Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine 19 leo zimetoa taarifa ya pamoja kuwataka watu wenye mamlaka nchini Afghanistan kuhakikisha usalama wa wanawake na wasichana nchini humo.
Taarifa hiyo imetolewa wakati ambapo hofu inaongezeka kwamba Taliban itautumia ushindi wake wa hivi karibuni kuwaondolea maelfu uwezo na kuwa na hali ya kutojiamini
Jumuiya ya kimataifa imesema ina wasiwasi kuhusu wanawake na wasichana wa Afghanistan, haki yao ya kupata elimu, kufanya kazi na uhuru wa kutembea. Jumuiya hiyo imesema iko tayari kuwasaidia kwa msaada wa kibinaadamu kwa kuhakikisha sauti zao zinasikika.
Wakati huo huo, takriban watu watatu wameuawa leo na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya wanamgambo wa Taliban kufyatua risasi wakati wa maandamano kwenye mji wa Jalalabad.