SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,328
- 2,217
Mimi sikuongea, nimeweka hiyo habari inayoongewa. Usitie maneno ya mwingine kinywani mwangu, na source nimeiweka, heee babuwee unanini?
FF!
Vizuri umeweka hotuba ya Raisi kuthibitisha hakusema vibaya na kwamba ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa kidini wanajishughulisha na hiyo biashara.
Sielewi kuhusu mahusiano ya hotuba uliyoiweka ambayo inasema ni ya Nyamagana - Mwanza wakati muanzisha hoja anasema Raisi alitoa hotuba Mbinga - Songea.
Hebu fafanua hapo tukuelewe na kama vipi hebu weka hiyo hotuba ya Mbinga tuone ili tuweze kujua Askofu Mokiwa kapata wapi uwezo wa kumdai Raisi awataje hao viongozi.
Kwa mtazamo wangu sioni kosa kwa Raisi kuiomba jamii na taasisi zote nchini kusaidiana katika mapambano ya dawa za kulevya na isitoshe hata viongozi wa dini wamekua mstari wa mbele kuwaasa waumini na jamii kwa ujumla kuepuka matumizi ya madawa hayo.
Sasa hizo kauli tata za kutajana zimetokea wapi(chanzo)???
Kwa yeyote mwenye hiyo hotuba ya Mbinga tunaomba atuwekee hapa tuione ili tuweze kupima pia ukweli wa jambo hili.
.