ni kosa na watu wanajua na police wanaona wanakaa kimya sasa pale jeshini ukidakwa unafanya kazi kama zile ni sawa ambazo hata kisheria zinaitwa ( community services) ile adhabu ni nzuri kuliko kupeleka mtu mahakamani akamalize mda na karatasi.

Wadau Somoche na Songambele sijui kama mnafahamu mnachozungumza. Kwanza majeshi katika karne hii sio vyombo vya kutumia mabavu katika kukabiliana na changamoto. Sasa hivi majeshi duniani kote yanajikita katika kutumia high tech. Pili ambacho wadau wamesema, hata kama mtu kavunja sheria( eg katanua), askari inabidi wakimkamata wamkabidhi kwa polisi kwani ndio wenye majukumu hayo. Wao kutoa adhabu ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
 
Wadau naomba kufaamishwa kisheria hii imekaaje,mara nyingi sana hapa lugalo ukipita asubuhi una kuta wanajeshi wakiwakamata waendesha pikipiki na bajaj kwa makosa aitha kwa kutokuvaa helmet au kupita kushoto aka kutanua.
Mara nyingi huwapa adhabu ya kufyeka nyasi kwenye campus yao.
Swali wajame kisheria inaruhusiwa?
Sio unyanyasaji kweli huu?

Nawakilisha!!!!
Hao jamaa wananiudhi kupindukia. Inaonekana wamekosa cha kufanya. Nina mpango wa kuuza mkweche wangu ninunee pikipiki halafu niwatanulie waliko wanikamate ili nilianzishe. Yaanai wanaudhi sana uatadhani si watanzania
 
Mimi naona bora wafyeke hizo nyasi kwa kuvunja sheria za barabarani kuliko wapelekwe polisi/mahakamani wotoe rushwa ya elfu mbili halafu waachiwe waendelee kuvunya sheria tena wangeongezewa mbali ya kufyeka nyasi wangesafisha na mitaro ya maji machafu na vyoo.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom