Juu ya Dini na Katiba Yetu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juu ya Dini na Katiba Yetu!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jul 11, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Je, ugharamiaji wa Mahakama za Kadhi unaweza kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977? Ndiyo!
  Ibara ya 19 (2) inaeleza kwamba "Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za ma mamlaka ya nchi". Kwa kuwa Waislamu wamesema kwamba uendeshaji wa Mahakama za Kadhi ni kuendesha ibada Mamlaka ya nchi haitakiwi kuingilia ibada hizo bali wahusika waachwe waendelee na uendeshaji ambalo ni jambo la mtu binafsi.

  2. Je, kuwepo kwa Mahakama za Kadhi Zanzibar ni kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hapana!

  NYONGEZA YA KWANZA ya Katiba hiyo imetaja Orodha ya Mambo ya Muungano na suala la Uenezaji wa Dini, Kufanya Ibada, Kutangaza Dini sio la Muungano. Pia suala la Mahakama zote isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano sio jambo la Muungano. Kwa hiyo suala hili ni la Tanzania Bara pekee ambapo utangazaji wa dini upo nje ya Mamlaka ya Nchi. Katika Ibara ya 99 (2) (b) ya Katiba ya Zanzibar, 1984 imeandikwa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano haitahusika na mambo ya Kiislamu ambayo yameanzia katika Mahkama za Kadhi. Kwa hiyo Mahakama za Kadhi za Zanzibar zimeanzishwa kwa Sheria za Zanzibar kama zilivyo Mahakama zingine hadi Mahakama Kuu, isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.

  3. Je, kuna mtu amewakataza Waislamu kuunda Mahakama za Kadhi? Hapana! Wafuate Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kuhusu uenezaji wa dini na sio kunukuu Katiba za Kenya, Ethiopia, Uganda, n.k.!
   
 2. m

  majuva Senior Member

  #2
  Jul 11, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TOO much about mahakama ya kadhi, kwani hii inatofauti gani na zilizotangulia, nini kipya kitapatikana katika thread hii ambacho kwingine hakipo, kila siku new thread, is this the only issue now for the development of our country????

  ebu leteni habari kuhusu mustakbali wa wale mafisadi..labda watanzania wanaweza wakagaiwa vile vijisent vikasaidia kuinua hali ya maisha
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ..anatafuta attention Mwenzio!!!!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Acha kukwepa hoja kiaina!
   
 5. m

  majuva Senior Member

  #5
  Jul 11, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna hoja hapo mkuu, hayo yote ni marudio, ni bora ungechangia kule kwenye thread zilizotangulia, mbona yote hayo kule pia yapo?

   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  .... Ibara ya 19 (2) inaeleza kwamba "Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi......!

  Mmesahau tu ,watu walikuwa wakieneza dini hapa na mihazara kibao .wwakubwa wakikiristu walipoona wengi wa wafuasi wao wanabwaga manyanga na kuingia kwenye uislamu ,mkaingilia kati na kusema mnakashifiwa ,mihazara ile ikafungwa ,sasa hapo hamkuona kama katiba inavunjwa ,ila kelele za mlango hiyo ni sera ya CCM sasa sijui kama watawasikia.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hujaelezea ni kwa vipi serikali ilikuwa inaendesha hiyo mihadhara! Nafikiri pia ilifungwa kwa kuwa ilikuwa inahatarisha amani!
   
Loading...