Jussa na wawakilishi wenzake wasema kama Muungano uwepo basi ni wa mkataba kila nchi kuwa na Malaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jussa na wawakilishi wenzake wasema kama Muungano uwepo basi ni wa mkataba kila nchi kuwa na Malaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Sep 26, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  TUNATAKA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

  [​IMG]

  TUNATAKA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI KITAIFA NA KIMATAIFA ITAKAYOFUATIWA NA MUUNGANO WA MKATABA KATI YAKE NA JAMHURI YA TANGANYIKA

  Muungano wa Mkataba maana yake nini?

  Muungano wa Mkataba ni MASHIRIKIANO kati ya nchi mbili au zaidi ambazo kila moja huwa inabaki na mamlaka yake kamili ya KIDOLA kitaifa na kimataifa lakini vado zikawa zina mashirikiano katika maeneo maalum zitakazoamua kushirikiana, mahusiano ambayo huwa yanaongozwa na Mkataba.

  Muungano wa Mkataba ni tofauti kabisa na Muungano wa Kikatiba ambao huwa unamaanisha kuwepo kwa Serikali ya Muungano inayosimamia mambo ya Muungano. Katika Muungano wa Mkataba, kila nchi hubaki na Serikali yake kamili yenye kusimamia mambo yote. Yale maeneo ya USHIRIKIANO husimamiwa kupitia ama KAMISHENI YA PAMOJA au KAMATI YA PAMOJA kwa kadiri makubaliano yatakavyokuwa yamewekwa kwenye Mkataba.

  Ni zipi faida za Muungano wa Mkataba:
  1. Hakuna khofu ya nchi moja kuimeza au kuitawalia nchi nyengine.
  2. Kila nchi inabaki na uhuru na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kuamua mambo yake.
  3. Kila nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katika jambo lolote ililoamua mwanzo kushirikiana pale inapoona hakuna maslahi au faida kuendelea nalo.
  4. Huvutia nchi nyingi kuingia katika Muungano wa aina hiyo kwa sababu hakuna khofu ya kupoteza mamlaka au kupunguziwa madaraka au mambo yake kuamuliwa na nchi nyengine.

  5. Mahusiano huwa ni ya kirafiki na ya ujirani mwema yanayopelekea kuaminiana na kuondoa kutiliana shaka kusikokwisha.
  Zanzibar iwe na mamlaka yepi kitaifa na kimataifa katika Muungano wa Mkataba?

  1. Iwe na Serikali kamili yenye Wizara zote ikiwemo Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani na Ulinzi.
  2. Iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa na pia uanachama wa Jumuiya zote za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Nchi za Bahari ya Hindi.
  3. Iwe na Benki Kuu yake na Sarafu yake.
  4. Iwe na mamlaka yote ya kuamua serĂ¡ za fedha na uchumi, kodi na sarafu.
  5. Iwe na Uraia wake.
  6. Iwe na Paspoti yake na kusimamia Uhamiaji katika nchi yake.
  7. Idhibiti Anga yake na Usafiri wa Anga yenyewe.
  8. Isimamie Elimu ya Juu yenyewe na kuamua Mitihani gani itumie katika masomo.
  9. Isimamie na inufaike na rasilimali zake zote za ardhini na baharini ikiwemo mafuta na gesi asilia.
  10. Idhibiti yenyewe eneo la mipaka ya Bahari Kuu (EEZ) katika eneo lote inalopakana nalo.
  11. Idhibiti mamlaka mengine yote yanayokuwa yanamilikiwa n anchi kamili.

  Ni ipi Mifano ya Muungano wa Mkataba?
  - Muungano wa Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.
  - Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye wanachama 5 mpaka sasa.
  - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS).

  PAMOJA TUNAWEZA
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kwani viongozi wakuu wa zanzibari ni wakomoro hata wawaamulie kwa hasara yenu?

  Mwambieni Shein na Sefu waitangazie Tanganyika kwa niaba yenu kuwa mnasepa! Mbona katiba hamkukatazwa kuiandika!!!! Mamlaka mnayo, lakini waogaaaaaa, jifungieni kwenye kamjengo kenu semeni ili yawe sheria, haya myasemayo kwa kupayuka mabarabarani.
   
 3. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na sisi watu wa bara hatuutaki muungano mwingine wa mkataba kwa kuwa tayari tunao wa EAC. Kama wazenj mnaona vipi jitoeni kwenye huu muungano wa sasa muunde hiyo JWZ kisha mje kivyenu kwenye EAC. Wabara tumechoka kuwabeba mbeleko kila siku. Na the fact kuwa mnataka muungano wa mkataba na Tanganyika (ilhali tayari sisi tupo EAC) ni kutung'ang'ania ili tuendelee kuwabeba mbeleko zaidi na ziadi.

  Kama mna ubavu wa ku-exist kama JWZ basi fanyeni haraka muende kwenye BLW na muweke hoja hiyo mezani kama mlivyofanya katika marekebisho ya kumi ya katiba yenu na pia uamuzi wa kuunda GNU. Mbona kwenye mchakato huo wa marekebisho ya katiba na kuunda GNU sisi wabara hamkuomba baraka zetu? Sasa mnashindwa nini kwenye hili la kujitoa kwenye muungano mkatafuta kwingeneko kwenye muungano wa mkataba mkajiunga?!! Sisi huku, hatutaki mkataba na nyie. Tukutane EAC na muone kama mbeleko tuliyowabebea all along kama bado itakuwepo.

  Kifupi, acheni kelele zisizo za manufaa kama za bata, badala yake chukueni hatua na tukutane EAC. Sababu mnayo, nia (kama ipo) mnayo na uwezo mnao. Tukutane EAC kwenye muungano wa mkataba.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..hakuna haja ya mkataba baina ya Tanganyika na Zanzibar.

  ..tayari nchi za Afrika Mashariki zina mkataba wa uanachama wa jumuiya hiyo.

  ..TANGANYIKA na ZANZIBAR zivunje muungano na kujiunga na EAC ambayo makao yake makuu yako ARUSHA.
   
 5. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Ndo maana huwa nasema wazanzibar ni wazandiki na wanafiki kama nini. Jusa na wenzake wanazungumza kwa mafumbo lakini baada ya maelezo yote unaona wanataka nini . Kwa nini wazanzibar wanazungumza Muungano wa mkataba huku wakimaanisha kuvunja muungano. Maeleezo yote hayo ni kuvunja Muungano
  Sasa acheni usenge wenu , kuja na kauli moja kuwa hatutaki Muungano tunataka kuuvuja, hapo tutawaelewa
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hii kuna mtu anajua Zanzibar wanataka nini hasa?? Kama wanataka kujitenga je ni kwanini wanataka mkataba? Mkataba wa nini kama unataka kuwa nchi kamili? Je kama unataka kujitenga kwanini unajali sana jina jina Tanzania halitabadilika kwa mika mingi nchi imekuwa ikiitwa Tanzania na huwezi kuibadilisha sasa kwa sababu ya kujitenga. Zanzibar kama wanataka kujitenga wajitenge lakini wasijichanganye ma mambo ya jina Tanganyika au mikataba mingine kwani mikataba hiyo ndiyo imeleta matatizo. Hakuna mikataba ni tuwe nchi moja au ncho tofauti tuone nani atataka kuwa upande wa Zanzibar!!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hapa ni TANGANYIKA na ZNZ zitengane......

  Kelele za kinafiki za kina jussa wakati uwezo wa kujitoa kwenye muungano wanao tumezichoka........
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,430
  Likes Received: 19,754
  Trophy Points: 280
  mimi ni mtanganyika-mwamunyange(askari)
   
 9. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Wazanzibar mbona ni rahisi sana kujitoa kwenye Muungano,Fungeni virago nyote mlio Bara , nikimaanisha waPemba wote na waUnguja , viongozi wenu walio Bara, Makamu wa Rais, wafanya bihashara wote , wabunge wa Jamhuri mtokomee kisiwani alafu mseme hayo ya mikataba yenu , muone kama kuna mtu atawafuata huko.
  Tumewachoka na chokochoko zenu hamna lolote.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..lakini Jussa alikuwa mbunge ktk bunge la muungano na hakupata kutamka maneno hayo.

