Juu ya kaburi la baba mdogo kuna nyumba imejengwa. Je, nifanye nini?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Naomba msaada wa mawazo,

kaburi la baba yangu mdogo lilikaa muda mrefu bila kusafishwa.

Hakuzwikwa makaburini ila kwenye kiwanja cha familia.

Alifariki 1982/3. Eneo lile mji uliposogea ndugu wakapauza.

My father passed away watoto wa marehemu wapo ila hawajasoma hivyo hawajui waanzie wapi.

Mahali lilipo Kaburi imejengwa nyumba na ni chumbani kwa mwenye nyumba.

Nataka nianzishe mtiti maana wamegoma kuniuzia nyumba sasa mifupa ya marehemu naitaka!
 
Duuuh

Walilijua hilo kabla hawajanunua/jenga au mmewashtukiza baada ya kujenga? Kama walilijua basi kuna taratibu za kufuata.

Ila na nyie mtahojiwa, iweje kiwanja chenye kaburi kiuzwe?, sawa inawezekana kwanini hamkuhamisha mabaki?

Japo na mnunuaji nae atakutana na hilo swali kutoka kwenye mamlaka,
Iweje ununue kiwanja chenye kaburi na ukajenga nakati kuna taratibu za kufuata kuhamisha mabaki?

Kuna makosa ya makusudi kwa upande mmoja kati yenu, au wote.

Sina uhakika sana, lakini nahisi pa kuanzia ni Mamlaka ya nyumba na makazi.
 
reyzzap,
Nadhani hawakujua pia hata cc tulikuwa wadogo na waliokuwepo wengi wametangulia MYH ila majirani na wazee na hata Bibi alisema hapo Kuna KABURI Tena chini ya chumba Cha kulala sasa Mimi nataka nikafukue nitoe mifupa nikaizike Tena hawataki gharama zote nitalipia mpaka ku rebuild wamekataa.
 
Basi waweza fuata taratbu kama kweli umedhamiria na hata kugharamikia marekebisho yatakayohitajika.

Ila sasa mzee uwe na uhakika kweli kweli km hilo kaburi lipo hapo, specificaly chumba hicho. Laa sivyo utapata usumbufu na gharama za bure na pia Kupata second chance Itakua ni ndoto, unless wakubali ununue nyumba.

Yaani kwa ufupi usiende kubomoa kwa ku bet, wewe unafika unapiga sululu unakua na uhakika 100% unakutana na Fuvu.
 
Aaaah umenikumbusha kuna nyumba niliwahi panga Kigamboni, nimekaa kama miezi mitatu hivi. Sasa nikafahamiana na jamaa wa pale, kwenye story story siku wakanichana bhana, "aah huyu mzee noma sana hizi nyumba za kupangisha alinunua eneo la makaburi akajenga" kuna mmoja akathibithisha kabisa kilipo chumba changu ndo lilikuwa kaburi.

Toka siku hiyo kile chumba nilikuwa silali kwa raha, hofu kubwa kuna kipindi naota ndoto za ajabu wakat kabla ya hapo mambo yalikuwa shwari, nilisepa bila kuaga.

Anyway sidhani kama huwa serikali wana-care sana makaburi ambayo yapo nje ya eneo la makaburi.
 
Huwezi kujenga juu ya kaburi alafu ukaishi kwa amani kwenye nyumba hiyo! Kaburi ni lango la mashetani yatakusumbua! Labda huwe mchawi ndo utakuwa na uthubutu wa kujenga juu ya kaburi! Watu wengine kiwanja tu kakaribiana na kaburi hanunui sembuse kujenga? Kwenye makaburi kuna maroho machafu na utaambatana na ndoto mbaya na mikosi!
 
Naomba msaada wa mawazo,

kaburi la baba yangu mdogo lilikaa muda mrefu bila kusafishwa.

Hakuzwikwa makaburini ila kwenye kiwanja cha familia.

Alifariki 1982/3. Eneo lile mji uliposogea ndugu wakapauza.

My father passed away watoto wa marehemu wapo ila hawajasoma hivyo hawajui waanzie wapi.

Mahali lilipo Kaburi imejengwa nyumba na ni chumbani kwa mwenye nyumba.

Nataka nianzishe mtiti maana wamegoma kuniuzia nyumba sasa mifupa ya marehemu naitaka!
Wengi wamejenga juu ya makaburi bila kujua.
Mila na desturi za makabila yetu zinatofautiana sana. Sisi wengine makaburi sio big deal. Baada ya muda panandwa migomba na maisha ya kawaida yanaendelea.

Kwa wengine ni issue kubwa sana. Matambiko nk.

Hata kiserikali kwa sheria kabisa. Miaka 50 baada ya mtu wa mwisho kuzikwa, ni eneo kama mengine tu. Lolote linaweza kufanyika hapo.
 
Huwezi kujenga juu ya kaburi alafu ukaishi kwa amani kwenye nyumba hiyo! Kaburi ni lango la mashetani yatakusumbua! Labda huwe mchawi ndo utakuwa na uthubutu wa kujenga juu ya kaburi! Watu wengine kiwanja tu kakaribiana na kaburi hanunui sembuse kujenga? Kwenye makaburi kuna maroho machafu na utaambatana na ndoto mbaya na mikosi!
Unawaambia nini ndugu zetu wachaga wanaozika kwenye makazi yao ?
 
Kama ww ni mfuasi wa dini, au mfuasi wa imani za jadi fuatilia kwa wanazuoni au wakuu wa Mila Kisha ujue inakupasa kufanya nini?

Khali Kama hiyo inapotokezea ? Yawezekana fikra zako za upendo kwa Marehemu zikafarijiwa na wanazuoni au wakuu wa Mila.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom