Jumuiya yetu ya Kanisa Katoliki imevunjika sababu ya michango kuwa mingi

Hivi ukatoliki nao ni Ukristo au njia ya kuwapeleka watu jehanam?Acheni roho mbaya jamani,mnawadanganya watu kuwa wanamuamudu Mungu,kumbe wanamwabudu Shetani.Huruma sana.Adhabu yenu itakuwa kubwa sana mbele za Mungu.
Huyu Kenge naye katokea wapi ???. Hivi hujui Kanisa Katoliki ndo lililopata Ufunuo wa Roho Mtakatifu ??. Shauri yako endelee King'aa sharubu huko. Njoo RC wewe uokolewe na moto wa milele.
 
Wanajamii sijui tunaelekea wapi katika maisha haya?

Kanisa Katoliki tumezoea kuwa na Jumuiya ndogo ndogo kwa ajili ya kusali pamoja na kushirikiana mambo mbali mbali ndani na nje ya kanisa. Zamani tulizoea kutoa sadaka tu kila tunapokutana katika jumuiya huzi zetu na sadaka hizo hupelekwa kanisani.

Lakini siku hizi mambo tofauti michango imekuwa mingi mno tena michango hiyo huanzia elfu kumi kwa kila kichwa.

Mfano, sisi katika jumuiya yetu msalaba ukilala kwako yani siku jumuiya ikisali kwako unatakiwa utoe shilingi elfu kumi, sadaka iliyopangwa kutolewa kila jumamosi ni shilingi elfu moja na mia tano kila kichwa, pia kuna mchango wa ujenzi wa kanisa kila mtu elfu 30.

Kuna mchango wa familia ya mtoto Yesu kila mmoja anatakiwa kutoa elfu kumi ili tuitimize laki tatu kwa kila jumuiya, mbali na hiyo kunakuwa na bahasha ya zaka zinakuwepo.

Yaani kwa kifupi kila wiki tunaposali kunakuwa na michango karibu 8 na yote inaanzia elfu kumi.

Tatizo linakuja usipolipa hiyo hela jumuiya inakutenga hadi ulipe madeni yote ndo unaruhusiwa tena kuingia kwenye jumuiya. Kwa sasa jumuiya yetu imevunjika kwa ajili ya michango kuiwa mingi ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.

Kweli wakristo nwenzangu hapa ndipo tulipofikia? Tunaelekea wapi kanisa katoliki la leo?!
Haya ndiyo matumizi mabaya ya Uhuru wa kujieleza.

Sina uhakika, kama michango ya Jumuiya yenu, ni ya kulazimishana. Nacho weza amini ni kuwa:

1. Ni makubaliano kati yenu yakiwa yamelenga ama kutengeneza uwekezaji wa kukabili michango ya uendelezaji huduma za sub parish,Parokia ama Jimbo lenu.

2. Ni sehemu ya mpango mkakati wa kujiwekeeni akiba, ama ya kuhudumiana kama wana Jumuiya ndani ya kanisa.

Sasa hebu jihoji kabla huja kurupuka, mlilazimishana au ni papara za matumizi ya mitandao ya kijamii.

Wakati mwingine, kaa chini jadiliana na walio anzisha utaratibu kabla hujasaka sifa za kijinga mahala.
 
Ningekuwa Kenge nisingeweza kujiunga JF,mimi ni mtu,tena kama wewe mkuu.Ila kweli nimeamini kwamba sikio la kufa halisikii dawa.
 
Nyinyi kama jumuiya mlishindwa kumsaidia mwana jumuiya mwenzenu shs 10,000/- ??????? Really ????
Kama nyie mlishindwa mnategemea padre afanyeje, huo sio ukristu. Msaada unaanzia nyumbani kwanza ndipo utoke. Kama jumuiya mnashindwa ??? Jumuiya haina fedha ??

Unafiki huh na Nina shaka na wewe. Siyo mwana jumuiya wa kweli.
Ni wanafiki jumuiya mpaka inachangia watoto wasio kuwa nauwezo kwenda mafia ndo washindwe kumsaidia 10k. Huu uzi watu wengi wanamshuhudia uongo roho mtakatifu ni bora wakatubu juu ya uzushi Huu wamesahau matendo ya mitume mtu na mkewe walipodanganya kanisa kilichowakuta
 
Wanajamii sijui tunaelekea wapi katika maisha haya?

Kanisa Katoliki tumezoea kuwa na Jumuiya ndogo ndogo kwa ajili ya kusali pamoja na kushirikiana mambo mbali mbali ndani na nje ya kanisa. Zamani tulizoea kutoa sadaka tu kila tunapokutana katika jumuiya huzi zetu na sadaka hizo hupelekwa kanisani.

Lakini siku hizi mambo tofauti michango imekuwa mingi mno tena michango hiyo huanzia elfu kumi kwa kila kichwa.

Mfano, sisi katika jumuiya yetu msalaba ukilala kwako yani siku jumuiya ikisali kwako unatakiwa utoe shilingi elfu kumi, sadaka iliyopangwa kutolewa kila jumamosi ni shilingi elfu moja na mia tano kila kichwa, pia kuna mchango wa ujenzi wa kanisa kila mtu elfu 30.

Kuna mchango wa familia ya mtoto Yesu kila mmoja anatakiwa kutoa elfu kumi ili tuitimize laki tatu kwa kila jumuiya, mbali na hiyo kunakuwa na bahasha ya zaka zinakuwepo.

Yaani kwa kifupi kila wiki tunaposali kunakuwa na michango karibu 8 na yote inaanzia elfu kumi.

Tatizo linakuja usipolipa hiyo hela jumuiya inakutenga hadi ulipe madeni yote ndo unaruhusiwa tena kuingia kwenye jumuiya. Kwa sasa jumuiya yetu imevunjika kwa ajili ya michango kuiwa mingi ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.

Kweli wakristo nwenzangu hapa ndipo tulipofikia? Tunaelekea wapi kanisa katoliki la leo?!
Ni keweli. Tena utasikia "mchango wa upadirisho, nk". Michango ni mingi hivyo wanajumuia wengine wanaokwepa aibu, kama hana kitu basi haendi. Kwasababu wawezaona michango hio ni kwa majina!
 
huu ujinga ndio sitaki.nimesoma seminari na mkatoliki mzuri ila hii michango ni ujinga ndio maana wazungu hawataki huu ujinga
Umeshawahi kukaa na wazungu. Wazungu wanachangishana kusaidia makanisa ya Africa kwanini unashindwa changia kanisa lako
 
Nikifa mtupe tu Maiti yangu swala la kutoa Pesa kanisani bora ninunue mtetea Watoto wangu wale washibe, Makanisa yenyewe Mahubiri ni kumtolea bwana hakuna jipya.
 
nyumba za ibada za siku hizi zilizo nyingi ni source of income za wajanja,sasa huwa najiuliza kwani hizi nyumba za ibada si ndio zingekuwa zinaongoza kutusitir na matatizo yetu,yaani leo ndio zingekuwa zinawatunza mayatima wengi na kuwasomesha,lakini thubutu,seminary zenyewe ada yake kama si mtoto wa kigogo huwezi soma,mkuu wacha wakutengetu ila ukweli juu ya Mungu wako uko moyoni mwako,ila wao walipaswa kukupunguzia mzigo
Ila misikitini hatuna hizo huduma
 
Hakuna jazba hapo...,mtoa mada kama michango ni mingi hakuna aliyemshikilia kwasababu kanisa haliwezi likavuruga taratibu zake kwasababu ya mtu au kikundi cha watu wasiopenda kujitolea.

Akumbuke hata hilo kanisa analosali lilijengwa na watu kama yeye au wewe 3Angels massage au Abby Newton, naomba kwa makini pitieni kwa umakini kitabu cha Wafalme,zaidi Wafalme 9:3.

Mkishamaliza kusoma mlinganishe hicho mnachokishabikia na mpango wa Mungu kwa mwanadamu,mathalani mtoa mada na washirika wake watakuwa wamebeba agenda nyengine wakijificha kwenye kivuli cha Michango...!!!!

Hekalu la Israeli liliwahi kukarabatiwa kama si kujengwa upya sio chini ya mara moja na waliolijenga ni wana wa Israel bila manung'uniko kama yenu.

Yeye mtoa mada pamoja nanyi washirika wake mnafikiri jengo la kanisa linashuka toka mbinguni...???

Naomba niishie hapa asbh hii.
Ha ha ha

Inabidi utofautishe namna ya utoaji wa wana waisraeli wakati wa kujenga mahekalu na huu wa kwenu unaolalamikiwa

Waisraeli waliambiwa wale watakaotoa watoe kwa moyo wa kupenda hivyo kila mtu kwa kadri ya uwezo wake alitoa ili kulijenga hekalu LA Bwana

Tofauti na nyie mnaoweka viwango kuwa kila mtu atoe sijui elfu 10 wakati mwingine hiyo elfu 10 ni bajeti ya wiki na asipotoa anatengwa kama wachangiaji walivyosema

Kwa hiyo utaona kanuni yenu ya utoaji ni ya lazima na sio ya kutoa kwa upendo kama Mungu atakavyo kitu ambacho ni makosa
 
Kuna mdada namjua huwa anauza juice yaaan juzi hapa alikwenda huko kanisani wamempulula pesa zote, kaja tumuazime6000 aongezee msingi wake, anakwambia labda kwa mwaka anaenda mara mbili, tatizo michango kedeked mtu akienda na 100,000 anarud na 20,000
 
Mlaze msalaba kwangu, niwalundie halafu bado mnitoze hela? Nyumba za Inada ni kati ya maeneo ambayo nimepoteza kabisa mwamko nayo. Mimi nina iishi injili hivyo sioni thamani ya hizo taratibu zao.
Kuna kanisa moja lipo pale kimara ndanindani, hilo siku ya jumapili unapikwa mpka ugali, kila mtu anachangia mchango wa MENU, na mnaitwa majina kabisa, huku jmaaa akitia tiki, sasa kuna dada mmoja anaitwa Martha alikuwa akipiga huduma hapo anakwambia usipokwenda balaaa
 
Ovyooo.
Wanajamii sijui tunaelekea wapi katika maisha haya?

Kanisa Katoliki tumezoea kuwa na Jumuiya ndogo ndogo kwa ajili ya kusali pamoja na kushirikiana mambo mbali mbali ndani na nje ya kanisa. Zamani tulizoea kutoa sadaka tu kila tunapokutana katika jumuiya huzi zetu na sadaka hizo hupelekwa kanisani.

Lakini siku hizi mambo tofauti michango imekuwa mingi mno tena michango hiyo huanzia elfu kumi kwa kila kichwa.

Mfano, sisi katika jumuiya yetu msalaba ukilala kwako yani siku jumuiya ikisali kwako unatakiwa utoe shilingi elfu kumi, sadaka iliyopangwa kutolewa kila jumamosi ni shilingi elfu moja na mia tano kila kichwa, pia kuna mchango wa ujenzi wa kanisa kila mtu elfu 30.

Kuna mchango wa familia ya mtoto Yesu kila mmoja anatakiwa kutoa elfu kumi ili tuitimize laki tatu kwa kila jumuiya, mbali na hiyo kunakuwa na bahasha ya zaka zinakuwepo.

Yaani kwa kifupi kila wiki tunaposali kunakuwa na michango karibu 8 na yote inaanzia elfu kumi.

Tatizo linakuja usipolipa hiyo hela jumuiya inakutenga hadi ulipe madeni yote ndo unaruhusiwa tena kuingia kwenye jumuiya. Kwa sasa jumuiya yetu imevunjika kwa ajili ya michango kuiwa mingi ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.

Kweli wakristo nwenzangu hapa ndipo tulipofikia? Tunaelekea wapi kanisa katoliki la leo?!
Ovyo. Mambo ya jumuiya. Usharika unakuja kuyaweka hadharani hapa wakati unajua kuna wa famasia na na waganga wasiotoa sadaka aina yoyote kwenye nyumba zao za ibada. Hujivunii makanisa yanavyo vutia sababu ya michango. Unaweza kuyalinganisha na nyumba za ibada za upande ule mwengine ambao michango yao kwa wiki haifiki hata laki. Hujibunii sisi sadaka ya jumapili moja ni ova 20 m.
Ovyoo sana wewe. Ova and out
 
Haya ndiyo matumizi mabaya ya Uhuru wa kujieleza.

Sina uhakika, kama michango ya Jumuiya yenu, ni ya kulazimishana. Nacho weza amini ni kuwa:

1. Ni makubaliano kati yenu yakiwa yamelenga ama kutengeneza uwekezaji wa kukabili michango ya uendelezaji huduma za sub parish,Parokia ama Jimbo lenu.

2. Ni sehemu ya mpango mkakati wa kujiwekeeni akiba, ama ya kuhudumiana kama wana Jumuiya ndani ya kanisa.

Sasa hebu jihoji kabla huja kurupuka, mlilazimishana au ni papara za matumizi ya mitandao ya kijamii.

Wakati mwingine, kaa chini jadiliana na walio anzisha utaratibu kabla hujasaka sifa za kijinga mahala.
Hulazimishwi kutoa na Usipotoa " unatengwa" sasa huelewi nini hapo kama siyo wewe ndio unakurupuka!
 
Ni kweli michango imekuwa Mingi sana,yaani kama mtu unatoa kama kanisa linavyotaka unaweza kukosa hata hela ya matumizi yako binafsi,kumbuka tunatakiwa kutoka zaka 10% ya kipato chako,hapo hapo kuna michango lukuki nje ya hiyo zaka,na bado kodi za serikali pia.Kiukweli ni mzigo mkubwa
 
sina hakika sana na mchanganuo wako lakini kama ni kweli hii ni hatar sana kwani inawasababisha wasio na kipato kuto penda kwenda kusali kwa kuhofia mfuko
 
Back
Top Bottom