Jussa: Mkoloni Tanganyika hawezi kuacha Zanzibar ichimbe mafuta yake

Balagha

Member
Oct 8, 2016
21
17
Ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook haya:

KISIWANDUI IMEITIKA JINA

Katika SURA AT-TAUBAH, aya ya 119, Allah ametuusia tumche Mwenyezi Mungu na tuwe pamoja na watu wakweli. Wasia huu hautaki ufafanunuzi kwa sababu maisha yanasherehesha tafsiri na sababu za wasia huo.

Watu wasipokuwa wakweli wataanza kudanganya watu lakini wakishtadi katika upotofu huo huanza kujidanganya wenyewe na kuwataka watu sasa waamini uongo wao. Haya ndio yanayojitokeza kwa uwazi katika utawala wa sasa wa Kisiwandui. Kujidanganya na kutaka watu waamini uongo wao.

Mswada uliopitishwa hivi karibuni na Baraza lisilo na Wawakilishi umezaa kioja cha ajabu na Mwenyekiti wa Wenyeviti Bwana Hamza Hassan Juma akiamini ana hoja timamu ya kutungua hata roketi ikiwa angani alisema kwa kinywa kipana hoja zumbukuku hoja tatu za kituko.

Hapa tunaangazia kwa ufupi hoja zake hizo na kutoa majibu kwa ufupi.

a) Hoja ya Baraza la Wawakilishi Kuidhinishwa Kutunga Sheria ya Mafuta ya Zanzibar.

Alisema kuwa Bunge la JMT kwa kutumia mamlaka yake ya kutunga sheria za Muungano limeidhinisha Baraza la Wawakilishi kutunga sheria ya mafuta ya Zanzibar. Alisema haya kwa kinywa kipana, kadamnasi akiwa live katika redio Swahiba FM.

Majibu aliyopewa yaliakisi hoja pofu na potofu aliyotoa. Kwanza ni kanuni ya Sheria yoyote duniani kuwa Sheria haiwezi kukasimu mamlaka ya kutunga sheria nyengine. Sheria siku zote inakasimu uwezo wa kutunga kanuni yaani sheria ya kukasimiwa (delegated legislation). Bwana Hamza hakuweza kujibu hoja hiyo kwamba hivi kwa kuruhusiwa na Bunge, vipi Baraza litatunga Sheria? Baraza litakuwa limetunga Kanuni. Hoja hiyo pia iliambatana na ile ya masharti ya Ibara ya 64 ya Katiba ya JMT inayosema kwamba endapo Baraza la Wawakilishi litatunga sheria kwa jambo ambalo limo mikononi mwa Bunge, Sheria hiyo itatenguka. Wanasheria wanapenda kusema “void ab initio”…yaani hii ni sawa na noti feki, batil tokea nasabu yake, batili tokea mimba yake illipotungwa…batil zaidi ya haram. Mnajua majibu ya Hamza? .. Mhh yanachekesha. Anasema mbona sisi Zanzibar tumeshazoea kuvunja Katiba na hakijatokea chochote???

Majibu ya ziada aliyopewa ni kuwa hata hiyo sheria ya Bara mloisoma kinyumenyume mbona haijawapa mamlaka ya kutunga sheria ya mafuta mbona haijasema hivyo? Akauliza kwa sauti ya chini imesemaje??? Akajibiwa kakaeni muisome tena labda mlipoisoma mwanzo mlihadaliwa na gilligilani ya siasa na kicheko cha wizi cha Kikwete na maneno ya kifedhuli ya Magufuli... mkadhani mmepata kumbe mmepandwa mgongoni!!! Sheria ya Mkoloni inasema hivi:

“2. This Act shall, subject to subsection (2) apply to Mainland Tanzania as well as Tanzania Zanzibar-

(2) The regulation of petroleum upstream operations, midstream and downstream activities and matters incidental thereto to which this Act apply shall-

(a) where such operations or activities are undertaken within Mainland Tanzania, be governed and administered by institutions established or referred to under this Act; and

(b) where such operations or activities are undertaken within Tanzania Zanzibar, be governed and administered by institutions in accordance with the laws of Tanzania Zanzibar.

Sheria ya Mkoloni inasema wazi kuwa Sheria itayotumika ni moja tu nayo ni ile ya Mkoloni. Zanzibar inachoruhusiwa ni “devolution” katika kuisimamia tu sheria hiyo ya Mkoloni, sio kutunga ya kwake.

Mkoloni hajafanya hivyo kwa bahati mbaya. Ni kwa kuidhibiti sekta hii. Kwani mamlaka ya kugawa vitalu yanabaki kwa Waziri wa Mkoloni na hata mamlaka ya kutangaza eneo la utafiti yanabaki kwao.

b) Hoja ya Mipaka

Bwana Hamza anasema kuwa wamepitisha sheria ili wapate nguvu ya kudai mipaka kwani mipaka ni katika mambo madogo madogo ya kushughulikiwa baadae.

Alipewa majibu ya kina kwamba kwanza hoja ya mipaka ndio ilokwamisha suala la jambo hili kutolewa katika Muungano na Mkoloni ndio mana amesubiri mpaka Zanzibar walipoingia vipofu ndio akawadanganya kuwa kawaruhusu kumbe anawadhibiti zaidi.

Kwanza, Mkoloni ameshakivamia rasmi kisiwa cha Fungu Mbaraka ambacho ni cha Zanzibar kabla hata Mkoloni hajazaliwa. Na ametangaza hata katika makongamano ya kimataifa pale Chatham House, tarehe 26 Februari, 2013.

