Taso,Mkuu, Jussa sio Mbunge, hawezi kupeleka hoja yake kwenye Bunge la Muungano.
Kwenye Baraza la Wawakilishi haya mambo anayaongea kila wakati. Lakini yeye ni mwakilishi wa chama minority, hoja za minority mara nyingi zinazidiwa na nguvu ya namba. CCM, the majority hawataki muungano uvunjike, sababu CCM nayo itabidi ivunjike.
Ndio maana anafanya jitihada za kuzitoa hoja zake nje ya bunge, ku sensitive wananchi. Namuunga mkono asilimia 100, ni mkombozi wa wenzake Wanzanzibari na sisi pia Watanganyika.
Tunataka kila upande uwe ni dola huru yenye mamlaka yake kamili, ndani na nje ya nchi.
..kama umesikiliza mahojiano ya Jussa na aljazeera, amekiri kwamba Baraza la Wawakilishi lina mamlaka ya kuitisha referendum kuhusu muungano.
..kutokana na ukweli huo ndiyo maana baadhi yetu tumekuwa tunasisitiza kwamba suala hili lishughuliki haraka, sasa hivi, na BARAZA LA WAWAKILISHI.
..anachotakiwa kufanya Jussa siyo "kuyaongelea" tu masuala ya muungano, anatakiwa awasilishe hoja binafsi inayopendekeza Zanzibar ipewe FULL AUTONOMY, na kuwepo kwa "muungano wa mkataba."
..nadhani unakosea unapodhani kwamba Jussa anatutakia mema wa-Tanganyika. Kuwa makini sana na hayo mapendekezo ya "muungano wa mkataba." Hiyo ni hila tu ya wanasiasa wa Zanzibar kuendelea kuinyonya Tanganyika.
Last edited by a moderator: