Jumuiya za Kiraia, vijiwe vya wasomi na njaa ya Watz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya za Kiraia, vijiwe vya wasomi na njaa ya Watz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mgoyangi, Nov 27, 2008.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Nov 27, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Najaribu kupitia makala mbali mbali zinzohusu, Jumuia za Kiraia Tanzania ikiwa ni pamoja na NGO, nakuta lawama kuwa, hivi ni vijiwe vya wasomi wanajipachika huko kupata ajira na kuganga njaa, na kisha kujipachika majina kama Wanaharakati, wakati Mwingine Marais.

  Lakini pia naona Wapinzani na Chama Tawala nao pia wanazishambulia asasi hizi wakati mwingine, na wakati huo huo naona pia serikali imewahi kuwa kwenye mivutano na asasi hizi zisizo za kiserikali, Haki Elimu na kufutwa kwa BAWATA ni mifano halisi.

  Je kwa Jumuia hizi za Kiraia zikiwemo NGO, Serikali, Wanasiasa, wote hawa wanafanya kazi kwa maslahi ya umma?

  Je kuna tafiti gani ya uhakika ambayo imewahi kufanywa kama tathmini ya hali ya Jumuia za Kiraia Tanzania, mahusiano yake kwa umma, changamoto na mafanikio yaliyokwisha patikana?

  Mwenye nondo naomba anishushie hapa.
   
 2. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #2
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hizo baadhi ya NGO ni machaka ya uhujumu wa misaada ya walala hoi.Viongozi wengi wa serikali wamejikita kwenye hizi asasi zisizo za kiserikali kwa masilahi binafsi.Kuna watendaji wengi wanachuma kupitia hizi asasi kwa visingizio vya kuwapelekea huduma walengwa.
  Mathalani kuna taasisi moja inayokwenda kwa jina la kuwasaidia wasanii katika fani mbali mbali.Cha ajabu viongozi wa juu wa Asasi hiyo hutuma maombi kwa kutumia wasanii wachovu na kukubaliana kugawana mapato.Asasi hii inafadhiliwa na nchi kama tatu za scandinavia.
  Hiyo ni moja tuu kati ya zile ninazozifahamu.
  Hii ndo Bongo ambapo ukitumia bongo kuwaumiza Wabongo ndo unaonekana una bongo kuliko wenyewe Wabongo!!!
   
Loading...