Ripoti kuhusu uchimbaji wa dhahabu ambayo hivi karibuni imekuwa ikijadiliwa sana kwenye vyombo vya habari. Kama ilivyo ripoti ya Richmond, hii ni ripoti ambayo kila mtu anayewatakia mema watanzania na vizazi vyao vijavyo anapaswa kuisoma na kuifanyia kazi. Kwa ufupi, haya ndiyo baadhi ya masuala yaliyonigusa ndani ya ripoti hii na ambayo ningependa kuyafahamu/kuyafuatilia kwa undani zaidi:
1. Ardhi yetu ina dhahabu yenye uzito wa 'aunsi' milioni 45 na madini haya adimu yanachimbwa kwa kasi ya takribani 'aunsi' milioni 1.6 kwa mwaka.
2. Kasi hii mpya ya uchimbaji iliyosababishwa na kuwavutia/karibisha wawekezaji inatosha kumaliza hifadhi yetu yote ya dhahabu baada ya miaka 28.
3. Migodi 6 mikubwa ya dhahabu nchini inatazamiwa kufungwa rasmi baada ya miaka 10 maana kwa kasi hii dhahabu yote itakuwa imeshachimbwa.
4. Pamoja na kasi yote hii kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita serikali yetu imepata dola milioni 21.7 tu kati ya dola bilioni 2.5 za mauzo ya dhahabu nje.
5. Kuyapa makampuni makubwa ya kimataifa fursa nyeti ya kuchimba dhahabu kumesababisha wachimbaji wadogowadogo 400,000 kupoteza ajira.
6. 'Taasisi' ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inakadiria kuwa sekta ya madini nchini inaajiri 0.2% tu ya 'nguvukazi' yetu.
7. Vifungu vya mkataba wa kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji vinaizuia kampuni ya ukaguzi ya Alex Stewart Assayers kutoa ripoti yao.
8. Mrahaba wa 3% unatupatia wastani wa dola milioni 17. 4 kwa mwaka ila ungekuwa 10% kama ilivyo Botswana tungepata dola milioni 300 zaidi.
9. Rekodi zinaonesha kuwa serikali haijalipwa kodi ya makampuni, ya 30% ya faida zao, kwa sababu makampuni hayo eti yanadai hayajapata faida.
10. Benki ya Dunia ndiyo 'ilitushauri' mwaka 1992 na 'kutufadhili' mwaka 1997 ili tuanzishe mradi wa kuanzisha/kuendeleza sekta 'binafsi' ya madini.
Ripoti hii inadhihirisha kuwa ulegezaji wa uchumi tuliouanza kwa shingo upande katika miaka ya 80 na kuuendeleza kwa kasi ya ajabu katika miaka 90 ndio umetufikisha hapa. Wakati ndio huu wa kuzipitia upya sera na programu za uchumi wa soko huria 'tulizokopeshwa' na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa kabla hali haijawa mbaya zaidi. Pengine 'kichwa cha ripoti' kinamaanisha kuwa hii ni 'fursa ya dhahabu' ya kutunusuru.
NBNtaambatarisha RIPOTI yenyewe soon....INATISHA