abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 0
[h=1]Maoni ya leo 05/12[/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 05/12/2012 // Habari // 1 Comment
MAMBO YA LEO: Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa (ambaye aliwahi kuwa Waziri miaka ya 90), Mohamed Ramia, alijitokeza kutoa maoni yake Dimani. Alisema yeye anaunga mkono Muungano wa Serikali Mbili lakini akataka marekebisho makubwa. Kwanza, alisema mambo ya Muungano yapunguzwe na miongoni mwa mambo aliyotaka yaondolewe kwenye Muungano ni mafuta na gesi asilia, bandari, forodha, ushuru na kodi ya mapato. Akasema ingawa mambo ya nje ni suala la muungano lakini mahusiano ya kimataifa si suala la muungano na yalipenyezwa kinyemela. Akataka yaondolewe na kila nchi isimamie yenyewe mahusiano ya kimataifa. Akasema anataka pia Rais wa Zanzibar awe na hadhi inayotambulika na akasema hata katika Uamiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ni lazima iwekwe wazi kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa Naibu Amiri Jeshi Mkuu na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano asiweze kuchukua maamuzi yoyote kuhusiana na masuala ya ulinzi na usalama bila ya kwanza kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar. Alikuwa nayo mengine, akaambiwa kutokana na muda kuwa mchache ajaze fomu na ayaandike.
Katika utoaji maoni mchana huko Chukwani, Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Thuwaiba Kisasi, yeye alisema ni muumini wa Muungano lakini hakusema wa muundo gani. Baada ya hapo, akaorodhesha kero tele za Muungano ambazo haridhiki nazo. Na yeye akamalizia kuwa anataka mafuta na gesi asilia, forodha, ushuru na kodi ya mapato, bandari, elimu ya juu na takwimu na leseni za viwanda yaondolewe kwenye Muungano.
Najiuliza kwa orodha hii ya wana-CCM wanaokwenda kinyume na maelekezo ya Chama tena wakiwa viongozi wa juu wa Chama na Seriklai, nao watafukuzwa? Unafanya mchezo na uzalendo wa Zanzibar wewe?
[h=4]Related Posts[/h][h=3]ELIMU KWA WASIOJUA NINI MUUNGANO WA MKATABA[/h]
[h=3]Tume Katiba yabanwa Zbar[/h]
[h=3]Mawakili wa Uamsho wakwama kufika mahakamani[/h]
[h=3]JE, DK SHEIN UMEBAKIA PEKE YAKO??[/h]
[h=3]zanzibar chini ya muungano wa mkatabaa[/h]