Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
Raisi Jakaya Kikwete amehitimisha uteuzi wa wabunge 10 wa kuteuliwa na rais kwa kumteua Bw. Ismail Jussa Ladhu, wa CUF na Janet Mbene wa CCM kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huu, umetangazwa live jioni hii bungeni mjini Dodoma, na Spika wa Bunge, Mhe. Samweli Sitta wakati akikamilisha mjadala wa Richmond.
Jussa ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF na msungumzaji mzuri kwenye medani za media. Janet Mbene ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Masaki kwa tiketi ya CCM, na huku ndiko ziliko nyumba za waheshimiwa mawaziri na wenzetu waliojaliwa neema.
Wabunge hawa, wataapishwa kesho Bungeni Dodoma.