Pili, Mkoloni anadai kuwa katika kugawa mipaka itumike kanuni ya equidistance line. Hii ni hoja ya kichekesho lakini Mkoloni wetu hana haya. Kanuni hiyo haiwezi kutumika kwa sababu mpaka wetu wa kaskazini baina ya Tanganyika na Zanzibar ndio huo huo wa Kenya na Tanzania ambao umetumia mfumo wa “parallel of latitude”. Aidha, kwa upande wa Kusini Zanzibar haina mpka wa nchi kavu na Tanganyika, hivyo kinachoangaliwa ni wapi territorial waters za Zanzibar zimeishia kwa upande wa Kusini. Bila shaka ndio maana Mkoloni anadai Latham kwa sababu itaipunguzia Zanzibar urefu wa kilomita 60 ndani ya Bahari. Watu wetu wa Kisiwandui hata hilo hawalioni? Wanacheza siasa katika uwepo wa nchi???
 
Mafuta hayo ni mafuta gani?. Mafuta ya kujaa kwenye kinibu?!.
Watu hawana hata Shukrani tumewatenda wema kiasi gani, badala ya kushukuru ndio kwanza unaitwa mkoloni.
Ama Kweli Shukrani ya punda mateke, fadhila mfadhili mbuzi angalau utauonja mchuzi!, binaadamu atakutupa!
Pasco
 
Labda mafuta ya nazi
Jussa uwakilishi wake upo face book.Asante sefu kwa kulazimisha vikaragosi vyako visuse
 
Labda mafuta ya nazi
Jussa uwakilishi wake upo face book.Asante sefu kwa kulazimisha vikaragosi vyako visuse
Makamanda mbona mnamshambulia ushirika wenu? au kwa kuwa hakuzungumzia mambo ya Ukawa?
 
FB_IMG_1476560931977.jpg
Issue ya mafuta ya kwenye kinibu tumeizungumza sana humu,
Tatizo ni chako changu, chako chetu, lakini likija suala la changu, sio tena changu chetu au changu chako bali changu changu

Pasco

Usiwe miongoni mwa wale ambao kila watanzania wanne basi lazima mmoja atakuwa yumo!!!!!!!

Wazanzibari waliowengi linapokuja suala la muungano wa Tanzania wanakuwa wako straight kuwa hawana shida nao na wako tayari hata leo ukatikie mbali.

Hayo mafuta kwenye kinibu kwa udogo wao yanawatosha sana tatizo linakuja kwenu mnaoendelea kujazana mijini na vijijini.

Na nikitugani hasa mnachotoa kuwapa wazanzibar ikiwa nyinyi wenyewe Hakuna kimoja kinachowatosha!!!! Njaa hadi kwenye vidole.

MWISHO hayo maneno hakuyasema Jussa kama jussa bali yeye karipoti majadiliano yaliyofanyika Kati ya MSOMI MWENYE KUIJUA TAALUMA YAKE OTHMANI MASOUD aliekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar hadi pale alipofukuzwa kwa kuitetea Zanzibar katika bunge la katiba dhidi ya BORA TUMBO WA CCM Hamza Hassan Juma
 
MWISHO hayo maneno hakuyasema Jussa kama jussa bali yeye karipoti majadiliano yaliyofanyika Kati ya MSOMI MWENYE KUIJUA TAALUMA YAKE OTHMANI MASOUD aliekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar hadi pale alipofukuzwa kwa kuitetea Zanzibar katika bunge la katiba dhidi ya BORA TUMBO WA CCM Hamza Hassan Juma
Kama ni huyu aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Othman Masoud, soma hapa ushauri wangu kwa Dr. Shein. Angalia tarehe ya thread hii na angalia ni lini alitimuliwa.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...anM7KUfMPWZ4r0i4w&sig2=03VHd762ajfUhHlMlDXXKA
Pasco
 
Hizi hoja zumbukuku alizo zizungumzia nyingi hutoka kwa wakazi wa mtaa wa Lumumba.
Kingine Tanganyika tuna wapekekesha hawa wakazi wa mkoa wa zanzibar... Tuwaache tu wafanye yao.
 
Mafuta hayo ni mafuta gani?. Mafuta ya kujaa kwenye kinibu?!.
Watu hawana hata Shukrani tumewatenda wema kiasi gani, badala ya kushukuru ndio kwanza unaitwa mkoloni.
Ama Kweli Shukrani ya punda mateke, fadhila mfadhili mbuzi angalau utauonja mchuzi!, binaadamu atakutupa!
Pasco
Mkuu siku hizi umekuwa ukijibu hoja kwa staili tofauti sana.
Jaribu kutulia unapozipangua hoja kama zamani
 
Ccm kisiwandui wamepatwa tena kama ule utafiti wa vichaa wakifanyiwa basi watakua 3 kwa 4 ni machizi. Mtu mwenye akili timamu hukubali kuachia mafuta na gas wachimbe wengine....lazima hawa jamaa punguwani
 
Wa Africa kweli mmezidi kw upunguani mtu anaongelea issue tena kw kunukuu vpengele vya sheria nyinyi baada yakuvunja hoja kw kuleta vpengele vngine mnajtutumua kuporomosha mutuc hivi inakusaidieni? hebu kueni na akili hata kidogo wa Africa mnatia aibu sana yaani
 
Kila siku nawambia watu humu Chadema hawana kheri na CUF mnabisha wasomeni pro-Chadema/UKAWA wanavyomshambilia kiongozi wa CUF kisa kudai haki yao Wazanzibar.
 
Back
Top Bottom