Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya

we fox sijajua hasa kwa nini unatetea upuuzi but sikulaumu sana ndo kawaida yenu.

Unanshangaza! upuuzi upi huo nilioutetea? au huzisomi post zangu? ikiwa wewe unamtetea mzinzi halafu mimi nnamponda sasa ni nani anaetetea upuuzi hapo? Ikiwa wewe unatetea kiongozi anaevunja amri ya mahakama halafu mimi nnamponda sasa ni nani anaetetea upuuzu hapo? hebu kuwa mkweli japo kwa nafsi yako. Usijisute mwenyewe, unanini wewe?
 
wachungaji wenyewe mnaowatetea si ndiyo hawa? hebu oneni huyu hapa chini, watashindwa kuuza madawa kweli?B]BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz NI SIKU ZA MWISHO!!?? MCHUNGAJI KKKT AFUNGWA JELA MVUA SITA KWA RUSHWA YA NGONO...
[/B]

Hakuna kutetea mkuu. Everybody(haijalishi dini, jinsia, kabila, utaifa etc) anaweza kufanya kosa. Tunachoomba ni evidence sio kuropoka. Na zaidi ya hapo tunahitaji vitendo zaidi na sio mashairi au mipasho kwani mahakama na polisi si ndio zimewekwa kwaajili hiyo? Whats the use of keeping those names by the way? Apeleke mahali husika!!
 
Haya soma hapa chini....

JK awapasha viongozi wa dini
• Asema wapo wanaouza dawa za kulevya

na Stephano Mango, Songea

RAIS Jakaya Kikwete, amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali kuidhibiti biashara hiyo haramu.

Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga wakati wa ibada maalumu ya kupewa daraja la uaskofu na kusimikwa kwa askofu wa jimbo hilo, Mhashamu John Ndimbo, katika kanisa la kiaskofu la Mtakatifu Killian iliyohudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa.

Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakishiriki kufanya biashara hiyo ya dawa za kulevya kwa kuwatumia vijana ambao huwafanyia mipango ya kuwatafutia hati za kusafiria (Passport) kwenda nchi za nje.

Badala yake Rais Kikwete amewataka viongozi hao nchini kuikemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola katika kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaoifanya ili wachukuliwe hatua za kisheria.

"Inasikitisha sana na kutisha, biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili kwani baadhi yenu tumewakamata.

"Kwa kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususan vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi," alisema Rais Kikwete.

Ameyaomba pia madhehebu ya dini nchini kuweka mipango endelevu ya maendeleo ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika mipango yao ya kimaendeleo ili kuisaidia jamii katika ushindani wa soko la ajira. Alieleza kuwa kutokana na wananchi wengi kukabiliwa na tatizo kubwa la ajira ni vyema sasa serikali kwa kushirikiana na madhehebu ya dini kujikita zaidi katika kujenga vyuo vya ufundi ambavyo vitasaidia kupunguza kero iliyopo ya ukosefu wa ajira hususan vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.

"Kufanikiwa kwa viongozi wa dini katika shughuli za kimaendeleo ni faraja kwa serikali iliyo madarakani na Watanzania wote kwa ujumla," alisema Rais Kikwete.

Awali Rais wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki, Tanzania, Askofu Yuda Thadei Ruwa'ichi, aliiomba serikali kuwa makini wakati wa kuandaa bajeti ya nchi ambayo inatarajiwa kupitishwa bungeni hivi karibuni.

Alisema bajeti hiyo ni vyema izingatie maendeleo ya Watanzania ambao wengi wao ni maskini. Aliishauri pia serikali kudumisha amani na utulivu nchini kwa kuhakikisha wakati wote vitendo vya vurugu havipewi nafasi kamwe na kwamba kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na serikali na Watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, dini au ukabila.

Naye Askofu Ndimbo baada ya kusimikwa alitoa shukurani zake kwa Rais Kikwete na waumini wa jimbo hilo na kuahidi kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Askofu huyo alisema kuwa kazi yake kubwa ni ya kuwachunga kondoo wa Mungu (waumini) pamoja na kuwahamasisha kujikita katika kilimo cha kisasa ambacho kitawasaidia kupunguza ukali wa maisha.

source: Tanzania Daima 6th June 2011

Soma wewe halafu unioneshe huo udini wa Kikwete uko wapi hapo? unanini wewe? au kwa kuwa Kikwete si mkristo ndio kawa mdini? Basi kwa hilo ni kweli kabisa, na si yeye tu, waIslaam wote tu wadini kwa dini yetu tena sana tu. Haina upuuzi ati, unafikiri sie tunaoana wa jinsia moja kama wachungaji? au tunazikiuka sheria tunazosomea kama yule aliyezikiua za kanoni akenda kuoa na kuongeza hawara? hataaa, hatupo hivyo kabisa. Sisi ni wadini kweli kweli tena wala hatuna kificho wala kisingizio.
 
