Jumuiya ya kimataifa haioni kama tunaonewa?

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,336
21,434
Tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani,imeonekana kufanya kazi ya kuzuia wanasiasa wa upinzani wasiendeshe shughuli zao za siasa za majukwaa kwa kisingizio cha usalama mdogo,baada ya uchaguzi mzee wetu alitaka kuzunguuka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha mahaba na kumpatia kura lakini kupitia waziri mkuu lilitoka tamko kusitisha shughuli zote za mikutano ya kisiasa mpaka hali ya usalama itakapo kaa sawa.

Sasa hapa ndipo ninapoona kama jumuiya ya kimataifa kama nayo imetutenga na tunayofanyiwa ni sawa hapa kuna mabalozi wa ulaya,baba wa demokrasi amerika, lakini hawatoi tamko lolote kukicha wanakwenda ikulu,pili suala la bibi tulia kuanza kuwanyanyasa wabunge wa viti maalumu upinzani akaona haitoshi akabana upinzani wote na kuwafungia vikao,tatu kuzuiwa kwa mahafali ya chaso,kubwa zaidi ni hili tamko la mwisho raisi alilopiga msumari kuwa hakuna kufanya shughuli za kisiasa wakati vyama vya siasa kazi yake ni siasa.

Ina maana jumuiya ya kimataifa haioni,mabalozi wa kupigia kelele demokrasi au ni sawa upinzani kuonewa ili hali jumuiya za kimataifa zipo?
 
Hizo jumuia za ulaya kwetu ni sawa na wewe na nyumba ya jirani yako mkuu, kuna mahali huwezi kufika, mara ngapi tunaona majirani wanapiga wake zao na tunauchuna kwa kisingizio kuwa hayatuhusu..........nadhani ndivyo ilivyo kwa hata hizo jumuia, cha msingi ni Mtanzania mwenyewe kuamua hatima ya maisha na Taifa lake, hizi ndio malipo za Kanga na kofia.
 
Tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani,imeonekana kufanya kazi ya kuzuia wanasiasa wa upinzani wasiendeshe shughuli zao za siasa za majukwaa kwa kisingizio cha usalama mdogo,baada ya uchaguzi mzee wetu alitaka kuzunguuka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha mahaba na kumpatia kura lakini kupitia waziri mkuu lilitoka tamko kusitisha shughuli zote za mikutano ya kisiasa mpaka hali ya usalama itakapo kaa sawa,sasa hapa ndipo ninapoona kama jumuiya ya kimataifa kama nayo imetutenga na tunayofanyiwa ni sawa hapa kuna mabalozi wa ulaya,baba wa demokrasi amerika, lakini hawatoi tamko lolote kukicha wanakwenda ikulu,pili suala la bibi tulia kuanza kuwanyanyasa wabunge wa viti maalumu upinzani akaona haitoshi akabana upinzani wote na kuwafungia vikao,tatu kuzuiwa kwa mahafali ya chaso,kubwa zaidi ni hili tamko la mwisho raisi alilopiga msumari kuwa hakuna kufanya shughuli za kisiasa wakati vyama vya siasa kazi yake ni siasa.
Ina maana jumuiya ya kimataifa haioni,mabalozi wa kupigia kelele demokrasi au ni sawa upinzani kuonewa ili hali jumuiya za kimataifa zipo?
Walilie upate ukimbizi wa kwenda huko huko, ukapate butamu!
 
Donald Trump ndiye atakuwa Rais wa Marekani. Sijui mtaenda kulia lia wapi kwa maana dunia sasa inawataka marais wa aina ya Magufuli
Trump amesema wazi kuwa Africa needs to be recolonized. Anasema wananchi wa kawaida wa Afrika wanagandamizwa na viongozi madikteta Waafrika wenzao. Maana yake ni kuwa Afrika inahitaji viongozi wazungu waje wawatawale Waafrika ili kuwalinda wananchi wa kawaida wanaonyanyaswa na watawala wao. Ameenda mbali na kuwataja baadhi ya watawala wa Afrika ambao yeye Trump akiwa Rais, lazima awachukulie hatua. Jambo la muhimu ni kuangalia na sisi tusiingizwe kwenye hiyo orodha ya tawala dikteta.

Kwa ujumla ukiangalia utawala wa Afrika, Trump yupo sahihi sana. Ni wapi Afrika kuna utawala mzuri? Kwa fikra zangu, nadhani ni Botswana na South Africa tu. Nchi nyingine zote za Africa, tawala zake zinapishana tu kwa kiwango cha ubovu. Wengine wamewapa uwaziri wake zao, wengine wamewapa ukuu wa majeshi watoto wao, wengine wamewapa ugavana wa benki kuu watoto wao, wengine wamewapa uwaziri wa mafuta watoto wao, etc. Huu ujinga upo wapi zaidi ya Afrika?

Kwa maslahi ya wananchi wa kawaida na wanaopigania demokrasia na utawala bora, itakuwa ni jambo jema sana Trump akiwa Rais. Huenda atasaidia kupambana na tawala dhalimu za Afrika. Afrika ipo jehanamu iliyotengenezwa na watawala wake. Tatizo la Afrika siyo umaskini bali ni udikteta. Udikteta unazuia mawazo mapya, unazuia mawazo ya maendeleo, na unaua vipaji vya uongozi.
 
Back
Top Bottom