Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa!.

"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi nimeupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia umeupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu?.

Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Kwa vile tunatofautiana uelewa, just imagine ungekuwa na uwezo wa kuijibu hii SMS ya Rais Samia, ungekuwa na jambo lolote la kumweleza Rais Samia, ungemwambia nini?.

Mimi kwa upande wangu, ningemsalimia, ningempongeza kwa kazi nzuri, na amini usiamini pia ningemweleza kuwa sitaki uteuzi wowote wa hisani kutoka kwake.

Vipi wewe mwenzagu ungemwambia nini Mama baada ya yeye kukutumia SMS?.

Naendelea kusisitiza tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa
Asante Rais Samia kwa SMS ya sensa, tuko tayari kuhesabiwa na tutajiibu maswali kwa usahihi.

Nawatakia Sensa Njema.
Paskali.
Update
Mtu mwingine aliyefurahia kupokea ujumbe huu ni huyu
View attachment 2332646
Zitto ahesabiwa ampa tano mama Samia.
Zitto Kabwe kamaliza kuhesabiwa ana furaha kubwa Sana baada ya kupokea ujumbe wa simu kutoka kwa rais Samia ambapo naye aliuforward kwa m/kiti Mbowe incase Kama hakupata wake,
Jee na yeye mtamparura, kumbeza na kumtukana kama mlivyo nifanya mimi?.
P
 
Yani wewe jamaa kadiri siku zinavyosogea unashuka standards.

Yani push messages ndio unadanganya watu zimetoka moja kwa moja kwa rais?

Hizo texts si ndio mlikuwa mnazitumia kwenye uchafuzi mkuu za kumuombea kura jiwe baada ya kampuni za simu kushurutishwa na mkalabel jina la Tundu Lissu as "spam" kuelekea zoezi .

Historia huwa haidanganyi ila ni gharama kubwa kutetea uongo.

This is embarrassing and too low from you.
 
Pascal mbona heka heka nyingi sana ni huu huu Ubunge wa Akina Shyrose.Bhanji na Le mutuz?
Pascal sasa ni kama anazeeka. Uwezo wa kufikiri nao unapungua. Hivi rais akae chini aanze kuandika ujumbe aanze kuutuma. Kweli?? Kazi ya zuhura yunus ni nini sasa?

Unajua kuna level za kujipendekeza hasa pale unapotaka jambo lako. Ila ukifikia level ya uchawa hata unayemsifia anakuona mpuuzi na kukudharau na kukuona hautoshi.
 
Pascal sasa ni kama anazeeka. Uwezo wa kufikiri nao unapungua. Hivi rais akae chini aanze kuandika ujumbe aanze kuutuma. Kweli?? Kazi ya zuhura yunus ni nini sasa?

Unajua kuna level za kujipendekeza hasa pale unapotaka jambo lako. Ila ukifikia level ya uchawa hata unayemsifia anakuona mpuuzi na kukudharau na kukuona hautoshi.
Sisi wazee tunatakiwa kuunga mkono bila kuwa CHAWA
 
" ... Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Adv. Mayalla; ni sawa na kutaka kuuliza kwanini Mwl. Nyerere hakutuma SMS kwa watanzania at personal level! Kila zama na kitabu chake mzee, wakati wa Nyerere hata picha za rangi hazikuwepo sembuse kutuma SMS!

Nyerere aliwasiliana na wananchi kwa teknoloji iliyokuwepo wakati wake; kaja Mwinyi naye vivyo hivyo; Mkapa, Kikwete, Magufuli nao vivyo hivyo. Samia katumia tools ambazo ziko available kwa kizazi hiki; watakuja wengine na teknoloji za wakati huo, n.k. So, hakuna cha ajabu kuhusiana na statement yako hiyo!
 
Back
Top Bottom