SOURCE;MWANANCHI


Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa
Boniface Meena
JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT), imempa Rais Jakaya Kikwete saa 48 ikimtaka awataje hadharani viongozi wa madhehebu ya dini aliosema wanahusika na biashara ya kuuza dawa za kulevya na kwamba asipofanya hivyo itakuwa ni aibu kiongozi huyo wa taifa.

Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa alisema hayo jana wakati jumuiya hiyo ilipokuwa ikitoa maazimio ya Mkutano wa 45 wa Halmashauri Kuu ya jumuiya hiyo.Askofu Mokiwa alisema kauli ya Rais Kikwete imewasikitisha kwa kuwa amewahusisha viongozi wote wa dini jambo ambalo si zuri mbele ya jamii.

" Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na serikali," alisema Mokiwa.Alisema wanategemea Rais Kikwete atafanya hivyo na kinyume chake atakuwa hajawatendea haki wananchi.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, juzi kwenye ibada maalumu ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini akiwataka kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya, badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kudhibiti biashara hiyo haramu.

Alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanyia mipango vijana kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa ajili hiyo.

“Inasikitisha sana na kutisha. Biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata,” alisema.

Msimamo juu ya Katiba Mpya

Akisoma tamko lao baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu wa 45, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula alisema jumuiya hiyo imeitaka serikali kusimamia kwa umakini suala la Katiba Mpya hasa katika ukusanyaji wa maoni.

Alisema kuwa ukusanywaji huo wa maoni kwa wananchi na makundi yote ya kijamii ni muhimu ukafanywa na chombo huru.

"Kazi hii isiharakishwe na wala isicheleweshwe. Yafaa iwe imekamilika mapema ndani ya muda wa kadri kabla ya kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema.

Askofu Kitula alisema kuwa serikali inapaswa kuangalia ufa uliopo kati wananchi wa kawaida na wale wenye nacho kwani unazidi kupanuka na kuibua matabaka."Hali hii inasababisha malalamiko miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yetu. Malalamiko na ukweli huu umechukuliwa na wadau wa vyama vya siasa kufanya maandamano ambayo yamekuwa yakiwavutia wananchi wengi."

Alisema hali hiyo inachangia hali ya kisiasa kuwa tete hasa ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani ambako bei ya mafuta iko chini zaidi ya Tanzania na nchi hizo zinapitisha mafata hayo hapa."Serikali isahihishe jambo hili pasipo kuchelewa. Vyama vyote vya siasa vihamasishe wananchi kuleta maendeleo bila kujadi itikadi za vyama vyao."

Askofu Kitula alionya kuhusu siku za ibada na kutaka ziheshimiwe na watu wote na mamlaka zote. Alisema ni vyema serikali isipange matukio muhimu ya kitaifa kama uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa siku za ibada.

"Kadhalika, wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu, vya elimu ya juu na taasisi zake wasiwapangie wanafunzi mitihani au mazoezi ya vitendo siku za ibada," alisema Askofu Kitula.

CCT yazungumzia tiba asilia

Kuhusu tiba asilia, CCT imetoa wito kwa serikali kusaidia katika utafiti na matokeo yake yawekwe bayana ili kuwaondolea wananchi hofu ikiwa ni pamoja na huduma zitakazothibitishwa kupatikana mahali pengine nchini.

"Kadhalika, serikali isimamie utunzaji wa mazingira ili miti na mimea mingine yenye vyanzo vya tiba asili istawi na kupatikana muda wote," alisema Askofu Kitula.Aidha, CCT imesisitiza msimamo wake kutaka mambo ya kuendesha shughuli za dini yatenganishwe na mamlaka ya kuendesha nc
 
wachungaji wenyewe mnaowatetea si ndiyo hawa? hebu oneni huyu hapa chini, watashindwa kuuza madawa kweli?




BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz NI SIKU ZA MWISHO!!?? MCHUNGAJI KKKT AFUNGWA JELA MVUA SITA KWA RUSHWA YA NGONO...


MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka sita jela mwalimu wa shule ya sekondari ya Pomerini wilaya ya Kilolo mkoani hapa Michael Ngilangwa mchungaji wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Njombe kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake.

hii ni kwa mujibu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima tarehe 6/6/2011

Hay na hiyo semeni, ngoja niwaletee nyingine na yenyewe mseme!
 
Na hii jee, nayo mtaikataa?

Mchungaji akutwa na viungo vya Albino


Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste lililopo Idiwili Kata ya Iyula, wilayani Mbozi anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokuwa yakiuzwa Sh milioni 30.

Cosmas Mwasenga (39) alikamatwa Februari 13 mwaka huu akiwa na Luseshelo Mwashilindi ambaye inadaiwa alikuwa ameyahifadhi nyumbani kwake mabaki hayo. Mabaki hayo ambayo Polisi inahisi kuwa ni ya albino, ni vipande vinne vinavyosadikiwa kuwa sehemu ya mikono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Mlowo, Mbozi. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Zelothe alisema Februari 12 mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu Mlowo, wana vipande vya mabaki ya mwili wa mwanadamu vinavyosadikiwa kuwa ni mabaki ya mwili wa albino.

Source: Rudisha Rasilimali kwa Wananchi: Mchungaji akutwa na viungo vya Albino
 
Christian Council of Tanzania (CCT) jana imempa raisi Jakaya Kikwete masaa 48 kuwataja viongozi wa dini JK aliosema wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya. Vinginevyo atashusha heshima yake kama kiongozi wa nchi. Chama hicho kimetoa tamko hilo kwa Raisi baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu shutuma za Raisi kwa viongozi hao kujihusisha na biashara hiyo haramu.

Wakati akihutubia umati uliofika kushuhudia kusimikwa kwa Askofu wa Mbinga John Ndimbo, Raisi JK aliwataka viongozi wa dini kuisaidia serikali kupigana vita dhini ya madawa ya kulevya, na kusema kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanafanya biashara hiyo haramu. Raisi JK alisikika akisema kwamba baadhi ya viongozi wa dini huwatumia vijana kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Issue ilikuja pale CCT walipokuwa wanawahabarisha wanahabari kuhusu mkutano wao mkuu uliofanyika Dodoma siku ya Jumatano na Allhamisi wiki iliyopita.
Dr Mokiwa alisema kwamba Kikwete kushindwa kuwataja kwa majina viongozi hao wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya itaangusha uongozi wake kwa kutokuwa makini katika kuongoza nchi na watu wake"

“Tunategemea Raisi kuwa muwazi zaidi na kuwataja wahusika; kama ana data za uhakika ni bira awe muwazi ili sheria ichukue mkondo wake...hakuna sababu ya kuuficha ukweli kwa wananchi,” alisisitiza.
Aliongeza kwamba itakuwa ni muhimu zaidi kuwajua viongozi hao badala ya kutoa shutuma za jumla kwamba viongozi wa dini wanahusika na madawa ya kulevya.

Dr. Mkoliwa alisema kwamba wanaheshima kubwa sana kwa Raisi na kwamba statement zake hazijachukuliwa kirahisi rahisi. Anasema Mr Kikwete hatakiwi kuogopa kuwataja wahusika maana chama chao kitakuwa naye katika kuhakikisha haki inatendeka.
 
Acha ubishi wa kipumbavu, hapa tunajadili hotuba ya Mbinga na sio kile unachotaka wewe.Mwanzisha mada ameanzisha kutokana na hotuba ya Mbinga wewe unatuletea hotuba ya Nyamagana ; are you crazy?. If you're not informed siyo lazima kuchangia unatu chefua bora uachane na mada uendelee na shughuli zako .

Wewe weka hiyo ya Mbinga au huyo muanzisha mada, mimi nimekuonesha maneno ya JK mwanza akiongea na vinara wa dini zenu.
 
Rais wetu mpendwa Mh. Jakaya Kikwete hana uwezo hata chembe ya kutaja kwa sababu aliropoka kwa bahati mbaya maana ndo kawaida yake, hata mwaka 2006 alisema ana majina na vinara wa madawa ya kulevya na akasema atawashughulikia na wananchi wasubiri kidogo, mpaka leo bado tunasubiri.
mwaka juzi katika hotuba zake za mwezi alisema kuna viongozi wa ufisadi mbali na kina mramba, yona na mgonja, watafikishwa mahakamani kabla ya mwisho wa mwezi october 2009 au november 2009 lakini mpaka leo kimya, walaaa hakumbuki.

kama hayo machache tu wala hakumbuki kama aliwahi kukurupuka kuongea hayo sembuse viongozi wa dini, jamani msifanye mimi nicheke hali mbavu zinauma

Imewauma enhh? na bado, yeye si kisha sema sasa si mnataka majina? ngoja kidogo vijana wake wawaletee data, sijui mtasema nini hapo? mtaachana na hao wachungaji au?
 
Huyo Mokiwa kama nani wakumpa Rais masaa? hana adabu kwa Rais huyu? si akachunge kondoo zake waliopotea.
 
Yes, he must mention them!! Tuache usanii usio na maana. Rais mzima anakuwa msanii. Well, tusubir hayo masaa 48 yapite ili tujue mbivu na mbichi
 
Ndiyo askofu dr. Mokiwa, udaktari wako siyo wa heshima wala wa kupewa njiani hivyo umeopnesha usomi na ukomavu wako - ni lazima awataje.
 
kama akishindwa kutaja basi lengo lake litakuwa na kuchafua dini na si vinginevyo na hata heshima/mchango anaopewa ktk hafla za kikristo zinazofanyika hastahili tena maana anataka kusababisha migogoro baina yetu
 
Maneno 2 hayatoshi, kishasema sanaaa la msingi ni kuwapeleka mahakaman si kulalamika tuuu! Vitendo ni muhim bana.
 
hivi huyu mzee ana washauri kweli au anakurupukaga tu kusema vitu??? sasa atakoma na kuropoka ropoka.yaani rais anakuwa kama katibu tarafa bwana

huyo ndio mkweree.com , tuliwaonya kua huyu simtu wa kuaminika mkakataa ! Ndio hayo sasa.
 
Back
Top Bottom