Jux apewe ajira ya kuwa mwalimu chuoni (lecturer), anafaa kuwa balozi wa kuwapa moyo vijana wasiache elimu kwajili ya usanii

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
1664715025384.png


Asisubiriwe mpaka apoe, muda sahihi ni huu wakati bado anashika chati kwenye muziki.

Jux ni msanii alieweza kufanya muziki na kusoma kwa mpigo, anastahili kupewa ajira ya kipendeleo kabisa, ilibidi na mshahara wa ziada ili awe balozi kwa vijana wengi nao watamani kupita njia aliyopitia Jux.

Serikali iliangalie hili jambo maana kuna vijana mashuleni wanachizika na usanii na kukatisha ndoto zao za kielimu. Wanafunzi wengi wakianza kupata umaarufu kidogo tu hata kwa level ya mtaani wanapuuza elimu na kuweka umakini kwenye muziki.

hii italeta mwamko hata kwa baadhi ya wasanii watumie mapato wanayopata kutoka usanii, wayatumie kujiendeleza kielimu kama wana sifa za kujiendeleza kielim. Vyuo vingi kusomea diploma unahitaji D 2 tu na kuna wasanii kibao wanazo.
 
Tuwe serious.

hawa wadogo zetu wengi wanatuiga sisi wakubwa

dogo akimuona msanii hana elimu nae anahamasika apuuze shule, huu mzizi inabidi ukatwe kwa wadogo zetu wakianza kumuona kaka yao kafanikiwa kimziki na ni mwalimu chuoni wataanza kujenga mindset positive.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom