Junior Kasanga na raia wa China, wakamatwa wakitorosha dhahabu waliyochimba

Wafanyabishara wasishurutiswe, waongeleshwe ka upole....! Kazi na iendelee!
Wasukuma mnatapatapa tu shenzi nyinyi,,
Dikteta magufuli siyalikamatwaga madini kule Mwanza ya billion Tatu,,

Mwisho wa siku akatoa amri yaachiwe baada ya kupewa mgao
 
MAIGIZO YATAISHA LINI?
JUNIOR KASANGA HUO MGODI NI WAKE. KACHIMBA KAPATA DHAHABU 2.6 kg NYIE MNALAZIMISHA AWAUZIE NYIE! MUACHE AKAUZE PANAPOFAA.

HUYO SIO LAIZER MLIYEMDHULUMU!
 
viongozi wengine jifunzeni kwa DC wa Ulanga na Jeshi la polisi wilaya ya Ulanga.
Hakika DC wa Ulanga na Jeshi la polisi wilaya ya Ulanga ni mfano mzuri wa kuigwa.
Pongezi nyingi kwao, Mmeonyesha na kuthibitisha kwa taifa kuwa nyinyi ni wazalendo wa kweli kwa taifa lenu.
wote mlio pambana mmeingia ktk kumbukumbu za Taifa ya kuwa wazalendo wa kweli kwa Taifa la Tanzania.
Kazi iendelee.......
 
Wasukuma mnatapatapa tu shenzi nyinyi,,
Dikteta magufuli siyalikamatwaga madini kule Mwanza ya billion Tatu,,

Mwisho wa siku akatoa amri yaachiwe baada ya kupewa mgao
Usukuma wa huyo jamaa ulomquote umeutambuaje? au kila mtu uliye na chuki nae unamwita msukuma!
 
Siku Mtanzania atakaposhikwa Uchina akitorosha madini ndipo mtakapojua Mchina ni Mzungu au Muhindi
 
MAIGIZO YATAISHA LINI?
JUNIOR KASANGA HUO MGODI NI WAKE. KACHIMBA KAPATA DHAHABU 2.6 kg NYIE MNALAZIMISHA AWAUZIE NYIE! MUACHE AKAUZE PANAPOFAA.

HUYO SIO LAIZER MLIYEMDHULUMU!
Wewe tulia, Kuna taratibu za usafirishaji wa madini hata kama umeyachimba sebuleni kwako huwezi kuyapeleka hata distance ya mita 500 bila kupata Kibali maalum cha usafirishaji. Hao walikuwa wanasafirisha kiholela na kwa kwa tafsiri ya sheria zilizopo ni utoroshaji, period.
 
Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngolo Malenya na kamati yake ya usalama wamemkamata mwekezaji Mtanzania Junior Kasanga akishirikiana na watu wengine wakiwemo raia kutoka nchini China wakitorosha madini ya dhahabu waliyochimba kwenye mgodi uliopo kijiji cha Isyanga wilayani humo.

--
Serikali wilayani Ulanga mkoani Morogoro imewakamata watu saba akiwemo mwekezaji mzawa Junior Kasanga na raia wawili wa China kwa tuhuma za kutorosha madini ya dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 337.5 kutoka katika mgodi uliopo kijiji cha Isyanga wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngolo Malenya, amesema kuwa dhahabu iliyokamatwa ina uzito wa gramu 2,640 sawa na kilogramu 2.64 ambapo amebainisha serikali bado inaendelea kuwafuatilia wawekezaji wengine ambao wamekuwa na tabia ya kutorosha madini na kusababisha kupotea kwa mapato ya serikali.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Migodi wilaya ya Ulanga, Edward Ngulinja, ameeleza awali wawekezaji hao walifika katika ofisi ya madini ya wilaya hiyo kwa ajili ya taratibu za kisheria ndipo walipo watiliashaka kuwa kuna udanganyifu wanafanya na kuvitaarifu vyombo vya ulinzi na usalama.

Ni muwekezaji✔️
Ana leseni✔️
Madini alichimba mwenyewe✔️
Alienda mwenyewe ofisi ya madini kulipa mlabaha na kupewa rakili✔️

Naomba sasa wajuvi mnijuze: definition ya kutorosha ikoje, nisaidieni ndugu zangu nisijepatwa na janga hili maana nina kitalu hapa Morogoro, naandaaa zana nianze kuchimba
 
Back
Top Bottom