Jumuiya yetu ya Kanisa Katoliki imevunjika sababu ya michango kuwa mingi

Hivi pengo yupo?...okkkk....peleka malalamiko yako kwake...nashauri na jumuiya zingine zote zife ili maaskofu kama pengo wajuwe vimekaza ndio watamwambia uchwara....

NATAMANI KUWA MKRISTO MKATOLIC WA DRC....mpaka raha aisee...wanaandamana kushinikiza dictator kabila aachie ngazi.
 
we katekista acha kujivua ufahamu mnatukamua mno alafu mnatukaririsha kuwa sadaka n lazma kanisan? tatiz tunakaririshwa mno sheria za kanisa badala ya Bible
Acha kusali na uhame Kabisa Kanisa, halafu tuone km kwa ubahiri wako km utanunua hata ka Fast jet kamoja !!!.
 
Na wewe ndio wale wakatili, wezi na majambazi mnaowaibia waumini kwa visingizio vya sadaka, za mwizi 40, mtakamatwa tu..
Tafuta kazi, jipatie kipato chako halali kuliko kutegemea kuiba toka kwenye sadaka..
,imenibidi nicheke kidogo kwanza, maana kuna wakati Vichaa nao hawajambo kwa kuchekesha.
 
Nakushauri km vipi sepa hatukubembelezi.
Ha ha ha kumbe ni katekista

Sasa mtumishi jazba za nini mpk unafukuza waumini wanaolalamikia jambo la ukweli, mnawafunga midomo wasihoji

Punguzeni michango mnawakamua sana waumini na kuwatisha kuwanyima huduma kwa kigezo cha pesa
 
Tatzo kubwa la baadhi ya wakatoliki ni kushika sn sheria za kunisa kuliko biblia yenyewe. Mleta mada hapa ameleta malalamiko ya mambo ambayo yameenea takribani makanisa yote. Mimi nnajamaa zangu wa SDA nao walishanimbia kwamba hata kwao sku hz kero hz zimeanza kushamiri. Unapopaniki ili kuficha uovu haikusadiii ww wala dhehebu lako. Usjifanye kusahau baadhi ya viongoz walivyoliletea kanisa katoliki aibu kwa kupokea fedha za Es.c.r..w chanzo ndo hiyo hiyo michango. Funguka ndugu sote ss ni wamoja na ukristo ni wetu sote tumekemee kwa nguvu mambo yote yanayoweza kutusababisha tushindwe kuiona mbingu.
Mkuu mbona unatumia nguvu nyingi sana kutetea mambo ambayo ni kawaida..??

Mleta mada analalamika kuwa Kanisa Katoliki limezidi kwa michango ikiwa ni pamoja na mchango wa ujenzi wa kanisa.

Hivi hilo Kanisa analosali sasa hivi hajui kuwa lilijengwa na waumini kama mimi na yeye na wewe...???labda leo hii wameshatangulia mbele ya haki wanakula mema Peponi kwa kujitolea ktk kazi ya Mungu...,huyo mtoa mada anaonekana tatizo sio michango ila kuna agenda nyengine ameibeba...,

Ukifuatilia biblia kuna watu walijitolea kama sio kukarabati ni kulijenga upya Hekalu nyakati hizo na hata leo kuitegemeza nyumba ya Mungu ni pamoja na kujenga na kununua vifaa husika ndani yake.....,hapa ni tofauti na Zaka au Fungu la kumi..,

Ndg nimeona mahali umeni quote ukitumia mfano mfu wa Magufuli na shule za bure...!!kitu ambacho akiwezekani kikawa mfano kwa haya tunayoyaongelea.

Wahenga walisema "KUTOA NI MOYO NA WALA SIO UTAJIRI" mwisho wa kunukulu,sasa wewe mwenyewe Abby Newton hii gharama unayotumia hapa kutetea mambo yasiyokuwa na misingi ya kiimani ungeweza ukapeleka hata Tofali moja pale kanisani kwako nikiwa na maana tofali moja ni Tsh 1300/= ni sawa na Mb 400 kwa mtandao wa Voda au Mb 800 kwa mtandao Halotel nk.

Tumia nguvu kwa mambo ya msingi na Mungu atakubariki.

Asante.
 
Eti umesemaje??? Hivi unafikiri kuna Ukristo bila Ulatoliki..??
Hivi ukatoliki nao ni Ukristo au mpango mahsusi wa kuwapeleka watu jehanam?Acheni roho mbaya jamani,mnawadanganya watu kuwa wanamuamudu Mungu,kumbe kwa makusudi kabisa kwa siri mnawaabudisha Shetani.Huruma sana.Adhabu yenu itakuwa kubwa sana mbele za Mungu.
 
huu ujinga ndio sitaki.nimesoma seminari na mkatoliki mzuri ila hii michango ni ujinga ndio maana wazungu hawataki huu ujinga
 
Ha ha ha kumbe ni katekista

Sasa mtumishi jazba za nini mpk unafukuza waumini wanaolalamikia jambo la ukweli, mnawafunga midomo wasihoji

Punguzeni michango mnawakamua sana waumini na kuwatisha kuwanyima huduma kwa kigezo cha pesa
Hakuna jazba hapo...,mtoa mada kama michango ni mingi hakuna aliyemshikilia kwasababu kanisa haliwezi likavuruga taratibu zake kwasababu ya mtu au kikundi cha watu wasiopenda kujitolea.

Akumbuke hata hilo kanisa analosali lilijengwa na watu kama yeye au wewe 3Angels massage au Abby Newton, naomba kwa makini pitieni kwa umakini kitabu cha Wafalme,zaidi Wafalme 9:3.

Mkishamaliza kusoma mlinganishe hicho mnachokishabikia na mpango wa Mungu kwa mwanadamu,mathalani mtoa mada na washirika wake watakuwa wamebeba agenda nyengine wakijificha kwenye kivuli cha Michango...!!!!

Hekalu la Israeli liliwahi kukarabatiwa kama si kujengwa upya sio chini ya mara moja na waliolijenga ni wana wa Israel bila manung'uniko kama yenu.

Yeye mtoa mada pamoja nanyi washirika wake mnafikiri jengo la kanisa linashuka toka mbinguni...???

Naomba niishie hapa asbh hii.
 
Wanajamii sijui tunaelekea wapi katika maisha haya?

Kanisa Katoliki tumezoea kuwa na Jumuiya ndogo ndogo kwa ajili ya kusali pamoja na kushirikiana mambo mbali mbali ndani na nje ya kanisa. Zamani tulizoea kutoa sadaka tu kila tunapokutana katika jumuiya huzi zetu na sadaka hizo hupelekwa kanisani.

Lakini siku hizi mambo tofauti michango imekuwa mingi mno tena michango hiyo huanzia elfu kumi kwa kila kichwa.

Mfano, sisi katika jumuiya yetu msalaba ukilala kwako yani siku jumuiya ikisali kwako unatakiwa utoe shilingi elfu kumi, sadaka iliyopangwa kutolewa kila jumamosi ni shilingi elfu moja na mia tano kila kichwa, pia kuna mchango wa ujenzi wa kanisa kila mtu elfu 30.

Kuna mchango wa familia ya mtoto Yesu kila mmoja anatakiwa kutoa elfu kumi ili tuitimize laki tatu kwa kila jumuiya, mbali na hiyo kunakuwa na bahasha ya zaka zinakuwepo.

Yaani kwa kifupi kila wiki tunaposali kunakuwa na michango karibu 8 na yote inaanzia elfu kumi.

Tatizo linakuja usipolipa hiyo hela jumuiya inakutenga hadi ulipe madeni yote ndo unaruhusiwa tena kuingia kwenye jumuiya. Kwa sasa jumuiya yetu imevunjika kwa ajili ya michango kuiwa mingi ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.

Kweli wakristo nwenzangu hapa ndipo tulipofikia? Tunaelekea wapi kanisa katoliki la leo?!
Mbona hawara pamoja na bia unawapa nyingi? Huoni kwamba unamuibia Mungu? Siku hizi wajomba hawatoi. Hatuna budi kulitegemeza kanisa letu wenyewe
 
Sio huko Tu asee nyumba za Ibada karibia za Imani zote Wanakomaa na Michango tu, nyumba za ibada sio mahali tena pakukimbilia kwa wasio jiweza
 
Eti mtu km hatoi sadaka na michango wanagoma kumbatiza mtoto wake( japo ubatizo wa watoto si sahihi),wanagoma kufungisha ndoa nk sjui huu utaratibu wameutoa wapiii??Kituko kingine kubatiza mtoto hela, kuandikisha ndoa hela.Yaani hela hela helaa !!! Ukristo gani huu jamani tukubali ukweli na tuwaambie watumishi ukristo umepotokaaaa
Sasa kama hutaki shiriki kanisani kwanini tukubatize huna ushirika nasi halafu unataka batizwa
 
Usimwangalie Kardinali Pengo, wewe Mtazame Kristo huyo ndo Kipimo cha Ukamilifu, Pengo ni mwanadamu km wewe tu, Huoni hata Petro alikemewa na Yesu kuwa Rudi Nyuma yangu Shetani wewe ???!!!. Wakati kabla yake alimwambia "Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu ".Sasa km Petro aliwahi kuitwa Shetani, sembuse Pengo. Tafadhari Usikwazike kizembe hivyo.
Huyo mtu shida yake akiwa kanisani huwa anasinzia hakumbuki lile ombi "usizitazame dhambi zetu ila imani ya kanisa lako"
 
Viongozi wa kanisa hili wabaguzi, ukifa mlalahoi anatumwa katekista kwenye ibada ya mazishi, akifa tajiri kwenye mazishi anakuja padri. (Kwa walio waumini tuu)
Na ukiwa tajiri maarufu wanakuja maaskofu 5 na mapadri 8
 
Back
Top Bottom