SI KWELI Justin Bieber ameimba wimbo maalumu kuelezea manyanyaso aliyopitia kwa P. Diddy

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu kuna wimbo nakutana nao TikTok na X ukiwa na sauti ya Justine Bieber akieleza namna alivyonynyaswa na P. Diddy alipoenda kwenye party ikamgharimu.

Kuna ukweli hapa. Wimbo huu hapa chini:



1727707304403.png
 
Tunachokijua
Kumekuwa na wimbo unaoitwa 'Lost Myself at Diddy Party' ukidaiwa kuwa ni wa Mwanamuziki Justine Bieber. Mashairi ya wimbo huo yanaeleza unyanyasaji ambao msanii huyo aliupata kwa Mwanamuziki Diddy.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com wa kimtandao umebaini kuwa wimbo huo haujaimbwa wala kutungwa na Mwanamuziki Justine Bieber.

Uchunguzi wetu umebaini kuwa Wimbo huo umetengenezwa kwa teknolojia wa Akili Mnemba (AI) kwa kuundwa mashairi na kuweka sauti inayofanana na Mwanamuziki Justine Bieber.

Sambamba na hilo, JamiiCheck imebaini kuwepo kwa Nyimbo, Picha za watu maarufu zinazotengenezwa kwa namna tofauti kuchochea tuhuma zinazomkabili Diddy kwa sasa.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom