Jussa alitikisa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jussa alitikisa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Feb 13, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Feb 13, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  • Sitta amsifu JK kumteua mbunge makini

  na Hellen Ngoromera, Dodoma

  MBUNGE wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CUF), jana ameingia bungeni kwa kishindo baada ya kuzungumza kwa mara ya kwanza akionya kuwa suala la mgombea binafsi si hiari ya serikali bali ni uamuzi halali wa Mahakama Kuu hivyo serikali inatakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kulitekeleza. Jussa alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za uchaguzi wa mwaka 2009 uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Philip Marmo.

  Alisema hivi karibuni Jaji Mkuu Augustino Ramadhan akishirikiana na jopo la majaji kutoa kauli kuwa suala la mgombea binafsi ni halali kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo suala la serikali kupeleka rufani ya mgombea binafsi Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji Mkuu na jopo lake haileti taswira nzuri katika utawala wa mihimili mitatu ya dola ambayo ni mahakama, Bunge na serikali.

  ‘Mheshimiwa Spika nimepata shida kidogo baada ya kusikia maneno ya Naibu Mwanasheria Mkuu kuhusu suala hili kwani maelezo yake yalikuwa ya utatanishi,’ alisema Jussa.

  Alisema mahakama inapaswa kuheshimiwa kama ilivyo kwa Bunge hivyo hatua zozote za serikali kutaka kupindisha mambo na kuminya haki za msingi za Mtanzania haziwezi kuvumiliwa.

  Jussa alisema sehemu kubwa ya muswada huo imezungumza mambo ya juujuu na kwamba kuletwa kwake muda mfupi kabla ya uchaguzi, hakuleti sura nzuri.

  ‘Muswada huu una upungufu mkubwa sana, ungezingatia mambo mengi ikiwemo utendaji wa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi kwani suala hili halijaguswa,’ alisema Jussa.

  Akizungumzia kuhusu uteuzi wake, Jussa alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kufanya kitu cha kihistoria na anaamini kuwa amefanya hivyo kuyaletea nguvu maridhiano yaliyofikiwa kati ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na Rais wa Zanzibar Aman Abeid Karume.

  “Mheshimiwa Spika kabla sijatoa hoja yangu napenda kumshukuru mheshimiwa rais kwa hatua yake hii ya kihistoria kuniteua kuwa mbunge.

  “Awali sikuwa na taarifa kuhusu hili, lilipotangazwa hili, kuna mtu alinichokoza na kuniambia kuwa unaenda bungeni wakati ikiwa imesalia miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu kwa hiyo utaipeleka ile hoja yako uliyoitoa katika Baraza la Wawakilishi, nami nataka kusema kuwa sikusudii kuileta hoja hiyo hapa niliipeleka kule kutokana na uhalisia wake,’ alisema Jussa.

  Jussa aliitaka serikali kupunguza ukaidi kwa baadhi ya mambo na isikilize hoja zinazotolewa na kambi ya upinzani katika kurekebisha kasoro mbalimbali zinazotolewa ili nchi iweze kupiga hatua.

  Baada ya kumaliza kutoa mchango wake, Spika Samuel Sitta alimsifu Jussa kwa kuchangia hoja yake vizuri na kusema kuwa hakika rais anajua kuteua.

  Kwa mujibu wa Spika pamoja na ugeni wake, Jussa amepangilia vyema hoja zake na kuziwasilisha inavyotakiwa na kusema kuwa hali hiyo inaashiria mambo mazuri.

  Akijibu hoja mbalimbali, Waziri Marmo alisema suala la mgombea binafsi ni hoja nzito na kwamba si ya kupuuza kwani inagusa Katiba.

  Alisema kwa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu suala hilo si rahisi kushughulikiwa kwa sasa kwani linahitaji marekebisho mbalimbali yakiwemo marekebisho ya kisheria.

  ‘Mheshimiwa Spika suala la mgombea binafsi ni zito na linagusa katiba hivyo kwa kuwa muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu ni mdogo sio rahisi suala hili kushughulikiwa kwa sasa kwani linahitaji mchakato mzima wa kubadilisha sheria zetu,” alisema Marmo.


  Angalau Jussa ameanza vizuri...naamini tafanya vizuri zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha kulitumikia Bunge na wananchi.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Jussa is making sense than most of CCM long serving MPs
   
 3. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu ndio mbunge,siku moja tu kaanza kuchangia,sio wengine miaka 4,wala atujasikia sauti yake.Hongera Jussa.
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,931
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  mbunge mmoja wa upinzani sawa sawa na wabunge 10 wa ccm.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Hii hoja ya mgombea binafsi wala sio ngeni, imejadiliwa muda mrefu na kesi mpaka sasa ipo mahakamani, sasa huyu Jussa kalitikisaje Bunge na hoja hiyo? Amerudia rudia yale yale ya siku nyingi! Au kipya kinyemi ingawa kidonda? Muwe makini na vichwa vya habari!
   
 6. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 531
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dr amani walid kaborou alianza hivihivi sasa hivi hatunaye
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Wapo wengine akina Zitto Zuberi Kabwe, Dkt Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Augustine Lyatonga Mrema, etc ambao walivuma sana hata wengine magari yao yalisukumwa na mashabiki! Kwenye siasa ni kupanda na kushuka, acha mchezo bwana!
   
 8. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 429
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Acha (usisiemu) Hata kama amerudia kajitahidi sana kulifafanua jambo hili hasa ukizingatia kuwa ni mgeni. na hicho kichwa ni sahihi kabisa Jussa kalitikisa Bunge
   
 9. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 370
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  are you sure?lets be realistic in our comments
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa tena sio wabunge 10 ni wabunge 20..Ni ratio ya 1:20
  Rejea waliotaoa ripoti ya vinara wa ucgangiaji bungeni...Upinzani uliongoza.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Si ndio nikasema ugeni wake bungeni ndio "kipya kinyemi ingawa kidonda?" Hata JK alipolihubiria Bunge kwa mara ya kwanza, 2005 tuliona kweli "kazi imepata mtu na sio mtu kapata kazi!" Baada ya muda alianza kutoa kauli za kuboa za "ukitaka kula lazima uliwe!"
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...