Jumuiya ya wazazi mnaipeleka wapi ccm!

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Baada ya heka heka kubwa na vurugu za hapa na pale zikiambatana na mipasho kibao kwenye vyombo vyetu ya habari( sio udaku) japo kwa sasa naanza kupata wakati mgumu kutofautisha vipi ni vyombo vya udaku na vipi si vyombo vya udaku!
Naandika hili ili wote watakaoona kuna umuhimu basi nipate mawazo yao. Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi wiki iliyopita ilimaliza uchaguzi wake kwa kujaza nafasi mbali mbali ikiwemo ile ya Mkiti ambapo Balozi Mhina alimshinda mpinzani wake mkuu Bwana Bulembo! baada ya uchaguzi mengi yamesemwa mengine yakiwa ya kweli mengine yakiwa ni kuendeleza zile siasa zetu za maji taka! binafsi ningependa kupata mawazo hapa kwa kuamini kuwa hapa JF kuna wale waliokunywa maji ya Bendera (CCM) kama inavyoaminka na wengine wasiotaka hata kusikia jina hilo, hoja yangu hapa ni kuwa WAZAZI wametumia kigezo kipi kumchagua balozi Mhina mwenye umri wa lala salama? Mzee asiye weza kufanya hata mikutano mitatu ya ya hadhara ya kampeni kwa siku moja! Balozi Mhina ataweza kupambana na ZITO KABWE JUKWAANI KULE KIGOMA! BALOZI MHINA ATAWEZA KUPAMBANA NA NA NDESA kwenye kampeni Moshi! na kumuacha mtu kama Bulembo eti hana Elimu, aliyesema ukiwa Mkiti wa wazazi wa CCM utakuwa na vipindi chuo kikuu cha Muhimbili nani? wazazi wanaweza kutuambia nini juu ya F.S aliyepata uwaziri mkuu akiwa na Diploma ya kilimo? au A.L.M aliyepata kuwa waziri wa mambo ya ndani akiwa na cheti cha ualimu! na mifano mingi kibao. kibaya zaidi kinachozuka CCM muda huu ni kila mtu akiungwa mkono na watu wengi eti FISADI! FISADI, FISADI, FISADI. ninachokijua mimi ABDALA MAJURA BULEMBO angeweza kufanya kazi nzuri zaidi ya kuongoza jumuiya ya wazazi kuliko Mzee Mhina. katika mazingira ya kisiasa ya leo kumuacha Bulembo na kumchagua Mzee Mhina si elewi kabisa CCM inakwenda wapi! any way let me call it a story! nimalizie kwa msemo mmoja wa kisukuma na kinyamwezi MBITI YA TYULULUKA HA SHIGULU, YA MBULA NHALE! ( kwa kawaida fisi hupenda kusimama juu ya kichuguu kwa muda mrefu, ukimuona fisi kasimama juu ya kichuguu na kushindwa kuhimilikisha kuteleza basi ujue mvua imesha kubwa sana
 
M-bongo mbona walalamika sana au nawe ulikuwa Dodoma nini? na kama kashindwa Bulembo si uchaguzi au, na swala la kuwa alichaguliwa ni mzee we ina kuhusu nini! hata kama huyo hataweza kuhimili mikiki mikiki ya kampeni si ndio bomba ili tuwachape vizuri maana sikio la kufa halisikii dawa! malalamiko yako wengine hayatusaidii kama mnachemsha wengine ndo furaha yetu, twa subiri kwa hamu
 
Kuna habari kutoka Raia mwema hapa... ndio huyu jamaa yako alitaka kufanya vitu nini?
Mashushushu wazima mamilioni ya mgombea

MAMILIONI ya fedha zilizokuwa ziingizwe kwenye harakati za kusaka ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), wiki iliyopita, zimezua utata baada ya vyombo vya dola kuhakikisha haziingii Dodoma kuharibu uchaguzi, Raia Mwema limefahamishwa.
Imefahamika kwamba fedha hizo zilizozuiwa na watu walioelezwa kuwa ni “maalumu” zilikuwa ziiingizwe kwenye akaunti iliyopo benki moja maarufu nchini, tawi la Dodoma. Zilikuwa zimepangwa kugawanywa kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi. Wagombea katika uchaguzi huo walikuwa ni Balozi Athuman Mhina, Abdallah Bulembo na Esther Nyawazwa.
Habari zilizopatikana zinasema baada ya kampeni kuonekana kuwa ngumu kwa pande zote, mkakati wa mwisho wa mgombea mmoja ulikuwa ni kutumbukiza pesa (Sh. milioni 400) ambazo zilikuwa ziingizwe kwenye akaunti moja ya benki hiyo tawi la Dodoma ili zigawanywe; hivyo kumalizia kazi ya kuwaweka sawa wapiga kura, na hatimaye kufanikisha ushindi wa mgombea husika.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa nyendo za kundi la mgombea husika zilikuwa zikifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya dola vilivyohakikisha fedha hizo haziingii kwenye akaunti hiyo kutoka Dar es Salaam ili zisigawanywe kwa wapiga kura Dodoma na kuvuruga uchaguzi.
“Watu walikuwa wamejipanga vizuri sana, sijui kwa maelekezo ya nani, lakini walikuwa makini sana kuhakikisha kasi ya mbinu chafu haitawali uchaguzi. Kwa hiyo, wakajua kuwa kuna fedha zimeingizwa kutoka kwa kundi fulani linaloshirikisha wanasiasa na wafanyabiashara wenye tatizo la kimaadili...ni fedha nyingi kwa hiyo kazi ikafanyika kuwa ni lazima kuhakikisha hizo fedha hazitoki benki kwa wakati uliokusudiwa na wahusika wa kundi hilo ili kwenda kugawa rushwa,” alisema mtoa habari huyo.

“Sasa hawa watu na hasa viongozi wao katika kufanikisha mkakati huo walikwenda benki kuchukua fedha lakini huko walikutana na kikwazo, fedha hazikutoka kwa wakati...wakahangaika lakini hawakufanikiwa. Wakaamua kwenda kumwona meneja kujua kuna tatizo gani, huko wakakwama wakiwa wamejibiwa kwamba kulikuwa na matatizo ya kawaida ya shughuli za kibenki hivyo fedha hizo zingechelewa kuchukuliwa,” kinasema chanzo cha habari za mkakati huo uliofeli.
Habari ndani ya vyombo vya dola zimethibitisha kwamba wahusika waliotoa fedha hizo jijini Dar es Salaam kwa kutumia uzoefu wao katika sekta ya fedha walikuwa wameweka mkakati wa kukiuka taratibu za kibenki ili fedha hizo ziwahi kuingia katika akaunti iliyokusudiwa mjini Dodoma, lakini baada ya dola kuingilia kati fedha hizo zikalazimika kupitia ‘chekecheke’ la kawaida la fedha.
“Kwa kawaida fedha nyingi kama hizo (milioni 400) haziwezi kupitishwa kwa haraka haraka katika mfumo wa kibenki hasa kama mmoja wa wahusika hana kawaida ya kupokea ama kuingiza fedha nyingi kiasi hicho, kwa hiyo ni lazima ufuate utaratibu kwa kuzingatia Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu kupitia kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU), na ndicho kilichowaponza hao jamaa,” kinaeleza chanzo cha habari ndani ya serikali.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, uhakiki uliokuwa ukifanywa na vyombo husika vikiongozwa na FIU ulisababisha uchelewesho mkubwa wa fedha hizo kuingia kwenye akaunti husika mjini Dodoma, hadi uchaguzi ulipokamilika na imeelezwa kwamba fedha hizo zinaweza zisiingizwe tena katika akaunti hiyo kwa maelekezo mapya kutoka kwa wahusika ambao wamefahamishwa kuhusu utaratibu huo.
Mbali na tukio hilo lililozimwa kwa mbinu za kishushushu, vituko vingine vilivyoibuka katika uchaguzi huo ni pamoja na kuvunjwa kwa vioo vya gari la upande mmoja kati ya kambi zilizokuwa zikichuana vikali, pamoja na kuumizwa kwa baadhi ya wapambe na wana-CCM, ikidaiwa kuwa vurugu hizo zilifanywa na kundi la mgombea Abdallah Bulembo dhidi ya kundi la Balozi Athuman Mhina, ambaye hata hivyo ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kwa kura 60 zaidi ya mshindani wake wa karibu, Bulembo.

Habari zinasema matukio hayo ya ugomvi yalimkera sana Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kiasi kwamba katika hotuba yake ya kufungua mkutano wa uchaguzi huo, mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema wahuni walikuwa wameshirikishwa kwenye kampeni hizo na kuonya siku nyingine wagombea wasichukue au kushirikisha wahuni katika kampeni zao.
“Ninyi wagombea acheni kuleta wahuni katika uchaguzi kama huu, angalieni mlivyotia aibu kwa chama chenu, yaani mmeufanya uchaguzi siku hizi kuwa kama vita, tunakwenda wapi ndugu zangu.
“Ndiyo maana siku zote jumuiya hii imekuwa ikifanya mabadiliko ya viongozi kila kunapokucha, kwa mfano, ndani ya miaka minne mmebadilisha wenyeviti wawili, makatibu wanne na makamu wenyeviti wawili, hii si aibu jamani? Mbona jumuiya nyingine kuko shwari,” alisema.

Aliwataka wanachama wa jumuiya hiyo kuwachagua viongozi wa wazazi kwa utashi wao na si kwa kuzingatia maneno ya wapambe akitumia kauli mbiu kuwa “maneno ya kuambiwa ni lazima mtu achanganye na akili yake mwenyewe.”

Uzoefu unaonyesha kuwa chaguzi mbalimbali za jumuiya za CCM zimekuwa zikiandamana na malalamiko mengi yakiwamo matumizi ya rushwa katika kuwashawishi wapiga kura kumchagua mgombea na hasa atakayetoa fedha nyingi kuliko mwenzake au wenzake.

Kati ya chaguzi zilizozua malalamiko ya wazi ni wa Mwenyekiti na viongozi wengine wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambao Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sophia Simba, alichaguliwa akichukua nafasi aliyoachwa wazi na Anna Abdallah aliyestaafu.

Wakati wa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa uchaguzi huo uliomhusisha Rais Jakaya Kikwete, Anna Abdallah katika hotuba yake ya kumkaribisha Kikwete kufungua uchaguzi huo aliweka bayana kuwa “hajawahi kuona uchaguzi wenye matumizi makubwa ya fedha (rushwa) kama huo,” lakini hata hivyo, kauli yake hiyo ilibaki tu katika hotuba.
Uchaguzi mwingine uliobua malalalmiko ya matumizi ya rushwa ni wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ambamo Rais Kikwete alilazimika kuwaeleza vijana kuwa ni vema wakachagua viongozi wao bila kuingiliwa na wanasiasa wengine nje ya umoja huo kwa kutumia mbinu zozote zikiwamo za matumizi ya fedha. Kwa matatizo hayo aliyotaja Rais Kikwete, baadhi ya wagombea walilazimika kuenguliwa na hatimaye kiti cha Mwenyekiti kikamwendea Masauni Yusuf Masauni.
Matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi za CCM na jumuiya zake yameongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni kiasi cha kuwafanya watu wasio na fedha kutofikiria kabisa kuingia katika siasa na kwa upande mwingine hali hiyo imesababisha watu wenye fedha watumie mwanya huo kusimika viongozi kwa maslahi yao.
Pamoja na malalamiko hayo kuhusu rushwa ndani ya chaguzi za CCM na jumuiya zake, hakuna hatua zozote nzito za kisheria zilizowahi kuchukuliwa kwa kuwafikisha wahusika mahakamani ama kuwasimamisha uongozi.
 
Back
Top Bottom