JW ‘yawapongeza’ askari waliotoa kipigo kwa raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JW ‘yawapongeza’ askari waliotoa kipigo kwa raia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mlaizer, Feb 28, 2011.

 1. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanaJF
  Naomba tuchekeche hili pengine mimi ndio sijui sheria za TZ(source:mwananchi)
  Sunday, 27 February 2011 20:49 0diggsdigg

  Hussein Issa
  BAADA ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongolamboto, kuwapiga raia kwa madai ya kupigwa kwa mwenzao, jeshi hilo limesema hawana makosa kwa sababu wametekeleza mafunzo waliyofundishwa.

  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha JWTZ, Luteni Kanali Kapambala Mgawe, alisema wanajeshi wanatakiwa kuheshimika popote pale sio watu wa kuchokozwa.

  “Hawa vijana hawana kosa kabisa kwa sababu walichokifanya wao ni kutekeleza yale mafunzo waliyoyapata kule jeshini, kwani walijifunza kuwa na mshikamano mzuri, “ alisema Kanali Mgawe.

  Kanali Mgawe alisema kutokana na ushirikiano na mshikamano waliojifunza wakiwa jeshini, askari hao ilibidi kuvitumia kumsaidia mwenzao aliyepigwa Gongolamboto, kwani wangeacha kufanya hivyo wangekuwa wamekosea.

  “Unajua kijana kule jeshini kuna kitu kinaitwa ‘esprit de corps “ ndio maana wakafanya hivyo kijana sawa!” alisisitiza Kanali Mgawe.

  Pia, alisema mshikamano huo unawaelekeza wanajeshi kusaidiana wanapozidiwa vitani kwa kuishiwa silaha au kupoteza, ndio maana hata ukiingia jeshini leo utakuta heshima hiyo inaendelea.

  “Unaposimama katika gwaride kisha mkuu akafika pale kukagua viatu na kukuta wewe umepiga rangi viatu vyako na mwenzako hajapiga, utaulizwa uliyepiga kwanini hujamkumbusha mwenzako” alisema.

  Inasemekana watu zaidi ya 30 ambao walikuwa wamevalia sare za jeshi, waliingia mtaani na kupiga raia yeyote waliyekutana naye saa 6:00 usiku.

  Kwa mujibu wa raia hao, watu waliumia na ilibidi wengine wakimbizwe hospitalini, huku baadhi yao wakiugulia nyumbani.

  Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya milipuko ya makombora illiyoua watu kadhaa na kuacha mamia wakiwa hawana makazi.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  haya sasa! kumbe wanajeshi wetu wanafundishwa kupiga raia!! no matter wanaona kulipua mabomu ni ghara wacha yajilipukie waue!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,708
  Trophy Points: 280
  Nimetegua kile kitendawili cha kwanini pamoja na ukubwa wa milipuko ya gongo la mboto ambayo ni zaidi ya mara kumi ya ile ya mbagala lakini hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyekufa licha ya maghala na mabweni ya askari kusambaratishwa na mabomu. Kumbe tuna jeshi ambalo ni hostile kwa raia,hii ni roho ambayo imeanzia kwa wakubwa kabisa kuanzia Rais na wengine hawana huruma na watu, wao wanajali maslahi yao tu. Mimi nimefurahi kwa majibu ya Luteni Kanali Mgawe, ili watu wajue kuwa tuna Jeshi katili, Polisi katili, mahakama zilizokithiri kwa rushwa,Bunge linaloongozwa na spika dikteta, Tume ya uchaguzi inayochakachua kura,Chama tawala chenye mrengo wa kifisadi,na Rais anayetawala kishikaji.Dawa ni moja tuuuu, PEOPLESSSSSSSSSSSSS POWERRRRRRRR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ngoja wakutane na nguvu ya Umma tuone kama watatoa kichapo au watapewa kichapo
   
 5. s

  sawabho JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Naona vyonbo vyote vya dola vipo kwa maslahi yao na sio kwa ajili yamwananchi wa kwaida. Lakini waachceni tu, maana tunaishi nao mtaani, hata kama watajengewa makambi na maduka ya bei rahisi, ipo siku watastaafu na kurudi huku.
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmhhh sasa hii kali zaidi, inamaana kwenye mafunzo yao wanafundishwa kupiga raia.... :A S 13:
   
 7. garikicah

  garikicah Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  wakati mwingine raia wakiachwa kila mtu afanye anavyotaka nchi haiendi, watu wanapenda ku test zali na respond ikija weak then ina kuwa mazoea.
   
 8. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii siyo mara ya kwanza kwa wanajeshi wa JWTZ kupiga raia,ktk miji/vijiji vilivyo karibu na kambi za jeshi la JWTZ haya matukio yamekuwa ya kawaida sana.Mfano 1996 kule monduli ktk kambi ya jeshi ya SOFA kulikuwa na mwanajeshi alikuwa mahusiano wa kimapenzi msichana wa mji mdogo wa dukabovu karibu na kambi hiyo,kumbe kuna raia wa mji ule ambaye naye ana mahusiano na msichano huyohuyo.Wanaume wote waligongana maeneo hali iliyopelekea ugomvi kati yao,wanajeshi kusikia hilo ikabidi wajikusanye kupiga raia na kuchoma nyumba zote na biashara zilizo karibu na barabara ktk mji huo.Mfano mwingine ni 2001,mwanajeshi mmoja aliibiwa simu ktk mtaa wa sanawari Arusha mjini;wanajeshi walijikusanya wakaanza kupiga raia.
  MY TAKE:lazima wananchi tufuatilia kama kweli wanajeshi wanafundishwa hivyo basi tuamke kudai wabadili utaratibu wao kwani huo ni ugandamizaji
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wanaolalamika hawajaenda JKT.
  Enzi zetu ukichokozwa na raia mtaa huo haupitiki
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  Mafisadi tu nao, si wanamiliki mgodi
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mwanajeshi wa ISRAEL AKIPATIKANA NA HATIA YA KUMPIGA RAIA ANAPEWA ADHABU KALI SANA LAKINI HUKU KWETU WANASIFIWA.
   
 12. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hakuna mtu aliye juu ya sheria kuanzia rais, wabunge, askari wa majeshi yote na raia wote waliosalia. Na hakuna sheria inayolipa uhuru kundi moja kuvunja sheria.. Sheria zote zinatubana sawa.... Msemamji wa jeshi ajiuzulu kwa kutetea uvunjwaji wa sheria..kama raia alimpiga askari basi wakamatwe wapelekwe mbele ya sheria na wakukumie kwa mujibu wa sheria...alaaaa tunataka kuip[eleka nchi wapi ebooooooooooooo!!!! Shame!!!!
   
 13. P

  PatriotMzalendo Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo linabaki kuwa kosa tu. Watu kupigwa enzi hizo na kutodai haki yao,hakufanyi kupigwa kwao kukawa halali.Hiyo ni kinyume cha haki
  . Jeshi lolote lenye nidhamu hufunzwa kuwalinda raia wake na si kuwashambulia raia hao. As for chanzo cha kupigana huko, mara zote Wanajeshi ndiyo wachokozi kama kuwataka kimapenzi wake wa raia kwa ubabe nk. It goes without saying kwamba hakuna raia mwenye guts za kuanzisha chokochoko na askari but when it comes to fighting for a just cause on the part of a civilian, askari anapozidiwa nguvu na kupigwa, anaenda kukusanya wenzake wanaoshambulia kila mtu wa eneo hilo wakati ugomvi ulikuwa wa askari mmoja na raia mmoja tu! Huyo Mgawe wa JWTZ ni bugabuga wa kupitiliza kwa kutoa kauli rasmi ya JWTZ iliyo ya kipumbavu kuzidi upumbavu wenyewe!
   
 14. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kuwasifia wanajeshi kwa kulipiza kisasi hakuna tofauti na kumsifu muuaji aliyeamua kulipa kisasi baada ya mtu wake wa karibu kuuawa..

  Kama Jeshi letu lingekuwa linaendeshwa na waungwana huyo L. Kanali angewajibishwa kwa maneno yake hayo.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Waliopigwa na wajeshi hao ni watoto wa masikini tu ndio huyo luteni akasema mbovu bila ya aibu ,hivi huko jeshini hakuna military police ??? Kama kuna mjeshi aliepigwa na raia kwanini hakuenda kushitaki ? na sheria kufuata mkondo wake ?Mjeshi kupigwa uraiani alifuata nini huko na uniform za jeshi ? Nijuavyo mjeshi huwa haruhusiwi kuzurura na uniform bila ya sababu za msingi.

  Kama nilivyosema hao waliopigwa ni masikini za Mungu na hawana wa kuwatetea zaidi ya uchunguzi unaendelea ,kwa nini nikasema hivyo ,kuna kisa kilitokea Kiembe Samaki kwa wale wanaoifahamu Zanzibar ,wataelewa kuwa sehemu kubwa ya karibu na airpot ni nyumba za vigogo wa kila fani ,wa CCM polisi na hata majeshi ,kuna vigogo wanaishi hapo hapo kandokando ya Airport ,sasa kuna mjeshi alipanda daladala na hakutoa nauli ,konda na dereva wake wakamwekea bifu mteja wao wa kijeshi na kumkurupusha ,pembeni kulikuwa na vijana wamekaa wakipeana za siku,walichokifanya hao vijana ni kushangilia vurugu hizo ambazo zilimtia aibu mjeshi,mjeshi akajiondokea kuelekea kambini,kambi ambayo si mbali,muda si mrefu akarudi na kundi kubwa la wajeshi ambao ndio kwanza wapo kambini kwa mwezi ni wajeshi wapya(Trainees) wakawakuta wale vijana wapo palepale ,hapo wajesho hao hawakuuliza walivua mikanda na kutembeza mkong'oto wa aina yake ,ikawa pata shika nguo kuchanika.

  Msalie mtume kumbe wale ni watoto wa vigogo ambao huwa wanakutana hapo kusikiliza milio ya ndege zituazo na zirukazo huku wakipeana tumbaku(habari za siku za kizushi au kweli) ,habari zikafika kwa vigogo na kambi ikashukiwa na wakuu wa kijeshi kutoka makao makuu mjini ,wale waliohusika wote wakatakiwa wajitokeze kabla ya kutajwa(kwani baadhi yao wakijulikana na vijana hao akiwemo yule aliekataa kutoa nauli) ,idadi yao ilifikia hamsini kwa ufupi wote walifutwa uajiri na kuambiwa wafunge virago kila mmoja kwao ,hawana kazi. Ndio nikasema waliopigwa hapo Gongo lamboto ni masikini za Mungu na Luteni ndio akapata ubavu wa kutoa mbovu kwenye magazeti au vyombo vya habari.
   
 16. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  hakuna jeshi la wananchi ila kuna jeshi la CCM, na hata hayo mabom wamelipua makusudi ili watu wasahau maswal;a muhimu dhidi ya serkali hongera chadema kwa kutangazaaandamano nchi nzima lazima tuwatoe tu kwa nguvu ya umma
   
Loading...