Justine Kasusura: Mtanzania aliyefungwa "kwa kupiga pesa ndefu" ktk historia ya Tanzania na kisha kupangua kifungo bila wakili Mahakama ya Rufaa!!

Mkuu punguza jazba huu ni uzi wa JF sio proffessional article kwenye journal wala sio kitabu hiki. By the way hii ni stori ya miaka 10 iliyopita na sijui hao ma profesheno wako wapi kwanini hawajaiandika..?
Kamaliza BAed UDSM huyo acha aoneshe mbwembwe zake
 
'Pandikizi la mtu'
Screenshot_20190411-085525.jpeg
images%20(6).jpeg
images%20(7).jpeg
images%20(5).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiri ktabu mkuu
1. Usuli:

Watanzania nchini kote, kuanzia Ntwara hadi Kagera, Ijumaa ya tarehe 3.8.2001 saa 2 usiku, walipigwa bumbuwazi na kushindwa kuamini, pale walipomshuhudia luningani, SACP ALFRED TIBAIGANA, aliyekuwa RPC Kanda Maalum Dsm kuanzia 2001-2008, akitoa "Breaking Newz" kwa waandishi wa habari kuhusu unyan'ganyi wa $ 2M (TZS 4.400.000.000/=) uliokuwa umetokea jana yake majira ya saa 5 asubuhi nje kidogo ya "Airport" ya JKIA, ukiwa ni unyang'anyi wa kihistoria wa fedha nyingi kuwahi kutokea nchini ulioweka rekodi kipindi hicho.

RPC TIBAIGANA aliujuza umma kwamba mtuhumiwa wa unyang'anyi huo ni pandikizi la mtu lenye wajihi wa miraba minne liitwalo JUSTINE KAKURU KASUSURA, dereva wa kampuni ya ulinzi ys Knight Support yenye makao makuu yake eneo la Victoria, Dsm. Mzee baba" huyo alikuwa "amesepa na burungutu la fweza kama zote" na kutokomea kusikojulikana na kwamba "msako wa kufa mtu" ulikuwa umeanza kurindima nchi nzima hususan maeneo ya mipakani. Mwisho, RPC TIBAIGANA alitoa rai kwa wananchi na wasamaria wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo.

2. Miezi 5 Ikapita KASUSURA Hajulikani aliko

Licha ya kumtafuta maeneo mbalimbali, lakini KASUSURA hakuweza kutiwa mbaroni kwa miezi 5.

2. KASUSURA abambwa Hotelini, Mbeya usiku wa Manane!

Baada ya kupita miezi 5, huku wananchi wengi wakiamini kuwa kwa "mbumba" zote zile lazma "Mzee Mzima" KASUSURA atakuwa "amesepa" kwenda nje ya nchi na kwamba sasa atakuwa "akila bata refu" kwenye "viwanja vya mbele" kama Hawaii au Bahamas, walipigwa mshangao mkubwa ilipotangazwa kwamba KASUSURA amekamatwa usiku wa manani, jumatatu ya tarehe 24.12.2001(Christmas Eve), kwenye hoteli ijulikanayo kama "Three In One" iliyoko maeneo ya Soweto, Mbeya.

KASUSURA alikuwa amefikia hotelini hapo siku ya Jumapili, tarehe 23.12.2001 saa 12 jioni akitokea Sumbawanga na kujifanya ni mfanyabishara. Wakati akiwasili hotelini hapo, KASUSURA alikuwa amevaa kofia kubwa kuficha uso wake na akapewa chumba na. 101K ambapo katika rejista hakuandika jina la KASUSURA bali aliandika jina JOHN LAIZER na akalipia malazi ya siku moja kwa "buku tatu jero" (TZS 3,500/=).

Jioni ya Jumatatu hiyo, "mandata" walitinga kwenye hoteli hiyo na kuweka mtego kabambe nje na ndani ya hoteli hiyo huku wengine "wakizama" uvunguni na kabatini kama makomandoo wa Kiisraeli!.

Usiku wa manani, siku hiyo ya mkesha wa krisimasi, KASUSURA, huku akiwa yuko "bwaksi" baada ya kuwa "amepiga vyombo" kisawasawa baa, alirejea hotelini hapo akiwa na nungayembe alilojihomolea kwenye baa alikokuwa "akipombeka".

Alipojongea mapokezi, huku akiongea "Kikristu" kiiiingi, kama ilivyo kawaida kwa walevi wengi kupenda kuongea lugha ya "kwa mama" wanapokuwa "bwii", aliomba ufunguo na kuelekea chumbani kwake.

Baada tu ya kufungua mlango na kuwasha taa, KASUSURA akakutana uso kwa uso na "mandata" walioibuka kama "Bruce Lee" kutoka uvunguni na kabatini na kumtia KASUSURA nguvuni kiulaiini kama kumsukuma mlevi! Baada ya KASUSURA kunyakwa "hakuna rangi aliacha kuiona" na pombe zote ghafla zikamuisha kichwani akawa ameduwaa kama "zombi"!. Aliposachiwa alikutwa na TZS 200.000/= tu.!.

3. IGP MAHITA Aeleza Polisi Wamtorosha KASUSURA

Huku wananchi wengi wakilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kumkamata KASUSURA, zikaenea taarifa zisizo rasmi kwamba kuna polisi wengi wasio waaminifu walikuwa "wamevuta mkwanja mrefu" na kumsaidia KASUSURA kutokamatwa. Ilidaiwa kwamba kila polisi walipokuwa wakimkamata KASUSURA walikuwa "wanavuta mkwanja" kisha wanawapigia simu wenzao mkoa mwingine na "kuwapigia pasi" ili wamkamate na "akizama mfukoni" wanamwachia.Kutokana na sintofahamu hiyo, IGP wa wakati huo, aliyekuwa mtu wa shoka asie na mchezo, Alhaj OMAR IDD MAHITA, ikabidi aongee na waandishi wa habari tarehe 9.1.2002 na kukanusha vikali huku akibainisha kuwa si kweli kwamba polisi wengi wamehusika bali ni wachache tu. IGP MAHITA alifafanua kwamba kuna polisi 8 tu wakiwemo 3 waandamizi wanaodaiwa kumsaidia KASUSURA kutoroka walikuwa wamekamatwa na kusimamishwa kazi.

IGP MAHITA aliwataja polisi hao kuwa ni SSP BONAVENTURE MSHONGI(RCO- Tanga), ASP BEATRICE MAONA na ASP DEUSDEDIT KAJUNA(Ofisi ya RCO, Dsm), C.236 Sgt EMMANUEL na Konstebo ROGATHE(Tanga), E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH.

4. DCI ADADI Aeleza "Kufyekelewa mbali" kwa Polisi 5"

Tarehe 15.1.2002, aliyekuwa DCI, ADAD MOHAME RAJAB, aliufahamisha umma kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa limewafikisha Mahakama ya Kijeshi polisi 5 ambapo walipatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kutozingatia maadili ya polisi.

DCI ADADI, akiwa amekunja ndita na kuonesha kukerwa, alitiririka:
"Jeshi la Polisi limewafukuza kazi polisi wafuatao C. 236 Sgt EPHRAIM, E. 635 Konstebo ROGATHE, E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH. Hawa walikuwa wamefunguliwa mashtaka Mahakama ya Kijeshi na wamefukuzwa kazi kwa kukiuka maadili ya polisi na watashtakiwa mahakama za kiraia. Polisi hao walimkamata na kumuachia KASUSURA zaidi ya mara 3 Dsm, Tanga na Arusha, kitendo ambacho kimelitia aibu jeshi la polisi".

5. KASUSURA na "Wenzake" 6 Wafikishwa kwa "Pilato" Kisutu

KASUSURA, baada ya kuandika maelezo yake, alifikishwa mahakama ya Kisutu tarehe 7.1.2002 na Land Rover Defender No. PT 0881 akiwa pamoja na washtakiwa wengine 6 ambao ni WICKLIFF URASSA, LEONARD URASSA, LUCY URASSA(32-Mwanafunzi wa IFM) PROFILY KWEKA, WÌLLIAM MBETWA na LIBENT LIKUNDWA. Mahakama ya Kisutu ilijaa hadi pomoni kwani wakazi wa jijini la Dsm wanaosifika kwa kupenda "ubuyu" walitinga mahakamani hapo mapema kabisa kujione wenyewe huyo KASUSURA anafananaje.

Mwendesha mashtaka, ACP RAINHARD LISAPITA, aliwasomea mashtaka 5 ya Kula njama, Unyang"anyi wa kutumia silaha, Wizi na Makosa 2 ya Kupokea Mali ya Wizi. KASUSURA alikuwa akitetewa na Wakili nguli na bingwa a kupangua kesi za jinai, MAJURA MAGAFU. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao hivyo upande wa mashtaka ukaita mashahidi kuthibitisha mashtaka.

6. Mahakama ya Kisutu yaelezwa "Mchezo -Mzima" Ulivyokuwa:

Mashahidi wa upande wa mashtaka walieleza kwamba asubuhi ya siku ya tukio, 2.8.2002, KASUSURA alikabidhiwa na viongozi wake gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin TZL 3742 isiyopenya risasi ili kwenda JNIA kuchukua mzigo.

KASUSURA akaelekea JKIA akiwa na mwenzake, SAID MUSSA, aliyekuwa na jukumu la kupokea mzigo uliokuwa umewasili kwa Swiss Air ukiwa ni mali ya Citibank ambaowalikuwa wameingia kandarasi na kampuni ya Knight Support kuwapelekea mzigo huo ofisini kwao.

DAHACO walimkabidhi SAID MUSSA mzigo huo majira ya saa 4.30 asubuhi na akauweka vizuri nyums ya gari kisha akafunga kwa ufunguo.

KASUSURA akawasha gari na kuanza kuondoka JNIA na alipokunja kulia ili kuanza kuelekea mjini, "Mzee baba" KASUSURA "alijifanya kama anajikuna" kisha akaliegesha gari hilo mbele ya magari 2 aina ya Toyota Landcruiser na Toyota Corrola. Ghafla bin vuu, KASUSURA, kama VAN DAME, akatoa pisto na kumnyooshea SAID MUSSA na kumwambia _"Huu ndio mwisho wa mchezo"_na kumwamu "aishie". KASUSURA akamnyang"anya MUSSA funguo akaushusha mzigo huo akisaidiwa na watu wengine waliokuwa kwenye gari zile 2. MUSSA, baada ya kimuhemuhe hicho, alienda kuripoti kituo cha polisi ambapo alishikiliwa na kuanza kuisaidia polisi.

Upande wa mashtaka ulipofunga kesi yao, mahakama ilimuona KASUSURA peke yake ndiye mwenye kesi ya kujibu hivyo iliwaachia huru washtakiwa wengine wote.

Huku kesi hii ikiwa inaunguruma, tarehe 16.1.2002, maafisa 8 wa polisi(3 wa ngazi za juu aliwemo mwanamke mmoja) na 5 wa ngazi za chini walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashtaka 2 ya Kula njama ya kumtorosha KASUSURA na Kupokea rushwa toka kwa KASUSURA.

KASUSURA, bada ya kuonekana ana kesi ya kujibu, alitoa utetezi na kuelezea kuwa mashahidi wote wa upande wa serikali walikuwa "wameipiga fiksi" mahakama kwa hekaya zao za Abunuwasi. KASUSURA alidai kwamba ukweli ni kuwa yeye wakati aliendesha ile "ndinga" aliyokabidhiwa na ofisi yao ya Knight Support na baada ya kuchukua mzigo huo uliokuwa na "mbumba za kufa mtu" ghafla alipoanza kuendesha na akiwa nje kidogo ya JNIA "Watu wenye Kazi zao" yaani "Mabandido" walimteka na kusepa na "Mkwanja" wote!.

Huku kesi ikiwa inanguruma, KASUSURA alifiwa na mkewe, Bi. FAUZIA LAIZER tarehe 22.2.2005. KASUSURA alimuomba hakimu ruhusa ya kwenda kumzika mkewe ambaye alikuwa akifika mahakamani hapo kila mara na mtoto wao wa miaka 9.

Mh. Hakimu "alimchinjia baharini" KASUSURA kwa kusema: "Mahakama imetupilia mbali ombi la KASUSURA. Hatusemi kama itatokea, lakini ikitokea mshtakiwa akatoroka, wote tutawajibika".

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mh. Hakimu SILVANGILWA MWANGESI alitoa hukumu siku ya Ijumaa tarehe 30.3.2007 ambapo "alimpiga" KASUSURA "mvua" 30 kwa kosa la unyang'anyi na "mvua" 5 kwa kosa la wizi na kwamba atatumikia miaka 35 lupango (consecutively).

7. Polisi 8 Waachiwa huru

Polisi 8 waliokuwa wameshtakiwa kwa kudaiwa "kuvuta mbumba" na kumtorosha KASUSURA waliachiwa huru na mahakama hiyo.

SSP BONAVENTURE MSHONGI, aliyekuwa RCO wa Tanga wakati wa msala huo, alikuja kupandishwa cheo na kuwa ACP. Aidha, aliteuliwa kuwa RPC Pwani kabla ya kuhamishiwa Simiyu ambako analitumikia taifa lake vizuri tu na kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu.

8. Wakili MAJURA MAGAFU Akata Rufaa Mahakama Kuu

MAJURA MAGAFU, wakili wa KASUSURA, alikata rufaa Mahakama Kuu huku akiainisha sababu 6 za kukata rufaa.

Rufaa hiyo ikapangwa kwa Mh. Jaji THOMAS MIHAYO ambapo pande zote 2 zilisikilizwa.

Tarehe 23.6.2010 Mh. Jaji MIHAYO, akitoa hukumu, "aliimchinjia baharini" KASUSURA kwa maelezo kwamba rufaa hiyo haikuwa na "mashiko" ingawa alipunguza kifungo kutoka miaka 35 hadi 30 kwa maana ya kuzitumikia zile adhabu mbili za miaka 30 na pia 5 kwa pamoja concurrently badala ya kwa kufuatana consecutively.

9. KASUSURA Akata Rufaa Mahakama ya Rufaa

Baada ya kutoridhishwa na hukumu ya Mh. Jaji THOMAS MIHAYO, KASUSURA aliamua "kuingia fronti" mwenyewe bioa wakili kwa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa nchini ambayo ndiyo ngazi ya juu kabisa katika mfumo wa mahakama zetu ambapo Majaji 3 hukaa na kusikiliza na kuamua rufaa.

_"Mnyamblis" KASUSURA aliainisha sababu 9 za Rufaa.

Baada ya rufaa hiyo kupokelewa, Majaji 3 walipangiwa kuisikiliza. Majaji hao ni Mh. SEMISTOCLES KAIJAGE , MBAROUK MBAROUK na SAIDA MJASIRI.

Mahakama hiyo ikiketi jijini A-Town" ilisikiliza rufaa hiyo tarehe 11.4.2016. Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na TUMAINI KWEKA(PSA) akisaidiwa na CECILIA MKONONGO wakati "Mzee Baba" KASUSURA alionesha "unyamblis" kwa kujisimamia mwenyewe kwenye rufaa hiyo bila wakili.

KASUSURU, katika jitihada kubwa za kuhakikisha "anaipotezea lupango", aliainisha "matundu" kedekede kwenye ushahidi wa upande wa mashtaka.

Miongoni mwa "nondo na misumari ya moto" iliyodadavuliwa na "Bush Lawyer" KASUSURA ni Kwanza, Polisi walimhoji kwa masaa mengi kupita kiasi bila kuomba ruhusa ya korti kitu ambacho ni kinyume na sheria, Pili, Jamhuri haikumleta mtu hata mmoja wa Citibanki kuthibitisha kuwa mzigo ni wao na Tatu, Kulikuwa na tofauti ya kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye Hati ya mashtaka na ushahidi uliotelewa na mashahidi wa upande wa mashtaka kitu kinachoonesha hawajui kilichowaketa mahakamani au walikurupuka!.

Majaji hao waliwaweka "Kitimoto" Mawakili wa serikali ambao kijasho chembamba kiliwatiririka licha ya kuwa jiji la Arusha ni baridi na AC ilikuwa ikinguruma kortini! Hatimaye, majaji hao wakapanga kutoa hukumu siku ya Jumatatu, tarehe 9.5.2016.

"Siku ya Siku" ilipowadia, Mahakama hiyo, kama ilivyotarajiwa na walioskiliza jinsi rufaa hiyo ilivyosikilizwa, huku "ikiwachana" vilivyo Polisi na Waendesha Madhtaka, ilimwachia huru KASUSURA ambaye alionesha meno yote 32 kwani alikuwa amekaa Lupango kwa miaka 15.

Katika hukumu hiyo, Majaji hao walitiririka ifuatavyo:

"...With due respect, We wish to state from the outset that We have noted with great concern that this case has been badly investigated and consequently poorly prosecuted. We agree with the appellant, KASUSURA, that his cautioned statement was taken outside the prescribed four hours as required by Section 50 and 51 of the Criminal Procedure Act, 1985. The record does not show that an extension of time was granted by the magistrate in terms of Section 51 (1)(a) of the CPA. In the event, We expunge the cautioned statement which was admitted in contravention of the requirements of the law".

"The Charge sheet shows that the money belongs to Citibank but for no apparent reason the prosecution did not bring any witness from Citibank to testify that the money is, indeed, theirs hence We agree with KASUSURA that the prosecution failed to prove its case without any reasonable doubt".

Hivyo KASUSURA aliachiwa huru ambapo Jumanne, tarehe 10.5.2016 alitolewa gerezani huku akiwa "amepigilia" suti na kuonekana kama Diwani na si mfungwa!. KASUSURA alipokelewa kwa bashasha na nduguze ambao walimvisha shada la maua.

Hadi anaachiwa, polisi walikuwa wameambulia kupata TZS 2,500,000/= kati ya TZS 4.400.000/=.

10. Maisha ya KASUSURA Akiwa Lupango:

KASUSURA, akiwa gerezani Ukonga akitumikia kifungo chake, alikuwa "mtu poa sana" kwani alikuwa mpole, mtiifu, mwenye nidhamu na mnyenyekevu sana. Kutokana na umri wake na tabia yake nzuri alichaguliwa kuwa Mnyapala. KASUSURA akiwa Mnyapala aliwasaidia vijana wengi kwa ushauri mujarab uliopelekea baadhi ya wafungwa kubadilika tabia na wengine kushinda kesi zao. Aidha, hata yeye alijifunza mengi kwani alipoingia lupango hakujua baadhi ya kazi mfano ushonaji lakini akatokea kuwa mmoja wa mafundi wazuri hadi kushiriki kushona nguo za wafungwa wenzake.

Tafakuri Tunduizu:

1. Je , zile TZS 4,397,500,000/= ziliyeyukia wapi?

2. Je, kampuni ya Knight Support iliilipa Citibank au Citibank ililipwa "insurance"?

3. Je, kuna kifungu cha sheria kinachomkataza Jaji/Hakimu kumkataza mshtakiwa kwenda kumzika mtu wake wa karibu au anatumia "common sense"?

4. Je, ni kwanini polisi walishindwa kufuata taratibu za kumhoji mtuhumiwa? Je, ni kwanini haikutumia weledi hadi kutukanwa na majaji wa Mahakama ya Rufaa? Je, kwanini haikumleta mtu wa Citibank?

5. Je, ni haki mtu kukaa miaka 15 kisha kuambiwa hana hatia?

NB: Kujua KASUSURA sasa yuko wapi na anafanya mishemishe gani baada ya kutoka Lupango, na kujua nani aliwatonya polisi kuwa KASUSURA yuko hoteli ya _ Three In One_ na mengine mengi subirini KITABU..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasusura daah! Kawaponza mandata wengi kwa tamaa zao! Segera, Tanga mjini jamaa alikuwa anamwaga tu mshiko akikamatwa! Story Ni nyingi Sana ila kinachoelezwa pesa haikuingia hata ktk gari ya knight s,mzigo unapokelewa ukaingizwa ktk gari tofauti hakuna alioonyeshewa bastola,kingine inavyoonekana jamaa alipiga pesa bila kujua mipango ya mbeleni,ni Kama mtu flani aliojaribu nafasi akakipata bila kutegemea Sasa hajui afanye Nini! Siwezi kuisahau story ya kasusura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni kivutio tosha cha utalii tukimtumia vizuri anaweza akalitambukisha Taifa vyema zaidi ya Pierre... Dola million 2 unakamatwa na vilaki kah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Noma sana ila inaonesha kasusura alikuwa mbuzi wa kafara tu wenyewe walishakula mpunga wao zamani.
Kasusura hakuwa Mbuzi wavkafara, pesa alipiga yeye ila kwenda na Pesa kwa Urassa ndio kosa lake, madeal makubwa kama haya usicheze na Wachaga, pesa nyingi alibaki nayo huyo mchaga.
 
Kabla hajaandika hukuwa na cha kukosoa alipoandika ndipo uwezo wako wa kuona makosa ukatukea huoni kuwa unatatizo la kuona mbali yaani huna uwezo wa ku creat ila wewe ni ku modify tu. Kimsingi huwezi kuandika chochote.
Kama unabisha .jifanye kama unajikuna utupe hata ya akina Uncle Tom
Wabongo mtaacha argument za kijinga namna hii lini? Tuwaachie watu wenye uwezo kufanya kazi wanazozijua. Unataka mtu anayeandika below level akubalike na asihojiwe kwa sababu mimi siwezi kuandika? Stupid thinking!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hvyo mbunye, ulevi ndio vilimponza Sterling almando kasusura?? Ukute alikula bata sana akasahau kwamba yuko wanted
 
Hahah mkuu historian nzuri sana hii ila pia nimependa uandishi wako,yote kwa yote huyu faza alikuwa boya na siyo ajabu aliyemchoma ni muhudumu wa hiyo hotel au nungayembe alilokokotana nalo bar coz kipindi kile ilitangazwa bonus kama sikosei 10Mill {ilikuwa hela nyingi sana wakati huo} pia tukumbuke kipindi hiko pesa yetu ilikuwa na thamani ilikuwa uki-change Tsh1,000/= tumia utakavyotumia hadi jioni kesho unaamka na salio.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Siku ya kusikiliza rufaa yake nilikuwepo. Ni kweli alikuwa hana wakili lakini alikuwa ameandikiwa hutuba ya kisheria kabisa, akawa anasoma tu. Kilichomuokoa ni defective charge sheet. Alishitakiwa kwa kuiba dola za USA lakini ushahidi ukagongana kuwa kulikuwa na currency za mataifa mengine. Pili ni kuwa kulikuwa hakuna maelezo ya kwa nini ilipita zaidi wiki moja toka akamatwe na siku ya kufikishwa court. Serikali ilipata shida sana kulezea hoja hizo
Aliandaliwa maneno Yale yote,kunawatu walikuwa nyuma yake ili kufaidi pamoja xilr dollars.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom