Just in: UDSM wafukuzwa

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Kama kawaida ya serikali ya CCM-kutoa majibu rahisi kwa maswail magumu, dakika chache zilizopita, vijana wetu wa mlimani wameambiwa wafungaishe vilivyo vyao warudi nyumbani.

Haya Kikwete huyu aliyeahidi kuwa yeye asingefunga vyuo vikuu kwa sababu ya migomo imekuwaje tena?!
 
Mwanakijiji + mwanasiasa,

Kwa mkwara waliopigwa thru taarifa ya saa 7 nilidhania wataigwaya serikali kumbe wamekomaa hadi sekunde ya mwisho?

Maana waliambiwa wangerudishwa (kufukuzwa) nyumbani na kutakiwa kulipa laki 1 wale watakaorudishwa ikiwa ni pamoja na kuandika barua za kuomba kurejeshwa masomoni.

Pole zao; haya wengine yalitusibu enzi hizo... Haki kupatikana yataka jitihada sana. Ni raia wachache wanaoelewa undani wa kinachoongelewa na wanafunzi hawa na wengi ni rahisi kuona wanachodai ni utoto.

Yalianza haya mwaka 2000 nami nilionjeshwa joto ya jiwe tukipinga hii kitu inaitwa Cost Sharing.

Kazi ipo!
 
tatizo la serikali yetu ni kushindwa kujenga hoja zenye nguvu na badala yake wanajenga hoja kwa nguvu! Nimeshasema Prof. Msolla Wizara hii imemshinda watu hawaamini. Ni mara ngapi watakuwa wanawafukuza hawa vijana toka chuo ili kuonesha nani "got bigger balls"!? Of course serikali ina ubavu huo! Hivi kuna wanafunzi wangapi Chuo Kikuu.. we need to break down madai yao na kuona kama hoja hizo zina mantiki kweli. Hivi kuna mtu anajua idadi ya wanafunzi wanaotaka nyongeza hiyo, na nyongeza hiyo ni ya kiasi gani? Tunataka kuona ukweli wa madai ya serikali "kuwa haina uwezo" Nipeni hizo namba halafu nitawathibitishia kuwa serikali ina uwezo wa kutimiza hilo!!
 
Simple sana Mwanakijiji!

Ongea na rais wa serikali ya wanafunzi bwana mdogo mmoja anaitwa Magessa.

Huyu atakupa data za kueleweka and am sure he can give any data needed for this.

Namba yake ya mobile ukitaka naweza kukurushia kwa PM.

Ahsante
 
wOrM....labda tulikuwa wote..yaliyotusibu 2000! Ila mimi naamini FREE MONEY IS NEVER ENOUGH..Wengi tumesoma mlimani na we have first hand experience. ..sasa hivi wanapewa 3600 kwa siku....Tatizo hili ni la wanafunzi na serikali. As mwanakijiji said..majibu marahisi kwa maswali magumu. Kwanza wanafunzi bado wana mentality na elimu ya bure hatuwezi kuwalaumu ndivyo Nyerere alivyotukuza kwa kuamini kwamba tunaweza kuwa na sera za kuwakomboa wote! (JK na EL mlisoma bure na sisi tusome bure) wanasahau kwamba enzi hizo wanafunzi walikuwa less than 1000! waliokuwa wanaitegemea serikali. Leo Vyuo vyote vya elimu ya juu kuanzia UD mpaka Tengeru, Uyole, Nyegezi, Kairuki et al, vinaitegemea serikali iwalipie 100% (mkopo).

Sasa jiulize, hiyo hiyo serikali inabidi itoe elimu ya msingi bure kwa raia wote! na wana mpango wa kuweka elimu ya sekondari ya bure! Undoubtedly this is a very huge commitment ambayo serikali kama ya Tz HAIWEZI (LEAVE ASIDE COUNTER ARGUMENTS ON THIS KWAMBA TUNA RASILIMALI, SO WE NEED KUWEKA VIPAUMBELE). TUNAJUA WOTE SERIKALI VIPAUMBELE VYAKE. Tuna matatizo mengi. Where I come from hatuna hata dispensary ya kijiji, na Iam sure tuko wengi humu! sasa sijui kipi kifanyike, but I can assure you this project ya kuwapa watu mikopo ya 100% is not self sustaining! at all! Maybe we should moot ideas to invite private sector kusaidia kutoa mikopo! Do you think ingekuwa ni mikopo ya benki wanafunzi wangeandamana? i doubt..this tells you more of the whole issue!

Tatizo la serikali imejenga false hopes kwa watanzania kwamba inaweza ikafanya wanayotaka raia either through actions or ommissions, na sana sana wamefanya hivi kwa ajili ya kuscore political credits! Serikali haina muundo madhubuti wa kudeal na hili swala...tunafanya mambo kisiasa sana. I can assure hakuna chi ya maskini kama sisi.. inayoweza kuwapa mikopo hundred % watu wake kupata elimu ya juu. Forget. what we need ni kuweka sera ambazo zinaeleweka tuache maamuzi ya ad hoc basis

Swala la mikopo ni issue kubwa, I agree watu inabidi wsome, lakini vile vile Watz tuwe proactive katika maisha. Ulimwengu wa leo bwana elimu ni personal gratifications. Ndo maana kazi inatangazwa Dar mtu anatoka Peru anakuja kuwa consultant ofisi ya Raisi bongo! Swala la umaskini wa nchi yetu ndo watu wanalitumia, lakini jee, huu umaskini utaisha lini? unless we accept this to be a perpertual reason to justify continued governenment intervention in finanching education!

Kila la kheri my Alma maters at UD!
 
Wakulaumiwa ni wanafunzi wenyewe walijifanya wajanja pale walipovaa magwanda ya CCM na kwenda kumwona pale Karimjee. Sasa yako wapi? hakuna sababu ya Mzee Mwanakijiji kuwahoji. Wale wa Ukraine iliishia wapi?
 
wOrM....labda tulikuwa wote..yaliyotusibu 2000! Ila mimi naamini FREE MONEY IS NEVER ENOUGH


Hahaha najua wengine mlio humu yawezekana tuliimba pamoja kale ka wimbo ka 'kabla mambo kuharibika' ambako ni normal

"Nina imaniiiiii na Ojeeeendoooo....." hapo wengine tulijikuta u-waziri wa kishule unatutumbukia puani. Tukatemwa! Yote ni ajili ya umma wa watanzania na hawa wengine wadogo zetu tulipotimuliwa enzi zile walidhani tulikuwa tunacheza.

Anyway; Ole wahurumie hawa... hawakujua watendalo nyakati wakivaa zile Kijani! Labda walikuwa wana Yanga? Au ni sehemu tu ya wanafunzi. Ujue penye wengi pana mengi pia. Kuna uwezekano mkubwa kuwa si wote walipendezwa na wenzao kuvaa kijani kile.

Serikali hii hii ndiyo ilituzuia wengine kipindi kileee kuwa "Wanafunzi wa Elimu ya juu (nahisi na wakufunzi) hawaruhusiwi kujihusisha na mambo ya siasa moja kwa moja" lakini baadae nikaona kama ishakuwa ruksa japo sijui ilikuwaje. Kama iliruhusu wengine kuvaa T-shirt za CCM basi ujue ilishabariki siasa kuendeshwa chuoni.

We need to go deep; kuna uwezekano nao wanachochewa na wapinzani wa JK? Ah, hapo ndipo pabaya!
 
Tatizo la Wanavyuo halitotatuliwa kwa kuwafukuza chuo!Lazima Serikali kwa kupitia wizara Husika kuangalia kiini cha matatizo ya muda mrefu ya wanafunzi Tanzania.Ni Hatari kubwa kuwafukuza/kuwanyanyasa wasomi na kuwakumbatia Machinga!.Itakuwa Hatari vijana hawa wakiingia DOA kwenye Uzalendo wao.
Ukiona Baba anashindwa kuzungumza kwa Amani na kijana wake,ujue tatizo si la Mtoto tu hata Baba ana walakini katika Malezi ya Kijana huyo!.
 
Mzee Ole, samahani wanafunzi Ukraine wapi? mbona hilo sijasikia mwenzenu? au ndio mambo ya humu humu Jambo Forum?
 
