JWTZ Haya mazoezi yenu ya kurusha rusha ndege mngeyafanyia porini sio mijini

luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,849
1,938
Tangu kumekucha ni milio mikali ya ndege zinazofanyiwa mazoezi na Jeshi.

Hivi Hawatambui kuna wagonjwa mahospital na majumbani?

Imeshindikana vip kufanyia mazoezi yenu huko porini? Yani ukikaa kidogo unasikia sauti kali mno yani mie niliye mzima zinanipa shida hivi sasa najiuliza vipi kwa mgonjwa wa presha na wagonjwa wengine?

Hata kama ni kupata sifa, hamuoni pia sio salama kwa raia pia maana katika mazoezi kuna risk pia ya vyombo vyenu kufeli, itakuwaje ikitokea la kutoea mkaangusha hiyo midege mijini humu, ni vifo kiasi gani mtatutangazia?
 
Kuna kikosi cha Anga,Ardhini na Majini....sasa sijui unamaanisha nini? Acha woga huo...wapi huko kuna waoga hivi.
 
Wanachukulia poa ila kiukweli hizi kelele ni kero kubwa sana..mm binafsi hapa siko vizuri sababu ya sauti kali ya hizo ndege,sasa sijui walioko hapo Bugando hospital wenye tatizo la presha wana hali gani..wangeweza kuzielekeza ziwani huko katikati wakafanya mazoezi wakimaliza warudi ila hii misele wanayopiga humu mjini watakuja kuua watu kwa khofu...


Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Wangeenda mbali na mji ingependenza.hata hapa Dar huwa wanafanya hivyo.Sio powa wangeenda ziwani huko wawe wanatest kuvikwepa na kuvizunguka visiwa vidogo kwa spidi ya 25000kph
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom