Jumuiya ya Wazazi CCM yalaani maandamano ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya Wazazi CCM yalaani maandamano ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 6, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wazazi wa CCM nao!!! Kazi yao kubwa ni kupigia makofi chochote viongozi wao wakuu wakisema -- na wanaona kabisa serikali ya chama chao inavyokwenda hovyo hovyo!

  Angalau basi katika hili suala la maandamano ya CDM nao wangekishauri chama chao kijibu mapigo kwa hoja zinazoeleweka na za kifasaha, na siyo kubwabwaja tu eti CDM wanatishia amani!

  Hawa wazazi shule zao za kata ziko hali mbaya sana -- kwa nini wasiitake serikali kuziboresha kwa kuwaomba misada.

  Hawa ni watu walionichomoka kabisa -- mwaka 1992 walikuwa wanamshangilia Rais Mwinyi alipokuwa ananadi sera ya kuchangia elimu. Sasa wanaipata fresh kuhusu watoto/wajukuu wao wanavyonyanyaswa na bodi ya mikopo.
   
 2. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Jamani huko ndani ya CCM ya Nyerere hakuna mwenye maono (vision) aokowe jahazi. Naona kila mtu analalama tu hivis sasa imekuwa kana kwamba CDM ndo yenye serikali na CCM ni wapinzani. Hivyo wanaomba kuonewa huruma na CDM ili wasimamishe maandamano. Hivi CDM wanapita majumbani kulazimisha watu kujitokeza kwenye maandamano yao au imekaaje hii.
  CCM wameamua kwa dhati kuiongezea CDM umaarufu na ndo wanaikoleza zaidi ndani ya mioyo ya watu; manake kila siku wanaijadili badala ya kujipanga kujibu hoja.
  Sikio la kufa ......
   
 3. kitungi

  kitungi Senior Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jumuiya ya wazazi ccm imelaani maandamano ya chadema na kudai yanachochea uvunjifu wa amani kama ilivyo ktk nchi za misri, tunisia na libya. Pia wamekilaumu chadema kwa kumdhalilisha kiongozi wa nchi. Pia wameiomba serikali na vyombo vya dola viwachukulie hatua kali CDM bila woga.. Mwisho wamewtaka tendwa kuangalia uwezekano wa kikifutia CDM usajili.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye red: Vision yao kuu ni kutafuta namna ya kufanya ufisadi, basi!
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hivi hii jumuia uwa bado ipo?

  Tiba
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Jumuiya yenyewe imechoka mbaya mpaka hata shule za wazazi wakashindwa kuziendesha sasa leo watatuambia nini?
   
 8. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri wametoa tamko. Hii inaonyesha Chadema wamefanikiwa malengo yote ya maandamano hayo. Tunawashukuru wote wanayoyazungumzia.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Yaani CCM ni kama sijui viumbe gani wale...yaani akisema kitu mtu fulani hata kama ni Nonsense basi CCM wooooteeee wanakimbilia huko! Ukasuku mwingine bana
   
 10. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii jumuia mufilis bado ipo? ama kweli sasa hivi hadi maiti zinaongea. Nadhani CDM kweli wanafanya siasa, kwani hadi wale waliolala for ever wameibuka kutoka kwenye usingizi wao. Kwa nini wanalaani maandamano, hivi ni matokeo gani mabaya yametokana na hayo maandamano? Mbona hawa wanazidi kujiaibisha tu?

  CCM ya kikomunisti ilikuwa hai hasa kwa sababu jumuiya hizi zilikuwepo na zilikuwa karibu na wananchi. Sasa hivi jumuiya hizi ni historia, halafu watu wanasema eti CCM bado ipo! Hii jumuiya ni mzuka! Hebu tuone wana nini cha ziada mbali na yale yale ya kutishia kutumia vyombo vya dola kuiangamiza Chadema.

  wana wazo gani mbadala??
   
 11. markach

  markach Senior Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hama kweli wanaiongezea CDM umaharufu. Japo walibana vyombo vyao habari visionyeshe nn kinatokea lkn wao wenyewe wameamua kuipublicise. Hama kweli CDM ni chama tawala kwa sasa
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Leo ilikuwa ni Wazazi -- walionyesha ushuzi wao. Kesho watakuja Jumia ya Wanawake (UWT) nao watajitafuna midomo na kuityikia kwa vigelegele bila hata kujibu hoja moja ya akina Mbowe kuhusu masuala ya msingi waliyotaja -- hasa kuhusu ugumu wa maisha na ufisadi.

  Unajua UWT watasemaje? Watasema CDM wakileta vita wanawake na watoto ndiyo wa kwanza ku-suffer.

  Kesho kutwa itakuwa zamu ya UVCCM nao! CCM wataendelea hivi hivi tu bila hata kuingia katika kiini cha hoja zinazotolewa dhidi yao!!!
   
 13. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mwenyekiti amelewa maana nyuma kuna tangazo la Heinken
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  JEURI YA hEINEKAEN ANAYO HUYO?..

  NI WA CHIMPUMU HUYO!
   
 15. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Ningeshangaa kama angewasifu cdm. Hawa watu hawana hoja kwa kweli hakuna wakuinusuru ccm km kila mtu anakuja na pumba dhidi ya cdm. KIMSINGI TUMEICHOKA CCM PAMOJA NA MAMBO YAKE. Ni hell kuendelea kuwa na watu wenye fikra za kipuuzi km hzi dhidi ya watz. TO HELL WITH CCM
   
 16. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  enzi za digital hizi.

  enzi za 'geuzia mjini (antenna)' zilishapita.

  watu wazima hovyo kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona kila mtu sasa atatoa tamko, waifute chadema Amani ya Tanzania itabaki kwenye historia kwa miaka ile ilikuwa ya amani Ila toka utawala wa jk ndo ilikuwa mwisho wa Amani.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kama ni tamthiliya ni ramsa,wataalam wa kiswahli wanajua ramsa ni nini,tusubir matamko meng sana hadi ifikapo 2015
   
 19. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi hii jumuiya ya wazazi ya CCM inawakilisha wazazi wangapi hapa nchini? Nijuavyo mimi hiki ni mojawapo wa taasisi zilizoundwa wakati wa ukiritimba wa chama kimoja na sasa zinaendelea kuwepo kupitia mgongo wa raslimali iliyochangiwa na wananchi wote bila kujali itikadi yao.
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  alikua anakunywa za promosheni so muda huo anatangaza alikua ashaambiwa zimetosha ka vp ajinunulie ndo akageukia vyombo vya habari na kuanza kutoa maneno yenye harufu ya pombe
   
Loading...