Jumuiya Ya Watanzania Uingereza Yadaiwa Kuwa Kigenge Cha Maslahi Binafsi

barabaraya18

Senior Member
Sep 18, 2006
106
8
JUMUIYA YA WATANZANIA UINGEREZA YADAIWA KUWA KIGENGE CHA MASLAHI BINAFSI

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Abubakar Faraji amelaumiwa kwa kutumia jumuiya hiyo kwa maslahi yake binafsi. Hayo yameelezwa na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya waliodai wamemvumilia vya kutosha lakini kwa sasa wanahisi kwa maslahi ya wengi ni vyema akajiuzulu kwa faida ya watanzania waishio nchini hapa.

''Kwa kweli huyu bwana tangu ameingia imekuwa ni kutumia jumuiya hii kujinufaisha binafsi, tunashindwa kumuelewa hasa ni lini ataweka mbele maslahi ya watanzania'' alisema kiongozi mwandamizi wa Jumuiya hiyo ambae hata hivyo aliomba jina lisitajwe kwa sasa.

Abu Faraji ambae aliingia madarakani mnamo mwezi wa tatu baada ya kushinda uchaguzi inadaiwa kutumia madaraka, anajishughulisha zaidi na biashara ya kutuma mizigo nchini Tanzania ingawa tangu kuingia madarakani amekuwa na biashara nyingine kadhaa ambazo zinahusiana moja kwa moja na jumuiya ya watanzania waishio Uingereza.

Imedaiwa kuwa Abu Faraji kwa kutumia mwamvuli wa wadhifa wake amekuwa wakala wa taasisi ya kutuma fedha, Western Union ambayo humlipa kiasi kikubwa cha fedha ili waweze kuwafikia watanzania. ''Sasa badala ya kuingiza fedha hizi katika mfuko wa watanzania zitumike kwa maendeleo, Bwana Faraji amekuwa akidai kuwaleta Western Union kufadhili shughuli za Jumuiya ni mkataba wake binafsi na hivyo fedha hizo ni za kwake!'' alilalamika kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Abu Faraji aliwaburuza wajumbe wenzie wakubali yeye na aliekuwa Mwenyekiti Mwanzilishi Bi Norah Sumari wawe ndio waidhinishaji wakuu wa matumizi ya fedha za Jumuiya kwa kuwa ndio wadhamini wa akaunti ya Jumuiya, ''Kipindi kile hatukujua lengo lao kumbe walikuwa na njama maalum kwa vile sasa wawili hao wamesajili kampuni ABN REALESTATES wakishirikiana na Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Johnson Lukaza ambae ni mmoja wa waliotajwa kuhusika na kashfa ya BOT iliyopelekea kufukuzwa kwa Bwana Daudi Balali kama gavana wa Benki Kuu'' alisema.

Aidha kiongozi huyo alidai kuwa kwa kuwa Abu Faraji na Bi Norah Sumari ndio wadhamini wakuu wa akaunti ya Jumuiya kitendo chao cha kufungua biashara pamoja kinakwenda kinyume na maadili mema ya biashara kwa vile kuna uwezekano mkubwa wa fedha za jumuiya kutumiwa kwa miradi yao kwa vile ni wao pekee wenye mamlaka ya kuziidhinisha.

''Hivi sasa tunaandaa mkutano mkubwa kwa ajili ya kuhimiza uwekezaji nyumbani Tanzania na tunatarajia Rais Kikwete kuwa ndio mgeni rasmi, Abu na Norah wamejipa uratibu mkuu wa shughuli hiyo na hakika inahitaji fedha nyingi kutoka kwa wafadhili, sisi wajumbe tuna wasi wasi na matumizi ya mapato toka kwa wafadhili kwa vile ni wao tu ndio wanaojua nini kinaendelea na sisi tumewekwa kando, muda kama huu ilitakiwa tushirikishwe kuandaa mkutano huu lakini ni Abu peke yake na Norah ndio wanaouandaa sisi hata tukiulizwa tunaambiwa subirini mkutano muone vitu vyetu!'' alizungumza kwa masikitiko kiongozi huyo.

Jitihada za mwandishi wa habari hizi ziligonga mwamba kumpata Bwana Faraji kujibu tuhuma hizo za kumfanya Bi Norah kuwa mwenza wake kibiashara ingawa imebainika kuwa Bi Norah licha ya kuwa mjumbe wa kawaida kwenye jumuiya hiyo ana nguvu kubwa kutokana na ''kukumbatiwa'' na Mwenyekiti Faraji ambae humuweka mbele katika kila jukumu lenye fursa au mikutano na viongozi wakubwa wa nchi wakipita London kiasi cha kusababisha mgawanyiko baina ya Bwana Faraji na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bwana John Lusingu.

''Norah ukumbuke mdogo wake ndio alikuwa mmoja wa wahusika wa lile sakata la upimaji wa magari MOT na ndio maana kulikuwa na jitihada za jumuiya kuiunga mkono kampuni ya WTM Utility Services mpaka watu wa nje walipoingilia ndio Mwenyekiti akashtuka.

Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza ilianzishwa kutokana na jitihada kubwa ya Balozi Mwanaidi Maajar lakini hadi hivi sasa bado haijaonekana kufanya lolote kubwa katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania licha ya viongozi wake kuingia madarakani na ahadi kede kede ikiwemo ya kukusanya paundi 80,000 ndani ya miezi mitatu iliyotolewa na Mwenyekiti Abu Faraji wakati wa kuomba kura. ''Hata asilimia moja ya fedha hizo haipo kwenye akaunti, ni vichekesho kwa kweli, alifanya watu wajinga'' alisema kiongozi huyo ambae amedai kuwa amelazimika kuzungumza na Mwandishi wa habari hizi baada ya jitihada zake za kumtaka Mwenyekiti kuitisha kikao kujadili hayo kushindikana.

Hivi sasa ofisi za Jumuiya hiyo ndio pia makao makuu ya biashara za Bwana Abu Faraji na Bi Norah Sumari ambao kampuni yao ya ABNREALESTATES inashirikiana na Mfanyabiashara Johnson Lukaza ambae ametajwa kama mmoja wa wamiliki wa kampuni zilizojinufaisha katika utaratibu wa EPA sakata iliyosababisha aliekuwa gavana wa benki hiyo kujiuzulu.

Mwenyekiti Abu Faraji ambae hadi hivi karibuni alikuwa na heshima kubwa miongoni mwa Watanzania ameelezwa kuwa karibu mno na Balozi Mwanaidi Maajar ambae inadaiwa ndio hasa aliemshawishi Bwana Faraji agombee kwa vile anafahamiana na familia ya Bwana Faraji.

Mama yake Bwana Abu Faraji ni afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini ambae ana ukaribu mkubwa na Balozi Maajar tangu wakiwa shuleni pamoja.
 
Hivi huu woga tutauacha lini? Yaani huyu kiongozi anaogopa kutaja jina lake hata kwa akina Abu Faraja? Sasa kwa nini tusidharau hizi habari zake? Kama ana uhakika na anachokisema kwa nini asitaje jina lake? Sasa kwa nini tusizione hizi habari kwamba ni uzushi tu na kupakana matope?
 
Hivi sasa ofisi za Jumuiya hiyo ndio pia makao makuu ya biashara za Bwana Abu Faraji na Bi Norah Sumari ambao kampuni yao ya ABNREALESTATES inashirikiana na Mfanyabiashara Johnson Lukaza ambae ametajwa kama mmoja wa wamiliki wa kampuni zilizojinufaisha katika utaratibu wa EPA sakata iliyosababisha aliekuwa gavana wa benki hiyo kujiuzulu.

Makubwa haya! movie hii sijui itaisha lini yaani kama sinema ya ya kihindi sterling anazaliwa, anakua, then anakuja kulipiza kisasi cha kwa waliofanyizia mzee wake.
 
Watanzania tayari tunawakaribia Wanigeria.

Yebo Yebo umepotelea wapi? Naona watakuingiza na wewe kwenye ufisadi.

Usikubali mkuu, TZ inahitaji watu safi
 
Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza ilianzishwa kutokana na jitihada kubwa ya Balozi Mwanaidi Maajar lakini hadi hivi sasa bado haijaonekana kufanya lolote kubwa katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania licha ya viongozi wake kuingia madarakani na ahadi kede kede ikiwemo ya kukusanya paundi 80,000 ndani ya miezi mitatu iliyotolewa na Mwenyekiti Abu Faraji wakati wa kuomba kura. ''Hata asilimia moja ya fedha hizo haipo kwenye akaunti, ni vichekesho kwa kweli, alifanya watu wajinga'' alisema kiongozi huyo ambae amedai kuwa amelazimika kuzungumza na Mwandishi wa habari hizi baada ya jitihada zake za kumtaka Mwenyekiti kuitisha kikao kujadili hayo kushindikana.

Kama kweli huyu jamaa (mtoa habari) alimtaka mwenyekiti wake aitishe kikao, impliedly, Abu Faraji anamfahamu ni nani na hivyo sioni mantiki ya kutotaja jina lake. Mpaka hapo ameishajiweka wazi!

Vinginevyo halitakuwa swala la woga bali ni udaku ambao unaweza kuwa na ukweli ndani yake ila unakuja kwa style ya kuchomeana utambi ama kwa style ya ukimwaga ugali, mimi ninamwaga mboga ... kitu mgao kinaleta shida kwenye hizo deals!
 
Unajua haya anayoyasema huyu bwana yalikuwa wazi tangu siku ile wanachaguana. Wengine tulisema tuweke kwanza institutional structures in place, wao wakang'ang'ania kugawana vyeo akiwemo huyu anayelalamika kwa sababu tayari walishajipanga hivyo. Haya anayoyaongea hapa yalijulikana kwamba yatakuwa hivyo tangu siku ile ya uchaguzi. Sasa ndio maana mimi namuona ni mnafiki, hamna kipya hapa. There is nothing new here that we did not know before. Walichaguana ili watumie hii jumuiya kuweka mambo yao sawa hapa UK. Sasa namshangaa anajifanya ndio anayajua leo; inaonekana wameshaanza kuzidiana kete wao kwa wao sasa wanataka sisi wanajumuiya tuwasaidie.
 
Ufisadi na majungu vinaua waTZ kuanzia nyumbani(Bongo) mpaka ughaibuni........aibu hii!!.
 
ndio yale yaleeeee ya ccm na balali....leo wanapanga na kula dili la nguuuuvu one akishakua na power zaidi likitokea la kutokea baaasi anampiga chini mwenzie na yeye kuanza jifanya u so fresh so clean clean!!!!
yaani ni kama movie mbili tofauti with the same objective labda zimekua tu released muda tofauti
 
Yaaani bongo wanalimana sasa imetoka ripoti, na huko majuu ni hivyo hivyo yale yale ya bongo? Yaaani ufisadi hadi huko majuuu?
 
Yaaani bongo wanalimana sasa imetoka ripoti, na huko majuu ni hivyo hivyo yale yale ya bongo? Yaaani ufisadi hadi huko majuuu?

Mimi sijui hii nchi tutajificha wapi. Ndio mimi FMES nasema tufike mahala tukubali tujaribu na chama kingine. Nasema hivi kwa sababu CCM inatu-haunt kila tunapoenda. Hawa jamaa karibu wote walichaguliwa kwa ticket ya CCM balozi akiwa ndiye mdhamini wao. Sasa wameenda pale wakijua ni CCM ndiye iliyowaweka na wala sio hao watanzania waliopo UK. Haya tuliyaona na kuyasema tangu siku ya uchaguzi lakini ndio hivyo demokrasia ikachukua nafasi yake maana tulikuwa kama wawili tu wenye mawazo tifauti. Sasa ni deal tu kwa kwenda mbele, it is shame on us.
 
Sasa kama hii ndiyo hali, is there a solution. Kitila, na wengine any suggestions? At least this UK thing is a small and manageable situation- and to me if solutions can be sort for smaller structures, we can learn how to curb the bigger monsters like BOT..
 
Dawa ya Abuu na kummaliza balozi ni kupata uongozi mpya kabisa na waombeni wote wa zamani waondoe majina yao na hakuna kumpitisha mtu bila ya kupingwa .
 
Kwa nini watanzania mliko huko msiunde jumuia nyingine? au mnahisi hamtakuwa connected?????? Nnasikia harufu ya CCM syndrome.....
 
Kwa nini watanzania mliko huko msiunde jumuia nyingine? au mnahisi hamtakuwa connected?????? Nnasikia harufu ya CCM syndrome.....

Wakiunda umoja mwingine hawatatambuliwa na serikali yetu inayotaka kuona kila sehemu inaweka viongozi wake mfano chuo kikuu ambako wanajaribu kuakikisha viongozi wao ndo wanachukua madaraka.
 
Dawa ya Abuu na kummaliza balozi ni kupata uongozi mpya kabisa na waombeni wote wa zamani waondoe majina yao na hakuna kumpitisha mtu bila ya kupingwa .

Huu umoja kwa sasa ni kama vile una exist kwa watu wa london tu, hivi Balozi na viongozi wa TA wanatarajia watu wa, lets say Leeds, Newcastle au Manchester watajoin umoja huu na kuingia gharama za kusafiri kila mara kunapokuwa na vikao? Tunachohitaji sasa ni kuwa na matawi kwenye kila county, na naamini huku chini kwenye matawi tutapata viongozi ambao watakuwa na uwezo wa kuwango'oa wale wa 'Makao Makuu' London kwenye uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom