Jumuiya ya Uamsho ya Kiislamu wakusanya saini ya kutaka kura ya maoni juu ya Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya Uamsho ya Kiislamu wakusanya saini ya kutaka kura ya maoni juu ya Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 30, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on April 30, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa kushirikiana na taasisi kadhaa za kiislamu za hapa Zanzibar zimeanza kutoa fomu ya kuitishwa kura ya maoni juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. fomu hizo zinapatikana katika maeneo mbali mbali ikiwemo katika ofisi za Jumuiya ya Maimamu na Jumuiya ya Uamsho zilizopo Mkunazini Unguja
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Wazanzibar hawako kungagania Muungano kauli nikuvunja na kugawana mbao, Jee Wa-Tanganyika Muka tayari kubakia kuwa Watanzania na bye bye Tanganyika yenu?.
   
 3. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Every citizen has the right to decide on his destiny. And in his judgement there is no partiality.
  Let the people decide PEACEFULLY what they want.
   
 4. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hatuvunji muungano wasioutaka wazoweye tu
   
 5. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80

  Mimi ni MTZ bara na siko tayari kuona Muungano unavunjika. Sababu ni kwamba ndugu zetu wa Zanzibar hawawezi kudumu kama taifa kwa hata mwezi mmoja bila ya kuchinjana. Naamini kila dini ina mambo yake mazuri. Kutoka kwa Wayahudi kuna usemi kwamba; "Anayeokoa maisha ya mtu mmoja, ameokoa maisha ya binaadamu wote"

  Napenda kufikiri kuwa tunawaokoa Wazanzibari dhidhi ya kuchinjana
   
 6. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kwanini jumuiya za kiislamu ndo zimeshupalia jambo hili?
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Self determination
   
 8. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  [h=1]Zanzibar yaelekea kwenye uhuru wake[/h]

  i

  Rate This​
  [​IMG]
  [​IMG]Picha ya pamoja ya uongozi wa juu wa Tanzania na Tume ya Katiba.

  Rais Jakaya Kikwete ameiapisha Tume ya Katiba, kama inavyojuilikana, ambayo jukumu lake ni kukusanya maoni ya Watanzania juu ya katiba wanayoitaka. Katika uapishaji huo uliofanyika Ikulu ya Magogoni, Ijumaa ya 13 Aprili 2012, Rais Kikwete aliwakumbusha 'ambao' hawautaki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wajuwe kuwa si Tume yake aliyoiunda ya kuwasaidia kupata muradi wao.
  Mimi ninampa changamoto Rais Kikwete, akiwa kama kiongozi wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba iwe kwa kupitia Tume yake aliyoiapisha au njia nyengine, sio tu kwamba wasioutaka Muungano watauvunja, bali tayari 'wameshauvunja'. Kilichobakia ni kuusomea Arubaini yake, kwa mila za kwetu.
  Dalili moja kwamba Muungano huu umeshavunjika tayari, ni yeye kulazimika kutumia muda wake kuwazungumzia watu wa kundi hilo, ambao miaka 20 nyuma wasingekuwa sehemu ya hotuba ya Rais, bali watu waliokwishanyamazishwa chini kwa chini. Ndiyo, Mheshimiwa Rais, wanaotaka kuuvunja Muungano, wanauvunja vipande vipande!
  Wala sisemi hivyo kwa sababu ya mihadhara ya Jumuiya za Kiislamu na Baraza la Katiba na wimbi la maoni kwenye mitandao ya kijamii inayotumiwa na Wazanzibari. Najua na nathamini sana mchango wa kipekee wa kazi hizo, lakini najua pia kwamba kazi kubwa kabisa inahitajika kufanywa kutimiza azma ya wasioutaka Muungano.
  Nje ya sababu na hoja za kisheria na kisomi ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu na wanaharakati kadhaa, mimi nataka nizungumzie hizi za akina miye pangu-pakavu, ambao hatujui mengi sana kuhusu sheria na utaalamu wa siasa.
  La msingi kuliko yote, ni kuweka wazi kwamba Muungano wowote wenye nguvu unalazimika kujengwa na washirika wenye nguvu pia, walio huru na wenye uchaguzi wa uhuru huo. Kinachoipa maana hoja ya kuuvunja, kwa hivyo, ni hadithi nzima ya Muungano wenyewe. Nakusudia si kwa sababu tu Zanzibar imepoteza nguvu ndani ya miaka hii ikaribiayo 50 ya Muungano, bali kwa kuwa mshirika mwenzake naye amepoteza mengi sana. Zanzibar haitoki nje ya Muungano, kwa hivyo, kwa maslahi tu ya Zanzibar, bali pia kwa maslahi ya Tanganyika.
  Tanganyika ambayo imeshindwa kujisimamia yenyewe ndani ya miaka yake 50 ya uhuru haina uwezo wa kuwa na umoja na Zanzibar. Taifa ambalo limekumbatia udini, ukabila na ueneo, kwa hakika, si mwenza anayeweza kuwa na maslahi. Zanzibar inaonekana kuwa imeshaamua kwenda mbele kama taifa moja, likiwacha migawanyiko nyuma yake. Tanganyika ndiyo sasa inazidi kuzama kwenye utengano.
  Wala isije ikahojiwa kwamba Zanzibar iliihitaji Tanganyika siku hizo ilipokuwa na mpasuko, ikasaidiwa nayo kufika hapa ilipo na sasa inataka kuiacha mkono baada ya kufikia hatua ya umoja wake. Isisemwe hivyo kwa kuwa huo sio ukweli. Ndani ya miaka ikaribiayo 50 ya Muungano, Zanzibar ilijikuta ikigawanyika zaidi kuliko kuungana, na tupo wengi tunaohoji kwa mifano ya wazi kwamba Muungano ulisimama kama nyenzo ya kuwagawa na sio kuwaunganisha Wazanzibari. Kwa hivyo, kifo cha Muungano hakitakwenda na roho ya umoja wa Wazanzibari, maana uhai wa Muungano haukusaidia katika maisha ya umoja wa Wazanzibari. Uache Muungano uende, Zanzibar na Tanganyika zibakie kila mmoja na kwake. Baina yo mataifa hayo mawili, pawe na heshima ya udugu na ujirani mwema.
  Tanganyika ambayo imejaaliwa sufufu za mali na muluku, rasilimali za kila aina na majina, lakini ambayo kwa miaka yote 50 ya uhuru wake imezidi kuzama kwenye lindi la ufukara na kugeuka kuwa taifa ombaomba, si mwenza mzuri kwa Zanzibar ambayo ina uhaba wa rasilimali, eneo na hata watu. Yaliyopo Tanganyika yangelikuwa na maana kwa Zanzibar, lau Tanganyika isingalijiwachia yenyewe kuliwa na ufisadi, ubadhirifu na wizi wa mali ya umma. Lakini hivyo sivyo ambavyo imekuwa. Badala yake pande zote mbili zinazama pamoja kwenye umasikini uliotitia.
  Wala isije ikahojiwa kwamba Wazanzibari wametumia fursa zilizopo Tanganyika kujiimarisha kiuchumi kupitia Muungano huu, maana ukweli ni tafauti. Uwepo wa wafanyabiashara wa Zanzibar (na kwa hakika wengi wao ni wabangaizaji tu) ndani ya ardhi ya Tanganyika, hakuwezi kuwa na maana tafauti ya kuwapo kwa wawekezaji wa nchi nyengine ndani ya ardhi hiyo. Ni bahati mbaya sana, kwamba holela waliyoikuta wafanyabiashara wa Zanzibar, wameitumia kwa kiwango kile kile ambacho wafanyabiashara wengine wote wanaitumia. Na hilo si jambo la kujisifu hata kidogo.
  Sasa nini kinachotokea? Watanganyika hucheka na kujipongeza waangaliapo namna walivyoidhibiti Zanzibar wakiamini haifurukuti na kamwe haitafurukuta. Huipuruzia na kuwapuruzia Wazanzibari mshipi, lakini kwa mawanda yasiyokwenda mbali. Kisha wenyewe hulia wazitazamapo hali za maisha yao wenyewe, changamoto nyingi na matatizo yanayowakabili. Na ndio hapo hugundua kwamba hata haya mabavu yao dhidi ya Zanzibar hayawafalii jambo. Nguvu ya Muungano inapungua na Zanzibar inaelekea kwenye uhuru wake.
  Kwa hivyo, kwa Rais Kikwete na wenye mtazamo kama wake, ukweli uliopo ukutani ni kwamba, Muungano huu unavunjika si kwa sababu tu Wazanzibari wanataka iwe hivyo, bali kwa kuwa Tanganyika haiihimili tena Zanzibar. Si leo tena!
   
 9. IROKOS

  IROKOS JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,191
  Likes Received: 2,625
  Trophy Points: 280
  Nimewahi kusoma makala moja ikimnukuu mmoja wa waasisi wa muungano, hayati Karume akisema: 'Muungano ni kama koti likikubana unalivua na kuliweka kando' je alikuwa akiimanisha nn kipindi hicho? nadhani sasa tunaanza kupata baadhi ya majibu.

   
 10. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 659"]
  [TR]
  [TD] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tuiache Zanzibar iende kwa amani

  Innocent Nganyagwa
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent, colspan: 2"]
  Wasiliana na Mwandishi
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  [/TD]
  [TD="width: 110, bgcolor: transparent"] +255 752 227 594
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  [/TD]
  [TD="width: 110, bgcolor: transparent"] Tuma barua-pepe
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.
  Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.
  Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.
  Kimsingi, Zanzibar in mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.
  Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena.
  Inashangaza kuwa kwa miaka sasa Zanzibar imekuwa ikipaza sauti kuwa hairidhiki na jinsi Muungano unavyoendeshwa. Lakini, wahusika walichokifanya, na ambacho wamekuwa wakiendelea kusisitiza kukifanya, ni kiini macho walichokipa jina la kutatua kero za Muungano.
  Kinachowafanya waonekane kuwa ni majuha ni kuwa kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakiendelea na kiini macho hicho cha kutatua kero za Muungano lakini badala ya kwisha, kero zimekuwa zikiongezeka.
  Ajabu ni kuwa wanaonekana kuwa hawaoni kuwa kero zinaongezeka badala ya kupungua licha ya juhudi zao za kushughulikia kero za Muungano.
  Kwangu mimi, ilichokifanya Zanzibar mpaka hivi sasa ni njia za kuonyesha kistaarabu kuwa hairidhishwi na Muungano kwa sababu Wazanzibari wanaamini kuwa hauzingatii masilahi ya Zanzibar. Na walichokifanya wahusika ni kutumia nguvu kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kujiamulia mambo yao.
  Walianza kudai kwa maneno tu, wakaonekana hawana hoja, wakakataliwa. Kwa kuwa walidhamiria kuendelea kudai kile wanachoamini kuwa ni haki yao, wakaanza kufanya baadhi ya vitu kwa vitendo.
  Wakabadilisha sheria kadhaa ambazo kimsingi zinakiuka kabisa makubaliano ya Muungano kama ilivyopo sasa. Walipoona upande wa pili haujashtuka, wakaamua kubadili na Katiba kabisa. Lakini, inaonekana bado wahusika hawaelewi hawa jamaa wanataka nini.
  Kitakachotokea sasa, sidhani kama ni kosa la Wazanzibari kwa sababu kama ni onyo walishalitoa na wakadharauliwa.
  Upo msemo kuwa paka akibanwa kwenye kona, anaweza kugeuka kuwa chui. Hilo ndilo litakalotokea kwa Zanzibar. Kwa sababu imebanwa sana katika azima yake ya kutaka Muungano ambao una masilahi kwake, sasa itageuka kuwa mbogo kweli kweli. Na dalalili zimeanza kuonekana.
  Zipo chockochoko za chini kwa chini ambazo zinawahusisha watu wa kawaida tu hivi sasa. Wapo watu wenye asili ya Tanzania Bara huko Zanzibar ambao wameanza kunyanyaswa na watu wa kawaida tu wa Zanzibar.
  Kwa maelezo yanayotolewa, inaonyesha kuwa hilo ni suala la uhalifu wa kawaida tu ambao hata Tanzania bara upo, ingawa haulekezwi kwa Wazanzibari.
  Lakini kwa wanaotaka kukiita kitu kwa jina lake halisi wanaelewa fika kuwa chokochoko hizi zina uhusiano ya kutoridhishwa kwa Zanzibari katika masuala ya Muungano. Wahusika hawataki kulikubali hilo lakini hiyo haibadilishi ukweli wa suala hilo.
  Kwa kuwa tumeamua kuficha maradhi, tusubiri kifo kituumbue. Naamini kuwa Zanzibar haitachoka wala kuacha kudai haki zake ndani ya Muungano. Na kwa jinsi mambo yalivyo, wahusika wataendelea kukataa kutekeleza matakwa hayo.
  Kwa kuwa suala hili limeshafika kwenye ngazi ya wananchi, ambao wameamka baada ya kuona kuna viongozi wao wengi tu ambao wana mawazo kama yao, tusitarajie kuwa litakwisha hivi hivi.
  Nadhani wahusika wana hofu ya kuvunjika kwa muungano. Lakini wafahamu kuwa kuvunjika huko kwa Muungano kunaweza kuwa ndio suluhisho la kujenga Muungano mwingine utakaokuwa imara kwa sababu utajengwa chini ya maridhiano ya pande mbili zikikubaliana kuungana.
  Lakini, kuna uwezekano mwingine kuwa ni kweli Zanzibar inabanwa sana kiuchumi ndani ya muungano na hivyo kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuisaidia ikajitanua. Itaisaidia pia Tanganyika iwapo itakuwa na jirani tajiri.
  Kuendelea kulazimisha Muungano huu kutatuletea maafa hapo baadaye. Imeshajidhihirisha kuwa Wazanzibari hawataacha kudai haki zao mpaka wazipate.
  Na itafika wakati Watanganyika nao watakapochoka na chokochoko hizo na wao kuamua kuanza kudai haki zao kwa hila na kwa nguvu. Sijui kama wahusika watakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na Watanganyika na Wazanzibari watakapoamua kudai haki zao kila mmoja kivyake.
  Kuna nafasi adhimu ambayo viongozi wetu wanataka kutukosesha bila sababu za msingi. Kwa mtu anayepima upepo, atagundua kuwa watu wengi hawaridhishwi na aina ya Muungano uliopo. Na kwa hakika kabisa, miongoni mwa watu hao ni viongozi wetu wengi tu.
  Tatizo ni kuwa waliopo madarakani hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kuwa ndio walioshiriki kuua Muungano. Wana hofu kuwa Zanzibar ikiruhusiwa kutoka basi Muungano utakuwa umekufa. Ile fursa kuwa kuondoka kwa Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuunda Muungano imara wala hawajaiona.
  Wamejawa hofu ya kihistoria iliyopatia upofu wa masuala dhahiri kuwa kwa kulazimisha Muungano, eti tu kwa sababu ulianzishwa na waasisi wa taifa, watakuwa wanadumisha utaifa. Lakini kama wakiamua kufungua macho, watabaini kuwa wanachokifanya kinaua utaifa.
  Kama nilivyoeleza awali, Zanzibar haiwezi kuendelea kuvumilia kulazimishwa kuwepo ndani ya Muungano. Itafika mahali itageuka mbogo na kulazimisha kile inachokitaka. Itakuwa vigumu sana kuzuia na kudhibiti hali ya mambo wakati huo.
  Kama tunataka salama, ni heri tukaiacha Zanzibar iondoke kwenye Muungano sasa hivi kwa amani na utulivu, nasi tutabaki salama huku tukiwa na uwezekano wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu zaidi.
  Lakini iwapo tutasubiri mpaka Zanzibar, au hata Tanganyika, ikaamua kujiondoa kwa nguvu, hatutabaki salama na wala hakutakuwa na uaminifu uliobakia wa kuwa msingi wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  By (InnocentNganyagwa) mtafiti wamaswala ya sanaa
  Chozo Tanzaniadaima
   
 11. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80

  Jiulize ni kwa nini Karume aliona aungane na Tanganyika haa mwaka haujaisha tangu mapinduzi yafanyike.


  Ile nchi haitawaliki kama Zanzibar huru. Mtabisha lakini mtajuta
   
 12. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Abdulahsaf.
  Umeandika kwa mpangilio mzuri na weledi wa hali ya juu.
  Kikwete anashindwa kutambua kuwa;
  1. Muungano ni makubaliano ya nchi mbili.
  2. Wananchi wa kila upande (nchi), wana haki ya msingi ya kujadili muungano wakati wowote.
  3. Muungano si swala la kulazimisha.
  4. Huweze kuandika katiba ya 'TANZANIA', pasipo KWANZA kuujadili muungano unaounda hiyo Tanzania.
   
 13. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Watanganyika tumeamua kupoteza uhuru wetu ili kuwahifadhi wa Zanzibari. Kama hamuwezi kutushukuru, basi angalau msitutukane. nchi yenu haiwezi ikadumu kama nchi huru kwa muda mrefu
   
 14. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  'Nchi yenu haiwezi kudumu'. Wewe umekuwa Mungu?
  Tatizo la sisi waTanganyika ni kama makondoo au mang'ombe.
  Je, wewe huoni kama muungano una matatizo? Afu mwanaasha anakwambia hakuna kujadili muungano kwenye katiba mpya, sasa huo si uendawazimu...
  Wake up man, let straightening this matter out, you have to think BIG, usiwe na akili za magamba kama Nepi..
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kiukweli nina wasiwasi na afya ya huu muungano hapo siku za usoni. Na viongozi toka visiwani wana unafiki mkubwa sana juu ya hili. Wanachowaza wanazanzibari ndicho wanachowaza viongozi wao
   
 16. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Kwa chokochoko izi za wazanzibar ningekuwa na mguu mkubwa haki ningekipiga teke kisiwa chao kikawa mbali nasi hawa mda wote ni chokochoko wameweka mbele pia hawa ni walalamishi sana
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  unaongea unafiki mtupu. kama wewe una uchungu na nchi hii ungekua mstari wa mbele kupambana na wezi na wala rushwa wanoiba rasilimali za nchi yetu!
   
 18. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama Tanganyika ishakua koti na sasa hamuihitiji? hamjui kuwa hilo koti limewakomboeni kutoka kwa mnyama sultani na kuwalisheni mpaka mmenona sasa mnaliona labana mmenona sana eeh? mkirudishwa mlikotolewa na Tanganyika? nyinyi hamjawahi kuwa huru wala kuwa nchi.
  Wazanzibari wanabweteka tu utafikiri Nyerere alishindwa kuwaingiza moja kwa moja kwenye Tanzania moja ya serikali moja na hiyo ndio dawa tu, hamna cha kutulipa tuwaruhusuni muondoke, na haturusu adui azaliwe katika bahari yetu. muungano utabadilika na kuwa jamhuri moja ya tanzania tu.
   
 19. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umenena. Ndiyo maana braza Ben aliwatwanga kisawasawa. Hawa jamaa wana akili mgando, hawajui muungano ukivunjika watapoteza?`Ila ninavyofahamu muungano kamwe hautakuja kuvunjika kwani walio upande wa muungano ni wengi zaidi kuliko hao majuha wachache wenye itikadi za kidini!
   
 20. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tena jinsi walivyo waislamu? Ni nchi chache sana duniani za kiislamu zenye demokrasia, nyingi zinatawaliwa kwa udikiteta. Wajaribu waone. Mfano halisi ni Saudi Arabia=Hakuna mwanamke kuendesha gari, ukionekana unampenda yesu basi unahukumiwa kufa (wakati tz ya leo tunao uhuru wa kuabudu). Mfano mwingine ni Pakistani=Ukikiri Jina la Yesu Kristo basi unahukumiwa kifo (mfano juzijuzi kuna mwanamke kahukumiwa kifo na ma imamu wa misikti walishukuru kweli hukumu hiyo). Kwa ufupi zanzibar ni msitu uwakao, muda wowote wakijitenga basi wajue wameanza safari ndefu isiyokuwa na amani. Kwani kwa hali ya sasa hakun kiongozi ambaye ni dikiteta kama ilivyo huko ulikoanzia uislamu.
   
Loading...