  ..zaidi, ni mjumbe wa baraza la wawakilishi na hajawahi kuwasilisha hoja kutaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili.

  ..walikuwa na nafasi nyingine adhimu kabisa ya kuweka shinikizo kwamba suala la aina ya muungano liamuliwe kabla ya kuanza majadiliano ya katiba ya muungano wa Tanzania.

  ..well, sasa tuone basi kama kuna mbunge yeyote yule toka Zanzibar atakayetoa kauli za namna hiyo katika bunge la muungano.
   
 11. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Tatizo la jusa ni mwoga anaongea kwa kujifichaficha atamke tu kuwa mungano hautaki.
   
 12. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Ngoma ikilia saaana mwishowe hupasuka. Ila tu mimi ninachoshangaa ni kwamba, binafsi sioni umuhimu wa muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa nini tusiuvunje tuu!!!??? Mbona kuna vijinchi kama Rwanda na Burundi vidogo kwa eneo, rasilimali hata uchache wa watu, lakini raia wapo na wanaishi. Hivi kweli bara tukiwaacha wazanzibar wakaunda dola yao huru wabara tutadhurika na nini??? Tatizo hasa ni nini hapo??? Kwani ni lazima tufuate kila kitu kama alivyotaka Nyerere???
   
 13. m

  malaka JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamni mbona mwanitaja au ndio mnataka kunilimboka? Mamlakab au malaka?
   
 14. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  lakini kwanini mnalazimisha kuwabeba wazenji? na nyinyi si mfunguke tu bungeni kwenu kule mseme tumechoka kubeba wazenji. hawa jamaa msiwalaumu serikali hii ya chama hiki itafikia wakati hata arusha, mwanza, kigoma, mbeya, songea kila corner watasema wanataka kumeguka. after 50yrs hatuna prospective yyt. tunaishi kama samaki, future yako ni kumla mwenzako
   
 15. a

  abousalah2 Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ******* nani? Acha jazba khanisi weee! Toka apa umelewa nini au shauri ya kiti moto
   
 16. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kujifanya want aka Muungano aw Mkataba ni first step ya kijanja wagawe Jamhuri ya Tanzania, aliwashauri Mlezi na Mwanzilishi aw Uamsho Amani Abeid Karume kuwa tutoke pole pole .
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Can someone have the guts to tell these sons of #$%$#* to go to hell?
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha Muungano wa Mkataba, huyo kilaza Jussa na hao wawakilishi wenzake mbona hatuwasikii ndani ya BLW na mbona hatuwasikii ndani ya Bunge la Muungano? Huo mkataba si lolote zaidi ya udanganyifu katika kutafuta njia ya kuendelea kupakatwa na kujinufaisha na rasilimali za Tanzania bara kupitia mlango wa uani. Na kwa ufahamisho zaidi, jina Tanzania halitafutika hata wakijiondoa...jina India halikufutika Pakistani ilipojiondoa na baadaye halikufutika Bangladeshi ilipojiondoa, Ethiopia haikufutika Eritrea ilipojiondoa sasa kwa nini Tanzania ifutike kwa sababu tu tuvisiwa ambavyo wakazi wake hawafiki hata asilimia tano (<5%) ya Watanzania ikijiondoa? Wafungashe tu waondoke...Me? I definitely wont miss them, it is just good riddance!
   
 19. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Muungano wa mkataba si muungano wa nchi mbili bali ni ushirikiano wa nchi mbili. Wanaweka pale neno muungano badala ya shirikisho kupamba tu mchakato wa kuvunja muungano. Ili kupata "muungano" wa mkataba (borrowed word) sharti la kwanza ni kuvunja muungano Tz na Zbar kila moja iwe sovereign state kama tulivyo hivi sasa na nchi zingine kama Malawi, Kenya, nk. na ni baada ya hapo Tz na Zbar zitaamua kama kuna haja (maslahi) kuingia "muungano wa mkataba" na kama mbele ya viongozi wataona hakuna sababu ya mkataba huo basi muungano utakuwa umekufa na mkataba pia unakufa (unabaki wa kufikiriwa). Kwa maoni yangu seriously hakuna kitu kama "muungano wa mkataba" bali ni nchi moja kuingia mkataba na nchi nyingine. Haya ni maneno yanayoiumika kisiasa kuhadaa wanaoutaka muungano waingie ndani ya mtego kilaini. Utangulizi wa Kakke hapo juu unathibitisha maoni yangu.
   
 20. n

  ndovu New Member

  #20
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]TUNATAKA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI KITAIFA NA KIMATAIFA ITAKAYOFUATIWA NA MUUNGANO WA MKATABA KATI YAKE NA JAMHURI YA TANGANYIKA
  Muungano wa Mkataba maana yake nini?
  Muungano wa Mkataba ni MASHIRIKIANO kati ya nchi mbili au zaidi ambazo kila moja huwa inabaki na mamlaka yake kamili ya KIDOLA kitaifa na kimataifa lakini vado zikawa zina mashirikiano katika maeneo maalum zitakazoamua kushirikiana, mahusiano ambayo huwa yanaongozwa na Mkataba.
  Muungano wa Mkataba ni tofauti kabisa na Muungano wa Kikatiba ambao huwa unamaanisha kuwepo kwa Serikali ya Muungano inayosimamia mambo ya Muungano. Katika Muungano wa Mkataba, kila nchi hubaki na Serikali yake kamili yenye kusimamia mambo yote. Yale maeneo ya USHIRIKIANO husimamiwa kupitia ama KAMISHENI YA PAMOJA au KAMATI YA PAMOJA kwa kadiri makubaliano yatakavyokuwa yamewekwa kwenye Mkataba.
  Ni zipi faida za Muungano wa Mkataba:
  1. Hakuna khofu ya nchi moja kuimeza au kuitawalia nchi nyengine.
  2. Kila nchi inabaki na uhuru na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kuamua mambo yake.
  3. Kila nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katika jambo lolote ililoamua mwanzo kushirikiana pale inapoona hakuna maslahi au faida kuendelea nalo.
  4. Huvutia nchi nyingi kuingia katika Muungano wa aina hiyo kwa sababu hakuna khofu ya kupoteza mamlaka au kupunguziwa madaraka au mambo yake kuamuliwa na nchi nyengine.
  5. Mahusiano huwa ni ya kirafiki na ya ujirani mwema yanayopelekea kuaminiana na kuondoa kutiliana shaka kusikokwisha.
  Zanzibar iwe na mamlaka yepi kitaifa na kimataifa katika Muungano wa Mkataba?
  1. Iwe na Serikali kamili yenye Wizara zote ikiwemo Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani na Ulinzi.
  2. Iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa na pia uanachama wa Jumuiya zote za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Nchi za Bahari ya Hindi.
  3. Iwe na Benki Kuu yake na Sarafu yake.
  4. Iwe na mamlaka yote ya kuamua serĂ¡ za fedha na uchumi, kodi na sarafu.
  5. Iwe na Uraia wake.
  6. Iwe na Paspoti yake na kusimamia Uhamiaji katika nchi yake.
  7. Idhibiti Anga yake na Usafiri wa Anga yenyewe.
  8. Isimamie Elimu ya Juu yenyewe na kuamua Mitihani gani itumie katika masomo.
  9. Isimamie na inufaike na rasilimali zake zote za ardhini na baharini ikiwemo mafuta na gesi asilia.
  10. Idhibiti yenyewe eneo la mipaka ya Bahari Kuu (EEZ) katika eneo lote inalopakana nalo.
  11. Idhibiti mamlaka mengine yote yanayokuwa yanamilikiwa n anchi kamili.
  Ni ipi Mifano ya Muungano wa Mkataba?
  - Muungano wa Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.
  - Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye wanachama 5 mpaka sasa.
  - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS)
   
Loading...