Jussa na Seif mnawachelewesha Wazanzibari kuwa "huru kamili"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jussa na Seif mnawachelewesha Wazanzibari kuwa "huru kamili"!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Seif Sharrif na Jussa wasikie vizuri sana;tupo ambao hatutaki Muungano "wa mkataba"! Kama wao na wale wanaowashabikia wanaona kweli Tanganyika inawanyonya na wanataka uhuru kamili njia iko rahisi kabisa.

  Wawaondoe wabunge wao kwenye Bunge la Muungano; waitishe kampeni ya Wazanzibari wanaotumikia serikali ya Muungano kuachia nafasi zao (akiwemo Ghaib Bilal) na wajitangazie "uhuru wao".

  Lakini la kwanza ni kwa yeye (Seif) kuacha ziara za kisiasa Tanzania bara na kuamua kuvunja CUF ili chama cha siasa cha Wazanzibari watupu kizaliwe.

  Hapo ndio tutajua kweli wanataka kuwa huru. Watoke kwanza wawe na Zanzibari yao halafu ndio watuulize kama tunataka Muungano wowote na wao! Siyo watoke halafu wakati huo huo waamue aina ya mkataba wanaoutaka wao!


  LET ZANZIBAR GO!
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umenena ukweli mtupu, kwa sababu haiwezekani Jussa kutudanganya kuwa amejiuzulu nafasi ya ukatibu wa CUF kwa lengo la kutetea na kusimamia muungano wa mkataba wakati huo huo anaendelea kuwa mjumbe katika baraza la uwakilishi bara! Waachie nyadhifa zao zote ndani ya muungano ndipo wadai Z'bar huru wao nao wakiwa huru!
   
 3. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Muungano upo kwa maslahi ya ccm bara...ccm zanzibar hakuna muungano bali kuna sisi wazanzibar na wao watanganyika
   
 4. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatuwahitaji wazanzanzibari wala hatuwalazimishi wawepo katika muungano.

  Kama wanataka tuendelee na muungano basi kuwe na serikali moja ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na zanzibar iwe ni mkoa katika jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  Mipango ya Maendeleo ipangwe kwa usawa kutokana na uwiano wa watu bila kujali umetoka katika sehemu gani ya Jamhuri.

  Vinginevyo wana uhuru wa kujiondoa na kujiamulia mambo yao wenyewe. Hatutawafukuza.

  Wanasiasa wanaotoa wazo la serikali tatu ni wabinafsi wenye uchu wa madaraka. wanataka serikali tatu ili wapate vyeo vya kisiasa.
   
 5. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu mwanakjj umenena. kwani muungano kitu gani bhana. miungano yote iliyoingiwa kidwanzi km wetu ilishavunjika. why not ours?

  wazanzibari, its very easy fuateni ushauri wa mwanakjj muwe huru. km mseto mliamua wenyewe bila shuruti toka kokote kule, na hili pia mwaliweza wenyewe. ni uamuzi wenu tu.
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mzee mwanakijiji umenena ukweli m2pu sina cha kuongezea
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  ka nchi kadogo,hakana maliasili yoyote(hata sungura pori hawana),kama maji ya bahari tunayo hadi mtwara..let them go,tired of their nuisance!!!
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  MM, wanataka ZNZ huru wakiwa na 'strings attached' yaani muungano wa mkataba.
  Hapo ndipo ninaposema Maalim na Jusa wanauma maneno na sijui kama Wazanzibar wanjua nini wanataka.

  Jusa ni mbunge, kwa vile amejiuzulu uongozi wa CUF ili kuimarisha juhudi za ZNZ huru anapaswa pia ajiuzulu ubunge katika bunge la JMT. Akiendelea kuwa mbunge atakuwa anatafuna si maneno bali matapishi.

  Maalim Seif hatakiwi kuja Tanganyika katika mikutano ya kisiasa. Kwa kauli ya ujirani mwema kama Kenya, nasi tunataka ujirani mwema hivyo siasa za CUF mwisho Chumbe. Kama ataendelea kuja katika mikutano, kwanza apuuzwe kwasababu anaongea sichokiamini na watu wasiomhusu. Pili atakuwa amekula matapishi achilia mbali kujiuma uma.

  Maalimu Seif na Jusa wavunje kwanza CUF ili wawe na vyama huru vya kizanzibar halafu wavunje muungano. Kama hawawezi kuvunja CUF, wafunge midomo na kukaa kimya kwasababu wanakula matapishi yao na si kujiuma uma.

  Wamwite Gharibu na wafanyakazi wote wa muungano kutoka ZNZ, watengeneze Passport za ZNZ haraka haraka na watumie Rupee au dollar kama hatua za kuvunja muungano. Wasipofanya hivyo basi wakipanda katika majukwa waiteni manafiki, vizabi zabina, warongo na wahuni.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Jussa and Maalimu Seif...two confused minds. Naona mmoja anataka kuwa Rais wa Zanzibar mpya na mwingine sijui anataka kuwa nani.
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Maalim Seif ni katibu mkuu wa CUF Tanzania, na sio Zanzibar.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Week iliyopita Maalif Seif alikuja Arusha kwa ndege/gharama za Tanganyika na kuwaambia vijana wanalewa viroba. Jana alikuwa Pemba (ulinzi kwa gharama ya Tanganyika) kuhutubia ni jinsi gani anataka Zanzibar huru na kuachana na koloni Tanganyika. Kesho Jumanne tunaambiwa atakuwa Bukoba (Tanganyika).

  Hivi Maalim Seif anaamini anachosema? Afuatafuata nini Tanganyika? Kwanini asikae chini na kuandaa muswada wa kuachana na koloni? Chama chake (CUF) kina wabunge wengi toka toka Zanzibar kwenye bunge la Muungano, asiwapoge marufuku kuja Dodoma?
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu so far sijasikia sababu yeyote ya msingi kutoka kwa Seif Sharif Hamad kuhusu kuvunja Muungano. Ninachoona ni kuwa anataka madaraka tu, anataka awe rais wa Zanzibar halafu awe sultani wa Pemba.

  Siku zote anadhani watu wote ni wajinga, na kibaya zaidi anadhani kila mtu anamsikiliza.

  Kama kweli yuko serious atenganishe CUF bara na CUF visiwani, na ajitoe kwenye serikali ya muungano kwa kuwa inaifuniza ile ya Zanzibar aanzishe movement ya kuwaondoa wazanzibar wote toka bara na kuwapeleka Zenjibar, hapo tutajua kuwa yuko serious.
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nimekugongea like... Hawa wanatafuta tu umaarufu kuelekea 2015... Hawana la maana.
   
 14. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  MKUU MMJ, heshima mbele. Naona umeishiwa hoja, hujui hata ulisemalo. Unapapatika tu, kijiba cha roho kimekukaa. Haaa haa haa.
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Utashangaa Mtikila wanamfungulia kesi za uchochezi, gazeti la Mwanahalisi likafungiwa kwa uchochezi, wananchi wengi tu wanazo kesi eti ni uchochezi lakini hawa akina Jussa, Seif na wengineo haya wayafanyayo sio uchochezi.

  Labda tuseme tafsiri ya sheria zetu ina rangi na dini, lakini kama haina basi hawa jamaa wana kesi zaidi ya moja ya kujibu.

  Binafsi nimefika mahali sipendi aina yoyote ya muungano kati ya Tanganyika na hawa wazenj, labda ushirikiano kama tulivyo nao na Kenya, Uganda na Rwanda ila sio zaidi ya hapo.
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  let zanzibar go !!!!!
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi, tusisahau kuwa sera za CUF ni serikali 3. Sera za Jusa na Seif ni mkataba.
  Seif alikuwa arusha anaimarisha CUF na yupo njiani kwenda Bukoba kwa mikutano ya kisiasa.
  Swali ni je anakwenda kuhutubia mikutano kuhusu nini ikiwa yeye haamini katika sera za chama anachokitumikia?

  Je, ujirani mwema anoutaka ni upi huo ikiwa bado anakuja kueneza sera za CUF huru kwa 'wakoloni'?
  Huo mkataba anaosema ni upi zaidi ya mkataba tulio nao?

  Kwanini asiwazuie wabunge wa ZNZ kuhudhuria bungeni, kuwataka wajumbe 15 wa tume ya katiba wajitoe na watumishi wa SMZ ikiwa ni pamoja na wanafunzi warudi kwanza ZNZ kudai nchi huru kabla hawajaomba kujiunga na si muungano na Tanganyika?

  Maalimu anauma maneno, anakula matapishi halafu anawafanya WZNZ kama maliwato!
  Huyu ni mnafiki sana, anataka ZNZ huru akiwa anapata mafao kutoka hazina Dar es Salaam!
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  jussa na wenzie wanataka madaraka tu........... hakuna cha zaidi, bahati mbaya kwa chuki walizonazo wazanzibari zimewafumba mambo kuona lengo halisi la jussa na seif, lakini ndo heri yetu watanganyika, hatutaki muungano wala mkataba waende.....kuvuja kwa pakacha...   
 19. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapa mkuu umegonga msumari wa moto kwenye kidonda wataweza kujiondoa na kuacha asali na maziwa wanayo kunywa sasa hivi?
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Mungu (kama kweli yupo) alishatutenga kwa bahari sijui sisi tunang'ang'anizwa nini na huu muungano
   
Loading...