Juu ya utumishi wangu kwenye "Taasisi" ile ninapohakikisha treni la EL linatema abiria wake

KUna uwezekano mkubwa hujui asili hasa ya ukweli ni nini na kwanini ukweli uko juu ya vitu hivi vingine. Hutakuwa watu wako tayari kufa kusimamia busara bali utawakuta wengi ambao wamesalimisha maisha yao kwa ajili ya kile ambacho dhamira zao na ufahamu wao kimewashawishi kuwa ni ukweli.

SIO KILA AFAYE KWA KUSIMAMIA UKWELI HUTIBITISHA KWELI YAKE... We know people waliokufa wakiamini waaminicho only later ukweli wa kweli ukaja kujitokeza

ladba ujue kitu kingine, sio kila unachoweza kusacrifice basi ndio kiwe kweli zaidi, vingine ni sadaka au busara...

Mtu mwenye busara hatangulizi kifo, na kama kinatokea ni kwa ajili ya faida ya muda mrefu kwa wote hata afaye...

Kweli yako ndugu yangu ina walakini... Na si ajabu utajua hilo siku moja

On another note: Kitu ninachokukubalia (kama tukitaka kusimamia ukweli) ni kwamba wote wanaotaka kututawala mwaka huu ni walaghai, hakuna hata mmoja asemaye ukweli, sasa je tuwatose wote na tujitawale?? tumwache huyo msanii mkuu aongezewe muda? au tupige bora liende na tulipe ultimate sacrifice itakayorudisha busara, ukweli na ukomavu

I think you are stretching too far kwasababu ya personal ego na security hadi unaharibu zaidi mkuu, extremism na ukweli vyaweza kuishi pamoja, lakini kweli yake itakua biased tu
 
Kama huwezi kujifahamu, utafahamu vipi hata mazingira yaliyokuzunguka?

Mimi nadhani unasumbuliwa na inferiority complex ndiyo maana unadhani amejigamba, amejikweza na kujitapa.

Kwangu mimi naona na kufikiria aliyoyaandika ni mambo ya kawaida sana katika dunia iliyojengwa kwa nguzo ya ukweli.

Wale wale.Mimi sijamtaja mtu.Uwe unasoma na kuelewa.Kama huelewi uliza.
 
Hivi miye kuwa Marekani kinawakera saaaaaana? kwani hapo hakuna Watanzania wanaozungumzia mambo ya Marekani tena kwa undani tu wengine hata kukanyaga hawajakanyaga? Au hujawaona watu wanaojadili timu za Mpira za UEFA au Premier League utadhani wamewahi kukaa Ulaya na kufanya kazi kwenye hizo klabu? Huwa mnawakataza kuzungumzia mambo ambayo yako mbali na nchi waliyopo? Hii ni mojawapo ya hoja za kijinga kabisa zinazotolewa na watu ambao wanaamini wamewahi kupita karibu na shule.

Nadhani unajua kuwa hao wanaozungumzia mambo ya nchi nyingine au timu za UEFA mara zote wanapuuzwa... Alkadhalika thawabu yako ni kupuuzwa na watanzania...

Kwa akili yako hivi unafikiri kuna mtu anakereka wewe kuwa Marekani...???! Hoja hapa ni kwanini upo nje ya nchi lakini unawarubuni watanzania ambao wanapigika kila siku kwa ugumu wa maisha ulosababishwa na "wakoloni weusi" wa ccm...
Wananchi wa Tanzania wanataka mabadiliko... Haijalishi yanakuja kwa stahili gani lakini kwa pamoja wapo tayari kufanikisha mabadiliko...!!

Wewe kama unaona hizi harakati na hii hoja ni ujinga basi "Fanya yako ukiwa huko kwenu na sisi tuaache tufanye yetu tukiwa huku"...!

Matatizo ya ndani ya Chelsea anayajua mmiliki, meneja, viongozi, wachezaji.... Sidhani kama mashabiki na "wasemaji" wa Chelsea waliopo Tanzania wana ufahamu sahihi wa kinachoendelea ndani ya Chelsea...
Ni wa kupuuzwa tu..!!
 
Ukiona mtu anatenga masaa kuandika article ndefu namna hii tambua limemkuta na huenda kapoteza riziki yake kupitia mtu fulani aliyekuwa akimtegemea na sasa anashinda njaa na wanawe.

so sad tuache kutumika tujitafutie wenyewe.
 
Hii taasisi ya 'ukweli' ni ya aina yake na inavutia sana, ila haiwezi kutumika katika siasa hatuwezi kuwaweka wanasiasa kwenye taasisi ya ukweli, hasa siasa za Tanzania, kwa sababu wanasiasa wana tenda kazi kwa makundi, wanafunikiana makosa kwa makundi, wanafanya madili kwa makundi, wanapigania vyeo na maslahi binafsi kwa makundi, na wanapigania ukweli kwa makundi nk. Kwenye mambo ya siasa huwezi huwezi kujua mkweli ni nani na mwongo ni nani,kwenye siasa usemi wa umdhaniaye ndie kumbe siye na umdhaniaye siye kumbe ndiye una maana kubwa sana.

Hakuna mwanasiasa mkweli hasa tanzania, hakuna mwanasiasa msafi kwa sababu chochote wanachofanya wanafanya kwa makundi, na kwenye kundi hawezi kukosekana mchafu hiyo ni hali halisi ya kibinaadamu, na akiwepo mchafu mmoja tu basi wote walio kwenye hilo kundi wanahusika na huo uchafu. Hata akiwepo mwanasiasa mkweli hatuta mchagua kwa sababu atapanda jukwaani na kuongea ukweli ambao hauvutii masikioni mwetu, hakuna mwanasiasa atakayepanda jukwaani kwa mfano na kusema nchi yetu ina daiwa pesa nyingi na nchi zilizoendelea na bajeti yetu inategemea misaada kwa kiasi kikubwa naahidi hiki na hiki kadri ya vipaumbele vyenu wapiga kura ila ukweli ni kwamba mwisho wa siku utekelezaji wa hizi ahadi utategemea na mikataba, masharti na vigezo vinavyokuja kwenye makubaliano na misaada ya wazungu.

Watanzania tuna kazi moja tu kwanza, nayo ni kuhakikisha tunabadili fikra za wanasiasa, hiyo ndio hatua ya kwanza, wanasiasa lazima wafahamu kwamba siasa ni ajira na sisi wananchi ndio waajiri wao, hatua ya kwanza ni kukitoa madarakani chama tawala ambacho kimeshika nchi kwa nusu karne bila kutuwezesha watanzania kupata huduma za msingi zilizo haki ya binadamu asiyeishi jangwani , lakini kukitoa tu hiki chama madarakani haitoshi tuna takiwa kubadili katiba ya nchi ili tuweze kupambana na rushwa kati ya wanasiasa na wafanya biashara wakubwa, kupunguza madaraka ya raisi , kuwa na tume huru ya uchaguzi. Kusimamia malia sili na pato la taifa etc, inabidi tuangalie nani anatupa dira inayoeleweka inayozingatia Zaidi matakwa yetu sisi wananchi, sio katiba inasema hivi, ilani inasema hivi, mkukuta unasema vile, wawekezaji na tuliowakopa wanasema kingine na wananchi wanataka vingine jambo ambalo halijatusaidia kwa miaka Zaidi ya hamsini.

Inasikitisha jinsi tuna vyojiweka kundi moja na wanasiasa, wanasiasa hawakutakiwa na hawatakiwi hata kuwepo kwenye taasisi ya ukweli, kwa sababu siasa hazina uwiano na ukweli. Magufuri , Lowasa, Mama Mghwira wote wanachagua maneno yao ili kutafuta kura ila tunachotakiwa wananchi ni kuangalia nini tunataka na nani kwa kiasi kikubwa yupo upande wetu, then tu msapoti kwa ballot ifikapo October 25, huu utaratibu tukiurudia baada ya miaka mitano/ kumi wanasiasa watafahamu kwamba alaa kumbe ukitaka ajira ya siasa lazima usikilize wananchi wanataka nini ...hapo ndio makundi ya utapeli wa kisiasa yataanza kupungua na hapo ndio tutakapoanza kupiga hatua za maendeleo. Mambo yaku tizama historia ya mgombea mmoja mmoja na kuwaweka wanasiasa kwenye taasisi ya ukweli hayatatufikisha popote.
 
Hivi miye kuwa Marekani kinawakera saaaaaana? kwani hapo hakuna Watanzania wanaozungumzia mambo ya Marekani tena kwa undani tu wengine hata kukanyaga hawajakanyaga? Au hujawaona watu wanaojadili timu za Mpira za UEFA au Premier League utadhani wamewahi kukaa Ulaya na kufanya kazi kwenye hizo klabu? Huwa mnawakataza kuzungumzia mambo ambayo yako mbali na nchi waliyopo? Hii ni mojawapo ya hoja za kijinga kabisa zinazotolewa na watu ambao wanaamini wamewahi kupita karibu na shule.

Umepanic braza , kajipumzishe kidogo kuandika.
 
Hii taasisi ya 'ukweli' ni ya aina yake na inavutia sana, ila haiwezi kutumika katika siasa hatuwezi kuwaweka wanasiasa kwenye taasisi ya ukweli, hasa siasa za Tanzania, kwa sababu wanasiasa wana tenda kazi kwa makundi, wanafunikiana makosa kwa makundi, wanafanya madili kwa makundi, wanapigania vyeo na maslahi binafsi kwa makundi, na wanapigania ukweli kwa makundi nk. Kwenye mambo ya siasa huwezi huwezi kujua mkweli ni nani na mwongo ni nani,kwenye siasa usemi wa umdhaniaye ndie kumbe siye na umdhaniaye siye kumbe ndiye una maana kubwa sana.

Hakuna mwanasiasa mkweli hasa tanzania, hakuna mwanasiasa msafi kwa sababu chochote wanachofanya wanafanya kwa makundi, na kwenye kundi hawezi kukosekana mchafu hiyo ni hali halisi ya kibinaadamu, na akiwepo mchafu mmoja tu basi wote walio kwenye hilo kundi wanahusika na huo uchafu. Hata akiwepo mwanasiasa mkweli hatuta mchagua kwa sababu atapanda jukwaani na kuongea ukweli ambao hauvutii masikioni mwetu, hakuna mwanasiasa atakayepanda jukwaani kwa mfano na kusema nchi yetu ina daiwa pesa nyingi na nchi zilizoendelea na bajeti yetu inategemea misaada kwa kiasi kikubwa naahidi hiki na hiki kadri ya vipaumbele vyenu wapiga kura ila ukweli ni kwamba mwisho wa siku utekelezaji wa hizi ahadi utategemea na mikataba, masharti na vigezo vinavyokuja kwenye makubaliano na misaada ya wazungu.

Watanzania tuna kazi moja tu kwanza, nayo ni kuhakikisha tunabadili fikra za wanasiasa, hiyo ndio hatua ya kwanza, wanasiasa lazima wafahamu kwamba siasa ni ajira na sisi wananchi ndio waajiri wao, hatua ya kwanza ni kukitoa madarakani chama tawala ambacho kimeshika nchi kwa nusu karne bila kutuwezesha watanzania kupata huduma za msingi zilizo haki ya binadamu asiyeishi jangwani , lakini kukitoa tu hiki chama madarakani haitoshi tuna takiwa kubadili katiba ya nchi ili tuweze kupambana na rushwa kati ya wanasiasa na wafanya biashara wakubwa, kupunguza madaraka ya raisi , kuwa na tume huru ya uchaguzi. Kusimamia malia sili na pato la taifa etc, inabidi tuangalie nani anatupa dira inayoeleweka inayozingatia Zaidi matakwa yetu sisi wananchi, sio katiba inasema hivi, ilani inasema hivi, mkukuta unasema vile, wawekezaji na tuliowakopa wanasema kingine na wananchi wanataka vingine jambo ambalo halijatusaidia kwa miaka Zaidi ya hamsini.

Inasikitisha jinsi tuna vyojiweka kundi moja na wanasiasa, wanasiasa hawakutakiwa na hawatakiwi hata kuwepo kwenye taasisi ya ukweli, kwa sababu siasa hazina uwiano na ukweli. Magufuri , Lowasa, Mama Mghwira wote wanachagua maneno yao ili kutafuta kura ila tunachotakiwa wananchi ni kuangalia nini tunataka na nani kwa kiasi kikubwa yupo upande wetu, then tu msapoti kwa ballot ifikapo October 25, huu utaratibu tukiurudia baada ya miaka mitano/ kumi wanasiasa watafahamu kwamba alaa kumbe ukitaka ajira ya siasa lazima usikilize wananchi wanataka nini ...hapo ndio makundi ya utapeli wa kisiasa yataanza kupungua na hapo ndio tutakapoanza kupiga hatua za maendeleo. Mambo yaku tizama historia ya mgombea mmoja mmoja na kuwaweka wanasiasa kwenye taasisi ya ukweli hayatatufikisha popote.

Vatican ya Roma haiwezi kuwaamulia watanzania nani awe kiongozi wao nani asiwe eti kwa kisingizio cha "Taasisi ya Ukweli".
Wana ukweli gani wale...???
 
kwa sababu una chuki na lowasa basi tuendelee na hili dude tumekaa nalo kwa miaka 50 na limeshindwa kubadilika? Mwanankikjiji sasa anaongozwa na wivu wala sio ueledi tena!
 
nilijiandikisha baada ya kupata matumaini pale lowasa alipohamia upinzani. Sasa ni uvivu wa kufikiri, kufikiria kuwa unaweza kunibadilisha kura yangu iende ccm. Yaani aliyenihamasisha kujiandikisha, nisimpe kura?! Kwenda zako ... Subiri tupige kura then uje ulete hadithi hizi hata kama zina ukweli.
sitachagua shetani kisa kajibanza kwenye uwaraza wa kanisa
 
Ukweli maana yake Ni nini❔➖mkweli hajigambi,hajikwezi na wala hajitapi.Mkweli husifiwa,huonwa na pengine huwa hajitambui kama Ni mkweli.
Khaa!! Angalau ugetumia time yako kidogo kusoma na kutafakari kabla :glasses-nerdy:
 
Mabadiliko ya kweli hapa nchini petu yatapatikana tu pale tutakapoweza kuwa na KATIBA ILIYOTOKANA NA MAPENDEKEZO YA WANANCHI WENYEWE; SASA KATI YA lOWASSA NA MAGUFULI NANI ANATUAHIDI KUTUPATIA KATIBA HIYO? Mimi nitampa kura yangu yule ambae atatupatia katiba tuitakayo, nao ni UKAWA na sio Lowassa kama Lowassa but as an UKAWA VEHICLE.
 
Hukisii nini wakati umevamia wimbo usioweza kuucheza?

Wimbo wa kujifunza haukeshi ngomani wala aelekae jiwe hakumpi kuwa na mwana!!

Kubali umekurupuka na kichwa chako kidogo kama kima!!!
Dah! Umemtwanga za uso balaa.
Huyo ajuza kajiingiza kusupport kitu anachokilalamikiaga miaka yote mpaka mishipa ya shingo imemkomaa ,lakini kwasababu ni kilaza kama Mgombea wao ameshindwa kabisa kujipambanua.View attachment 288779
 
Ingependeza kama maelezo haya angekua anayasema mtu mwingine kukuelezea wewe...lakini kwa sababu unajisemea wewe mwenyewe yamepoteza ladha
 
mmechoka wewe na nani? Jisemee nafsi yako.

Hufahamu kama wengine kama mimi ninahitaji mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko ambayo yanaongozwa na Lowassa, Sumaye, Masha, Msindai, Mgeja na genge lao.
Akili mbovu kwani kushabikia CCM lazima uwe punguani? Ina maana hao uliowataja ndiyo pekee wanaoongoza mabadiliko? Changes are inevitable kawaambie wezi wa ESCROW, EPA, meremeta, rada, waliouza nyumba za serikali, na kila aina ya uwezo, tumechoka na wewe wala huyo chizi mzee hamtubadilishi.

Zamani tulifikiriri kila mzee ana hekima tumegundua hata wapumbavu wanazeeka pia na mmojawapo ni mtoa mada
 
Back
Top Bottom