Mikuki, sidhani kuwa wanafunzi wanadai pesa ya bure! Si hiyo ni sehemu ya mkopo, au sivyo?
Sasa kama ni mkopo sioni tatizo lipo wapi hapa - wapewe hela yao na waendelee na shule. Kama mkusanya malipo ya mikopo hiyo hatimizi kazi yake ipasavyo huko baadae, hilo si shauri la wanafunzi kwa wakati huu.
 
Kalamu,
Hoja ya serikali ni kwamba ukiwakopesha 40% utaweza kukopesha wanafunzi wengi zaidi kuliko ukiwakopesha 100% kwani chungu hakijajaa!
 
MKJJ,
You mean, 40% au 100%? Nadhani wakitaka INAWEZEKANA. Ni suala la vision na political will; baada ya hapo ni mipango. Vinginevyo, kupanga ni kuchagua!
 
Mzee Ole, samahani wanafunzi Ukraine wapi? mbona hilo sijasikia mwenzenu? au ndio mambo ya humu humu Jambo Forum?

Mzee mwanakijiji

Ulifanya interview na wanafunzi wa Ukraine ambayo nilisikiliza. naona sijui nini kilifuatia hebu tupe kilichotokea baada ya hapo?
 
Labda, ngoja vijana wakae nyumbani kwanza,watie akili, wakati serikali nayo inajipanga upya! Si unaona matumizi yashazidi mapato, sasa hizo pesa hawana tena; mpaka bajeti ijayo...
 
Haya yote ni matokeo ya mipango mibaya. 2005 JK na timu yake alijikuta akiahidi mengi hata yasiyowezekana kwa sera mbovu kabisa za chama chake.Ndoto hizo ndio jinamizi linalotafuna sasa.Hekaya hazileti mabadiliko wala haziongezi uwezo wa kukabili magumu. OLE kasema hapo juu,magwanda ya kijani sasa yanawaleta ukurutu mwilini. Acha wajikune.
 
Mkuki,

Elimu ya juu TZ sio bure kwasasa. Wanafunzi wanakopeshwa na kama tujuavyo ukikopeshwa inabidi ulipe baadaye.

Tatizo ni hilo la 60% na wanafunzi kulipa 40%. Kama huna hata ukiambiwa ulipe 5% utashindwa.

Pesa za mkopo sio lazima zitoke serikalini na badala yake zinaweza kutoka vyombo vya fedha na serikali ikaweka dhamana na labda kulipia interests
mpaka wanafunzi watakavyoanza kulipa.

Haya mambo yote ni kuongea kupitia wadau mbalimbali wa elimu. Kutunga sheria bila kuhusisha stakeholders wote matokeo yake ndio haya. Inatakiwa tujifunze na tukubali kwamba sio kila jambo lina simple answer. Kufukuza wanafunzi sio jawabu maana serikali na wananchi wana loose kuliko faida ambayo serikali inapata kwa kufukuza wanafunzi.
 
Je serikali ina uwezo wa kukopesha kiasi hicho?

Mzee Mwanakijiji,
Jibu la hilo swali liko wazi kabisa wanaweza sana tu. Tatizo la watawala wetu ni ubinafsi uliopindukia. Tuseme vyuo vyetu vina wanafunzi elfu ishirini, ni na mashaka hata kama wanafika, asilimia 40 wanayotaka watu wajigharimie ni kama sh laki tano au kwa haraka haraka dola mia 450, mara elfu ishirini ni kama dollar milioni kumi. Mradi bogus kama Richmond umetugharimu dollar 172 mil. au kamisheni ya rada imegharimu dollar mil 12. Kama wana pesa za kutapanya hivi watadai vipi hawana za kukopesha wanafunzi?
Mikuki,
Unajichanganya katika maelezo yako, hakuna anayedai free money, kama suala la kurejesha mikopo linaenda shaghalabaghala hili siyo tatizo la wanafunzi hawa bali ni serikali isiyokuwa na utaratibu wa urejeshwaji wa mikopo.
Hebu mtupe mifano huko kwingine duniani ambako wanafunzi wanajilipia ada zao kwaajili ya elimu ya juu. Na pia mtupe njia ya hawa wanafunzi kujipatia kipato cha kuweza kujisomesha, siyo muishie kutueleza tu eti wabebe mabox kama ninyi mnavyofanya huko mliko.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom